USALITI….Mke wa mtu ala kipondo baada ya kufumaniwa akiwa na rafiki wa mumewe chumbani…!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
HUU ni usaliti 100%! Mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Mwanahamisi au mama Daudi, mkazi wa Pugu-Kajiungeni, Dar, amejikuta akipata aibu ya karne baada ya kudaiwa kuingiza mwanaume mwingine chumbani kisha kufumaniwa na mumewe.




MSAMAHA:

Mwanahamisi ambaye ni mke wa mtu akiomba samahani baada ya kunaswa.

Tukio hilo la kufedhehesha lilijiri hivi karibuni, mchana kweupe nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo.
ILIKUWAJE?

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wanandoa hao, mume wa Mwanahamisi aitwaye Mashaka au baba Daudi ana rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Paulo ambaye alidai kusumbuliwa na shemeji yake (mama Daudi) kwa muda mrefu.
Ilidaiwa kuwa mama Daudi alikuwa akimtumia Paulo ujumbe wa mapenzi kupitia simu hadi wakati mwingine kufikia hatua ya kumbana na kumkumbatia pale anapokutana naye njiani.

Ikaelezwa kwamba Paulo alimwambia baba Daudi kuwa alikuwa ameshamtumia zaidi ya SMS 240 za kimapenzi.

Baada ya kuona kero zimezidi huku rafiki yake akimlalamikia kutomuelewa mke wake aliyezaa naye mtoto mmoja ambaye bado hata hajaacha kunyonya, Paulo aliamua kuvunja ukimya na kumuonesha ujumbe anaotumiwa na shemeji yake huyo ili wamkomeshe.



AIBU YA USALITI:

Mke wa mtu pamoja na njemba aliyokuwa nayo wakiwa na aibu baada ya kunaswa live chumbani.


Ilisemekana kwamba baada ya kufanya tathmini ya SMS hizo, baba Daudi na Paulo waliweka mtego huku wakimshirikisha mke wa Paulo ambaye aliwahi kugombana na mama Daudi kwa kitendo cha kumtambia ovyo.

Ilielezwa kuwa baada ya mpango kukamilika huku Paulo akimwambia shemeji yake kuwa amemkubalia, mama Daudi alimuaga mumewe kuwa baba yake ni mgonjwa huko Yombo-Buza, Dar hivyo anakwenda kumuona na siku hiyo atarudi saa 12:00 jioni akijua kuwa kwa mwanya huo ataweza kwenda gesti maeneo ya Ukonga-Mombasa, Dar na Paulo kama walivyokubaliana.

Ilisemekana kuwa baada ya Paulo kuona gesti patakuwa na shida ya kumshikisha adabu mama Daudi, alimshawishi wakutane chumbani kwa mumewe (baba Daudi) ili iwe rahisi kumfumania.

Ilifahamika kwamba ili kusaliti chumbani kwa mumewe, alimpigia simu baba Daudi kujua alipokwenda.

Kwa kuwa baba Daudi alijua mchezo, alimwambia mkewe kuwa amekwenda kufuatilia kitambulisho cha kazi kisha atakwenda Kigogo, Dar kwenye mishemishe nyingine.

Ilidaiwa kuwa majibu hayo yalimfurahisha mama Daudi ambaye alimwalika Paulo chumbani kwa mumewe bila kujua aliwekewa mtego.


KIPONDO:

Mke wa mtu akipokea kichapo baada ya kubambwa.SAA 7:OO MCHANA KWEUPE


Mishale ya saa 7:00 mchana, Paulo aliondoka nyumbani kwake na kuwaacha wafumaniaji wakiwa tayari, alipofika kwa mama Daudi naye akainua simu kumpigia baba Daudi kumhakikishia Mwanahamisi kuwa mume wake harudi muda huo, akamwambia kuwa amekwenda mbali wataonana saa 12:00 jioni.
Ilidaiwa kuwa ili wafaidi mambo vizuri, mama Daudi alimuondoa mtoto wake na mdogo wake kwa kuwapa fedha ya kwenda kulipia kuangalia ‘tiivii' kibandani ili abanjuke na Paulo kwa raha zake.

Nusu saa kabla ya tendo, Mwanahamisi alikuwa ameshasaula nguo zote mwilini ndipo Paulo alipomtaarifu baba Daudi kuwa mchezo tayari anaweza kufumania.
 
Kiukweli ndoa za idini hii zina asili ya mafumaniI na hata kesi nyingi mahakamani ni za upande huu. Povu,jaziba na matusi hazitabadilisha ukweli.
 
Ila maisha ya uswazi yana shida sana
 
Hizi ndoa nyingine full kizungumkuti.....
 
Kuna hati mke wa paulo atakuja kumpa baba DAUDI ili ngoma iwe droo. Maana ataendelea kutambiwa kwamba alishabebewa mume wake
 
Maisha yenyewe magum uswahln,usalit nao washka hatam!dah tatizo ni bei ya mkaa!
 
Mapenzi ya wizi sometime huwa matamu.

Heshima yako rafiki..mapenzi matamu ukiwa na wako bana sio wa mwenzako! haukabwi unavyo kula,yani huna papara! wizi hauna raha kabisa mkuu,au utamu gani ambao unausemea hapo?
 
Heshima yako rafiki..mapenzi matamu ukiwa na wako bana sio wa mwenzako! haukabwi unavyo kula,yani huna papara! wizi hauna raha kabisa mkuu,au utamu gani ambao unausemea hapo?
ndo nimesema sometime mkuu not all the time. but you are right kwamba kizuri ule peke yako.ila jiulize hao wanaaoiba waume au wake za watu kwanini hufanya hivyo au kwani baadhi ya wanadoa huchepuka kutoka njia akuu kama hawafaidi mapenzi ya wizi??
 
ndo nimesema sometime mkuu not all the time. but you are right kwamba kizuri ule peke yako.ila jiulize hao wanaaoiba waume au wake za watu kwanini hufanya hivyo au kwani baadhi ya wanadoa huchepuka kutoka njia akuu kama hawafaidi mapenzi ya wizi??

Sawa Ndugu,nimekupata vilivyo! lakini pia tatizo au chanzo cha michepuko hiyo sio kwamba cha wizi ni kitamu zaidi,nadhani tatizo ni kukurupuka wakati wa kuchagua wa kuoa,matokeo yake ndio small house...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…