Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
Taarifa kwa vyombo vya habari 14 Julai, 2009
Chama cha Wananchi (CUF) kimefadhaishwa sana na taarifa kwamba maafisa wa Usalama wa Taifa wilaya ya Micheweni, wamekuwa wakiingilia utendaji wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kuwafukuza wananchi wanaokwenda kujiandikisha katika vituo vya kupiga kura, kama ilivyoripotiwa kwenye magazeti ya leo ya Mwananchi na Nipashe.
Tukio hili sio tu kwamba linathibitisha ile kauli ya muda mrefu ya CUF kwamba ZEC inaendesha uchaguzi kwa kufuata maagizo ya Idara ya Usalama wa Taifa, bali pia linapigilia misumari mingine kwenye jeneza la kuizikia demokrasia Zanzibar. Kila mara tumekuwa tukisema kwamba vyombo vya dola ndivyo hasa vinavyosimamia na kuendesha uchaguzi wowote unaofanyika Zanzibar, huku ZEC ikiwa kama ni alama tu ya kuwepo kwa chombo huru kinachoendesha shughuli za uchaguzi. Taarifa zilizokusanywa na waandishi katika vituo vya Wingwi Mapofu, Mgogoni na Kinyasini, zinaonesha kwamba vyombo hivyo vya dola vimekuwa vikishiriki kikamilifu katika kutoa maelekezo ya nini kifanyike katika vituo vya uandikishaji wapiga kura ikiwemo hata kuwazuia masheha wasiongee na waandishi wa habari ambao huwa wanataka kujua usahihi wa madai yanayotolewa dhidi yao.
Itakumbukwa kwamba Usalama wa Taifa ni miongoni mwa mambo ya Muungano na, kwa hivyo, ni idara inayosimamiwa moja kwa moja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kwa mantiki hiyo, hakuna namna yoyote ambayo Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wanaweza kujivua na lawama za kuchafuliwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, maana inaonesha wazi kwamba ama wanaridhia utendaji wa vyombo vilivyo chini ya mamlaka yao Zanzibar au hawajali kile kinachofanywa na vyombo hivyo. Lolote kati ya hayo mawili linamaanisha kwamba wao ndio wanaopaswa kubeba dhamana na lawama za hali ya juu katika jambo hili.
Sisi, CUF, tunachukua fursa hii tena na tena kuwakumbusha viongozi wetu hawa wawili kwamba wao ndio wenye jukumu la kulinda usalama na haki zote za kikatiba za wananchi wa Tanzania. Kisingizio kwamba Zanzibar ina sheria zake za uchaguzi hakitoshi kuviachia vyombo vilivyo chini ya mamlaka yao kuvunja haki za wananchi wa nchi hii. Hakitoshi pia kudharau ukweli kwamba uchaguzi wa Zanzibar unavurugwa na vyombo vile vile ambavyo vilitarajiwa kuusimamia. Hili la kuwanyima wananchi haki ya kuandikishwa na kuweka vyombo vya dola kuhakikisha kuwa haki hiyo haipatikani ni katika mifano halisi.
Wakati tunathamini nafasi ya vyombo vya dola, ikiwemo Idara ya Usalama wa Taifa, katika kuifanya nchi yetu iwe katika amani, umoja na mshikamano, hatukubaliani kabisa na dhana kwamba jukumu la Idara hiyo ni kuhakikisha kuwa wananchi wenye mawazo tafauti ya kisiasa na watawala hawana haki katika nchi yao na kwamba lazima wadhibitiwe kwa namna yoyote ile, ikiwemo hii ya kuwafukuza kwenye vituo vya kujiandikisha kupiga kura.
Pamoja na salamu za Chama.
Imetolewa na:
Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,
CUF
Simu: +255 777 414 112
E-mail: cufhabari@yahoo.co.uk
Weblog: Haki Sawa kwa Wote