Usalama wa simu zinapoibiwa, tuwe makini

Usalama wa simu zinapoibiwa, tuwe makini

willzkichaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
422
Reaction score
190
Habari wana jamvi,

kiukweli nimesikitishwa sana na jambo lililonikuta hivi karibuni.
wiki iliyopita nlipoteza simu yangu ya mkononi aina ya SONY Xperia katika mazingira ya kutatanisha.

Hata hivyo ilikua ndani ya daladala nlikurupuka na kutoka haraka baada ya kukumbuka kitu na baada ya dakika 10 nligundua nimepoteza simu hii nliyoipenda na kuhifadhi kila aina ya docuent muhimu ninazozitumia, vyeti vya kuombea kazi vyote na mitandao ya kazi ya kutosha! tuishie hapo kwa hilo.

Iliniuma sana na nlianza fuatilia daladala hiyo na kuipata labda kama ingekua chini au konda ni mwema kanishikia maana sio wana nzengo wote wana roho mbaya, konda alikana na kufanya nizunguke na nlipata abiria wote waliopanda ndani ya dakika chach zile nao walikataa, Mwanza ni ndogo na ukiamua kupata mtu haraka haishindikani. siku hiyo nliahirisha hata upeleka application maana nlighafilika sana.

************POLISI*********
Sasa nikashauriwa kuripoti polisi maana huu mtaaa ulivyo naweza ipata na kushindwa ichukua, ilikua mida ya saa kumi na mbili na polisi nlikuta wakieka makabrasha vizuri wafunge, hawakunipa RB ila waliniambia kama ni 3G niende vodacom tu(mtandao nliokua nautumia). nikafarijika na kuona imeisha!

***********VODACOM*******
baada ya kutoka polisi nlipigaa simu vodacom na kuuliza kama huduma hii ipo, na nlijibiwa kuwa ipo na itapaikana haraka, asubuhi na mapema nlifika vodacom nikiwa na shauku ya kuipata simu yangu niendelee na mambo mengine, kufika na kuuliza nliona sura ya mhudumu inabadilika na akanijibu, nani kakudanganya huyo? ngoja niandike ripoti (anabonyeza kompyuta) kwanini wanadanganya wateja jamani. kha! nlihisi kupigwa ganzi nisiyojua imetokea wapi na hata miguu ikachoka kusogea, kumbe simu ikipotea kama sio samsung au iPhone asee jipange. niliambiwa niende polisi na registration namba za simu nao wanaweza kusaidia labda.

**********SOMO/ONYO**********
sasa ile simu ina uwezo mkubwa na hiyo brand nimeipata kwa rafiki mwenye mishe za simu za nje na ilikua used, hapo ndo kimbembe maana ningekua nimeinunua dukani atleast namba ingekuwepo.

Kosa nlilofanya naona ni kutonakili namba zake pembeni for emergency, na kutoweka appliation za kui track simu.
kutoka vodacom sikukata tamaa ila nlirudi kwenye kompyuta na kujaribu kui track na application kama Airdroid, PlanB na Android device manager na avast ila hakukua na bahati kwani inaonekana ilikua imezimwa kama sio kufutwa kila kitu!
kilichoniuma zaidi ni kuambiwa kua ingekua Samsung wangejaribu,

**********USHAURI*********
kama unatumia simu zenye uwezo mkubwa wa internet jaribu kuweka application za kui track movement zake na kuback up kila kitu (faili, picha na video) itawasaidia msiadhirike kama mimi, na ukiangalia ajira ngumu nlikua nishaitafutia mteja niongezee mtaji. MAJOR PULL BACK! sasa imebidi niendelee kuiweka katika maombi Mungu anisaidie nipate zaidi a hiyo.
Nawatakia Siku Njema.
 
Polisi na vodacom wangekua weledi wangekusaidia ungeipata cyber crime unit ina kila kitu lakini haitumiwi effectively
 
Pole sana mkuu... Uliibiwa makoroboi au pamba road?

Amesema alikua kwenye daladala au sikuelewa...

Halafu voda walifanya uzembe mdogo mi nnavyo fahamu... mitandao ya simu wana uwezo wa kujua ulikua unatumia simu ya aina gani na code zake pia... nakumbuka tusha wah pata kesi kama hiyo lakn mpaka wakusaidie unatakiwa uwe na vielelezo muhimu kutoka polisi
 
If z all about the documents and contacts ts easy as now android is owned by gugo all u can do is sign in with yo Google account on android phone o PC and retrieve them
 
Polisi na vodacom wangekua weledi wangekusaidia ungeipata cyber crime unit ina kila kitu lakini haitumiwi effectively

Yaani utachoka wanavyokaa kama hawana la kukusaidia, kwa hilo suala huduma yao kwa wateja yahitaji maboresho
 
If z all about the documents and contacts ts easy as now android is owned by gugo all u can do is sign in with yo Google account on android phone o PC and retrieve them

Na msisahau ku back up picha and every thing, itasaidia. Pia jaribuni kuitrack simu kwa pc wakati unayo, itasaidia hapo badae
 
Alafu kitu nimegundua sehemu nyingi za kutoa huduma kwa Umma wahudumu waliopo karibia wote wamepata hizo kazi kwa magumashi/rushwa, so mtu unapofika sehemu husika ili upate huduma wahusika huona kama vile unawasumbua, haya ndio madhara ya kuajiri watu wasio wa fani husika sababu ya rushwa tu!
 
Mshana Jr ndugu yangu hao waliopo Cyber Crime sijawahi kujua wanafanya nini, mimi nilikwishawahi wapelekea kesi ya kijinga kabisa ambayo hata mdogo wangu mwenye diploma ya IT nilivyomuhadithia niliona alifanya jitihada ambazo ziliniridisha, lakini wao waliishia kunipiga kelenda, kila siku ya kalenda wanasema lingine na kupiga kalenda tena. Hawajui wanalofanya wale watu.

Polisi na vodacom wangekua weledi wangekusaidia ungeipata cyber crime unit ina kila kitu lakini haitumiwi effectively
 
Katika maisha yangu sidhani kama nitaweza tumia simu nrand nyingine zaidi ya Sony.najua inauma kwakweli mimi juzi nilivamiwa na majambazi ila niliapa hawataichukua niliiwahi nakuitupa darini nusu waniuwe. EX Z bado mwizi hajanibebea kilaini .pole sana mkuu pole
 
Nashukuru, sishangai kwani naelewa uzuri wa Sony. Pole pia kwa kuvamiwa
 
Mshana Jr ndugu yangu hao waliopo Cyber Crime sijawahi kujua wanafanya nini, mimi nilikwishawahi wapelekea kesi ya kijinga kabisa ambayo hata mdogo wangu mwenye diploma ya IT nilivyomuhadithia niliona alifanya jitihada ambazo ziliniridisha, lakini wao waliishia kunipiga kelenda, kila siku ya kalenda wanasema lingine na kupiga kalenda tena. Hawajui wanalofanya wale watu.

Wako kimaslahi zaidi wanachagua kesi zilizonona ndio wanadeal nazo tu
 
Back
Top Bottom