Usalama wa familia yetu ni muhimu

Usalama wa familia yetu ni muhimu

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Nisikilizeni, Faru J ni kaka yenu haijalishi alighafirika vipi. Rasmi na wausia sasa, ni muhimu aheshimiwe na thamani yake apewe.

Usalama wa familia yetu ni muhimu kuliko magomvi yetu ya ndani. Na kama mnavyoshuhudia, Ukoo wa mwendazake wa kule Ilaki kwa hivi karibuni unaelekea kutupindua ki Utawala. Lazima kitu kifanyike kuzuia mwendelezo wao. Lazima Ufalme wetu urejee.

Mwanzo wewe umejiharibia mwenyewe kwa kutokuzingatia masharti ya mwenendo na ndiyo maana 001 kakushtukia na kukutupa nje ya Boma lake. Nilikupa maelekezo ujikite kwa chekechea wake ajabu ukaanza kumuonyesha chekechea yule mapito yako mlipokuwa Ng'ambo. Kakuchoma sasa na umepigwa marufuku kusogelea kwao.

Domokaya nawe ni walewale tu. Ulishindwa nini kuwa mtulivu hadi uanze kudhihili rangi na uelekeo wako?! Ona sasa pamoja na Mwanzo hamtakiwi kwenye Boma la mu-Ilaki.

Sasa nisikilizeni kwa makini, vita iliyopo mbele ni kubwa! Uwezekano wa Ukoo wetu kupotezwa siyo tetesi tena bali ni bayana. Nimempa maelekezo ya nini joka la kimbisa akafanye kwenye ule Mkutano wa hadhara. Joka akilianzisha na wewe chekechea wa Ki imani udakie haraka. Ninyi wapwa na wajukuu kazi yenu iwe kudakia na mapambio juu. Binti mu Ilaki atanitupia mpira na mimi nitasawazisha bao.

Habari njema yule mla nguruwe bandani ameomba ruhusa arejee kwao. Nami sasa nitahahikisha kaka yenu Faru akawe pale.

Endapo Faru J akiwa pale, ni rahisi Ufalme wa Ukoo wetu urejee. Ya yule mla Sato si mnayakumbuka wanangu? Mtemi wenu naelekea kibra, sasa ni muhimu ni hakikishe Ufalme wetu urejee kabla ya 3020.

Basi, nguvu zote tuzielekeze kwa Faru J.
 
Post ina akili nyingi sana hii.
Kama hafungui masikio hakika 3020 mbali kwake
 
Kwanini chama chenu kinaogopa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi?
 
Back
Top Bottom