KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Sabal kheri waungwana.
Nyakati fulani nilikuwa kwenye kijiwe kimoja tukibadilishana mawili matatu ya maisha na changamoto zake na kuangalia namna gani tunazikabili.
Katika maongezi hayo likaibuka suala mambo ya ndoa kama ilivyo kawaida kuwa na yenyewe ni sehemu ya changamoto kwenye maisha yetu ya kila siku.
Mada kuu ilikuwa namna gani usaliti kwenye NDOA ulivyo kithiri
Wakati tukijaribu kutafakari jambo hilo ndipo jamaa mmoja akaibuka na hoja kuwa mbona hayo sasa hivi ni mambo ya kawaida tu kwenye jamii zetu, kwamba hayo mambo (ya kutoka nje ya ndoa) ni ya kawaida tu isipokuwa kikubwa ni heshima tu akiwa anamaanisha kuwa ni kukufanya usijue tu au afanyie mbali yaani heshima ni kutokukuonyesha.
Maongezi yakiwa yanayoyoma lakini fikra zangu zikaganda kwenye haya maswali kadhaa. Inakuwaje kawaida kwa mke au mume wa mtu kufanya uchafu. Nini maana ya ndoa? Ina maana gani mtu kuingia gharama za kufunga ndoa ikiwa bado atayafanya yale aliyokuwa akiyafanya kipindi hajaoa. Lakini kinachotia hofu ni kwamba jamii imeshaliona kuwa ni jambo kawaida na hakuna anayeshtuka as long as long wewe hujui.
Wanasema kikubwa heshima tu, ni heshima ipi wanayoimaanisha? Utasemaje unamheshimu mtu unayemsaliti? Utasemaje unamheshimu mtu unamuibia mali zake. Utasemaje unamheshimu mtu unayemfanyia unafiki.
Kwa kweli tuendapo si kuzuri na tumeshafikia hatua mbaya. Ndio maana mioyo ya watu inapata ukakasi linapokuja suala la kufunga ndoa, maana haileti mantiki ya wewe kumhudumia ng'ombe lakini mazao ya huyo ng'ombe unavuna na wengine.