Usalama wa raia na mali zao

Nino

Member
Joined
Jun 21, 2007
Posts
38
Reaction score
1
Habari?

Tarehe 10 Machi nimeibiwa yuro 2000 na mwanamke, Suzy, alijifanya mchumba wangu huko Unguja baada ya kugombana nami. Nilimshtaki katika kituo cha Ng'ambo, Unguja, ambapo anaishi. Aliitwa kituoni na amekuja na wanasheria wake na amejitetea kwa uongo tu.

Mimi nina ushahidi wa wizi na yeye hana kitu! Tulipatana kwenda benki kuchukua pesa zangu siku ya pili. Siku ile huyu Suzy hakukuja! Polisi alimwita tena lakini huyu alithubutu kutojali mwito wa polisi! Aliitwa mara nyingi lakini huyu alidharau polisi. Mwishoni (baada ya siku 10!) Mkuu wa Polisi wa kituo cha Ng'ambo aliamua kuhamishia kesi kituo cha Paje kwa sababu tuligombana kule, ingawa Suzy aliniibia kwa kupitia tawi la Mkunazini la benki CRDB na nyumbani kwake ni Ng'ambo!

Nilipokwenda kituoni kwa Paje polisi walishindwa kumpata huyu Suzy, ambaye aliendelea kutojali miito ya polisi. Polisi wamechelewesha kila kitu mpaka mkuu wa kituo alituambia: "Tokeni msitushughulishe!"

Shemeji ya huyu Suzy ni askari polisi ameingilia na alianza kututisha kwa simu na alisema kwamba yeye ni rafiki ya viongozi wengi kwa hiyo hatuwezi kujitetea!

Ingawa sina hakika kwamba kweli polisi wanajali "Usalama wa raia na mali zao", ninngependa kujua nani anakinga haki na usalama wa wageni au watalii na mali zao? Mgeni au mtalii afanye nini? Watanzania hawapendi wageni na watalii?

Asanteni sana,
Nino V
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…