Ni mambo machafu na ya aibu ambayo sehemu ya jamii ya Kitanzania imedumbukia ktk dimbwi la matendo haya! Ukosefu wa maadili, malezi mabaya, utandawazi, kukuso utu na ubinadamu, kutokumuogopa na kumheshimu Mungu na kukosa mapenzi ya dhati baina ya wapenzi wawili ni sehemu ndogo ya sababu ambazo zinawafanya watu kuyatenda mambo haya bila aibu!
Nashauri ifike wakati, watoto wetu wafunzwe yafuatayo kusaidia kupunguza matatizo kama haya ktk vizazi vijavyo.
1. Tuwalee watoto ktk imani ya kufahamu kuwa Mungu yupo, then tuwafunze wamuogope na kumheshimu,
2. Tuwape watoto Malezi bora ya kijamii tukiowaonya juu ya tabia mbaya na madhara yake kwa jamii. Watawezi kubaini na kukataa maovu ukubwani maana tayari watakuwa na msingi mzuri wa malezi
3. Waelimishwe juu ya matumizi sahihi ya teknolojia na madhara yake ktk jamii kujenga na kukuza ufahamu wao
Kwa kizazi cha sasa, kila mwenye uelewa anatakiwa kupinga hali ya namna hii, najua ni kitu kigumu na kitachukua muda ila ipo siku itafika na jamii kubadilika. Tusipochukua hatua na kuendelea kukupambatia stori za namna hii tutakuwa tunaendelea kuwakumbatia watu wenye tabia hizi na kuwatia moyo waendelee na tabia hizi.
Mungu okoa kizazi chetu,
Amin.