Katika gazeti la leo tarehe 4/1/2016 la wananchi kuna habari yenye kichwa kama inavyosomeka hapo juu na kwamba wananchi wengi wamekuwa wakivamiwa mara tu ya kuchukua pesa nyingi benki.
Benki nyingi zimekuwa zikiwabana wateja wasizungumze na simu wanapokuwa benki na hili linatekelezwa kwa nguvu zote.
Huku zikiwasahau wafanyakazi wao ambao wameendelea kutumia simu wanapokuwa kazini na yako matukio mengi yamewahusisha wafanyakazi wa benki.
Swali la kujiuliza hawa majambazi wanapata wapi taarifa za wateja?
Je wafanyakazi wa benki (watunza fedha) wazuiliwe kutumia simu wanapokuwa kazini?