Usaliti (simulizi ya kusisimua)

Usaliti (simulizi ya kusisimua)

smartdunia

Member
Joined
Jul 29, 2021
Posts
12
Reaction score
9
Na Smartdunia.


‘’FURAHA NILIYOKUA NAYO TANGU NIKIWA MDOGO,ILIANZA KUFIFIA’’,Jessica alisema huku akifuta machozi kisha akaendelea.

Nakumbuka siku ile, tarehe za mwanzoni mwa mwezi wa saba miaka kumi iliopita,niliamka asubuhi nikiwa nimechoka sana.

"Uchovu wa leo sio wa kawaida kabisa",niliwaza huku nikikiacha kitanda changu taratibu.

Nikamueleza mama yangu kuhusu hali ile lakini nikaambulia kuambiwa eti mimi ni mvivu, eti naanzaje kuchoka asubuhi yote ile, inamaana sitaki kwenda shule? “Nenda kamwambie baba yako huenda atasikiliza huo ujinga wako” mama alisema na kunikatisha tamaa ya kuendelea kujieleza, niliamua kuyaficha moyoni mambo mazito Sana niliyoyahisi usiku ule, nisingeweza kuendelea kujieleza ,Niliingia ndani nikajifungia kwani nilimuogopa baba zaidi ya mama yangu, sikuthubutu kuongea nae kabisa tayari nilihisi mabadiliko yangu ya mwili yatakua ni upuuzi tu kwake hata angeyajua.

Dakika chache baadae usingizi ulinipitia hata shule sikukumbuka tena siku ile, kwa upande wa mama ilikuwa ni zaidi ya dhambi kwani hakutaka kuniona nyumbani, nilitakiwa kuwa shule hata kama nilikuwa na uchovu mkubwa kiasi gani. Cha ajabu baba yangu niliyemjua kuwa ni mkali zaidi ya simba mwenye njaa, hakuthubutu kutoa neno lolote, aliniangalia tuu kisha akaendelea kusoma gazeti lake la mwanahalisi, hapa nilijiuliza maswali mengi sikupata jibu japo bado niliamini tuu kuwa jibu lipo “ntajua tuu kinachoendelea “ niliwaza kabla ya usingizi kunichukua.

siku ile ilipita siku ya pili kisha wiki ya kwanza kwa mara nyingine niliamka asubuhi nikiwa na uchovu zaidi niligundua kitu kingine cha ajabu sana. Mapigo ya moyo yalikuwa yakienda mbio mnoo, “ hivi mbona nahisi harufu ya marashi?” sina kawaida ya kujipulizia marashi mimi!", Nilijiuliza hali nilikuwa najua kuwa harufu ile ni aina ya marashi aina ya kasablacka, marashi haya waliyatumia wazazi wangu. "Mungu wangu, nini hiki?". Nilijiuliza baada ya kushuhudia jambo lingine kubwa zaidi ya hata hayo marashi sikuwa na mtetezi nilikaa kimya ningemueleza nani anielewe Kuhusu maajabu yale?.

Zilipita siku tatu, hapa nilikuta hali imezidi mnoo.safari hii; niliamka na kukuta yale yale mambo mazito lakini la zaidi nilikuta mkufu ambao ulikuwa umekatika, nilimfahamu mvaaji wa mkufu ule. Ilionyesha wazi ulikatika bila yeye kuuona hadi kuusahau kitandani kwangu “nitafanyaje sasa?” niliwaza nikiwa nimekaa kitandani peke yangu.

Kutokana na heshima, pamoja na utu ambao nilijengwa akilini mwangu na wazazi wangu haikuwa kazi rahisi kufungua kinywa changu na kueleza jambo mabalo nilihisi likiendelea itakuwa aibu kufanya hivyo sikujua kuwa nilikuwa naharibu zaidi. Huwezi kuamini niliungana na wazazi wangu kutoa vicheko pale ilipobidi lakini ukweli ni kwamba sikua na furaha kutoka moyoni kama walivyofikiri wao, niliamua kulifumbia macho suala hili la kusikitisha mno niliapa kutokusema kwa yeyote pasipo kujua kuwa dunia haina siri, ipo siku nitafunguka tu aidha kwa kupenda au kwa kutokupenda .

“Jessica” , nilimsikia baba yangu akiniita niliitika kwa unyonge mno huku nikijikaza kuelekea mahali alipokuwa , tumbo lilikuwa likiniuma zaidi ya kawaida, uchovu pamoja na kichefu chefu vilizidi kuniandama pia “ .Unajisikiaje mwanangu?” mama aliniuliza baada ya kunionea huruma kwa jinsi nilivotembea kwa shida “ nahisi kichefuchefu mama , tumbo linaniuma pia” nilimjibu mama ambaye alizidi kunipeleleza kwa maswali ya hapa na pale .

“ Mmh mbona una dalili kama za ujauzito wewe” sentensi hii kutoka kwa mama ilinitisha mno, nilijikuta nikikumbuka matukio yaliyonitisha mno wiki kadhaa zilizopita, niliamua kujiongeza mwenyewe kwenda kwa daktari kabla mambo hayajaharibika zaidi dokta George ndiye aliyenifanyia vipimo katika hospitali ya St. Joseph na hakusita kunipa majibu kama yalivyokuwa, Dokta huyu nilimfahamu alipokuja shuleni kisha kufanya vipimo vya ujauzito wasichana wote,ilikua ni kawaida ya wasichana wa shule ile kufanyiwa vipimo vya ujauzito kila mwezi.

Dr aliniangalia kwa macho makali huku akinidadisi kwa umakini akaita Jessica kisha alishusha miwani yake na kunikazia macho zaidi “ wewe si mwanafunzi? ……

Kwanini umeanza vitendo hivi mapema mwanangu?” ,dokta George akasema kwa lugha ya upole mno nilikosa jibu nilibakia nikiuma vidole tu mithili ya mtoto mdogo “naomba …… naomba …… naomba unisaidie dokta” nilijithidi kuongea kwa upole nilitka dokta George anisaidie kutoa ujauzito ule kabla sijatamka sentensi ya kutoa ujauzito dokta yule alinijibu kwa jazba mno upole wake uliyeyuka kabisa “ siwezi kuua mimi, utajifungua tu ……. Na taarifa hizi zimefika kwa mzee Juma” nilichoka kumsikia dokta George akimtaja baba yangu sikujua amemfahamu vipi, pia hapa nikagundua kuwa dokta George anawafahamu wazazi wangu zaidi ya vile nilivofikiri niliamua kusimama na kutoka nje ghafla nikiwa na mawazo mazito mno “ inamaana baba ndiyo kanifanyia hivi” niliwaza baada yakukumbuka ule mkufu na mvaaji kuwa ni baba yangu mzazi , mkufu ule niliukuta asubuhi kisha kugundua pia niliingiliwa kimwili bila ridhaa yangu , japo niliogopa kujieleza kwa wazazi wangu mawazo yangu yalinizidia huku nikiwa njiani kuelekea nyumbani machozi yalianza kunitoka ghafla.

Nilijua kuwa ujauzito ule ulizidi kukua kisha kuonekana wazi lakini nilipanga kuuficha hadi pale watakapo ona wenyewe.

mwanamke mzoefu acha tu aitwe mzoefu,kumbe mama aligundua tatizo langu kabla ya mimi mwenyewe kujigundua “ Jessica naomba uniambie ukweli huu ujauzito ni wa nani la si hivyo utanijua kuwa mimi ni zaidi ya binadamu” maneno haya ya mama yangu mzazi yalikuwa na maana kubwa japo sikuyatilia maanani ilikuwa ni lazima nimfiche ukweli huo hadi pale kitakapotokea chochote ambacho kilipangwa na mwenyezi mungu, siku zilizidi kusonga.

Sikuzote hakuna kazi ngumu kama kumficha anayejua ukweli kufanya hivyo nisawa kukimbia kwa nguvu kumbe upo pale pale yaani huendi mbele wala nyuma, nasema hayo kwani sikuile nilishangaa mama akichukua simu yake na kumpigia mtu ambaye sikujua ni nani , ghafla nilisikia sauti ya mtu huyo , alikuwa ni wa kiume , “ naomba uongee na binti yako kabla sijafanya maamuzi ya hatari “ mama yangu aliongea kisha kunikabidhi simu ile, sikuwa na budi kuipokea.

Mungu wangu , alikuwa ni dokta George , nilijua kwa haraka kwani sauti yake nilijua vyema.

“ Jessica ongea ukweli usaidiwe , ni nani mhusika wa kiumbe hicho , aliuliza dokta yule , sikuweza kuongea kwani kwikwi ilinizuia kabisa ningemtaja nani ? ni nani hasa ambaye nilikuwa na uhakika naye ?

Sikuwa na jibu, sauti za vilio zilimfanya dokta kukata simu “ nakupa siku hii ya leo tu umtaje mtu hujo” la sivyo ninacho cha kukufanya ! “ Mama yangu alimaliza na kuondoka kwa hasira huku akipiga hatua ndefu kama mtu anayekimbizwa .

Huko nje nilimsikia akiongea na baba yangu juu ya suala langu, “Asiposema nitamfukuza nyumbani kwangu,” hata baba yangu alikuwa upande wa mama , sikujua nini cha kufanya. Lakini pia sikujua dr George alihusika vipi na familia ile hata kuweza mkazo kiasi kile kuhusu ujauzito wangu “Ee muumba wangu, nisaidie niondokane na tatizo hili” Niliomba dua nikiwa chumbani kwangu , suala lile lenye utata liliendesha sana akili yangu.

Maisha yangu yaliendelea kuwa yenye maswali mengi niliwaza ni jinsi gani kiumbe atakayezaliwa atamjua baba yake wakati hata mama yake simjui “. namshukuru sana Mungu kwani alinepusha kosa la kutoa ujauzito ule, huenda nisingeishi tena kwa kufanya hivyo.

Nikiwa na mawazo nikakumbuka jina Harrison huyu ni mwanaume niliyempenda mno alinipenda pia, mapenzi yetu yalianza toka kidato cha kwanza,tulipanga mengi kuhusu maisha yetu ya baadae lakini nilimpoteza siku nilipofukuzwa shule baada ya kugundulika na ujauzito, machozi yalinitoka kwani sikutegemea kuwa nitatengana na Harrison bila kupenda .

Miezi ilikatika nikaamua kuacha kulia isingewezekana kulia milele, kama ni shule huenda ilipangwa niishie kidato cha tatu na kama ni Harrison sikupangiwa kuishi naye. Ugomvi na mama yangu ulipungua kidogo,wote walishirikiana kulea ujauzito ule na siku ya kujifungua ikawadia, hapo ndipo hadithi ya masiha yangu ikaanza upya kabisa.

Nilijifungua mtoto wa kiume nikamuita Jonathan pamoja na kujifungua salama mama yangu hakufurahishwa kabisa ,nilimuona akimuangalia mtoto yule zaidi ya maramoja na kuguna waziwazi kabisa sikujua ni kwanini swala hili liliendelea mara kwa mara .

Kitendo cha mwanangu kufanana na baba yangu kilikuwa na maana kubwa kwa mama yangu jambo hili lilimtesa sana mama,sikujua kua kilichomtesa ni dhambi zake mwenyewe na sio vinginevyo.

Huenda ,ningejua mipango ya mama baada ya mwanangu Jonathan kulionja joto la dunia ningembeba na kutoroka nae milele, Nasema haya huku nikikumbuka usiku ambao mama alinigongea mlango usiku wa manane nilimfungulia bila hiana,aliingia na kufunga mlango taratibu mkono wake wa kushoto ulikuwa na kisu kikali mno hapo nilishindwa kutafsiri tukio lile kwa haraka ,“mbona unaingia na kisu mama! Kuna nini tena?” nikamuuliza kichovu mno bado usingizi ulinitesa “mama Jonathan”, aliniita kisha akatoa kisu taratibu niliiona wazi hasira yake.

" nataka kujua mzazi halisi wa mtoto huyu usiposema namuua huku ukishuhudia “,mama aliongea haya bila kusita sikujua kua ni utani au alimaanisha kweli ” “ Simjui mama nili………’’ kabla sijamaliza mama alimvuta mwanangu Jonathan aliyekuwa kitandani kwenye usingizi mzito nilishtuka mno kutokana na ule ukatili kwa kichanga wangu Jonathan , Umri wake wa siku chache toka azaliwe haukuendana na ukatili aliofanyiwa.

Hapo niliamini kuwa mama alimaanisha alichopanga na alichonitamkia,sikuwa na budi kusimulia kilichotokea hadi kupata ujauzito japo sikuwa na jibu la moja kwa moja kuhusu muhusika mkuu. Mtiririko wa matukio yale yaliyonitisha ulitoshakabisa kumfanya mama yangu kujua ukweli na kufanya maamuzi yanayonitisha hadi leo.

Nakumbuka mama alipoondoka chumbani kwangu usikuule alionekana wazi kuwa alikuwa na jazba . Laiti ningepata nafasi ya kumuona tena ningembembeleza asifanye kile alichokifanya lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa kumuona.

Kutokana na uchovu nikiwa bado na siku chache tangu nilipojifungua nilichelewa mno kuamka,huenda labda nisingeshuhudia mauaji yale ya kikatili kama ningeamka mapema, lakini kumbe ilipangwa nishuhudie.

Damu nyingi zilikuwa zimechuruzika kutoka chumbani kwa baba na mama yangu , nikalazimika kugonga mlango wa chumba chao hukunikiwa nimetawaliwa na uoga wa hali ya juu ukimya uliendelea na kutokufunguliwa mlango ule kulichangia uamuzi wangu kuita majirani hapo ndipo niliposhuhudia kuwa miaka yote niliishi na katili wa dunia ,nikiishi katika tumbo lake kwa miezi tisa kisha katika nyumba yake mwenyewe.

Mlango ulivunjwa na jirani mmoja baada ya kutofunguliwa pale tulipogonga kwa muda mrefu mimi na majirani wale tukashuhudia miili miwili ikiwa na visu katika matumbo yao.

Haikuwa rahisi kubuni chanzo cha mauaji yale, lakini maandishi machache yaliyoandikwa na mama yangu mzazi yalitosha kunipa ushahidi na ulinzi pekee dhidi ya kesi ile ya hatari. Yalisomeka hivi:

“Jessica,nimeamua kisasi hiki nwanangu, nikiwa na akili timamu kabisa, kilichoniponza ni hasira lakini ilikuwa ni bora nifanye hivi kuliko kuishi na hasira niliyokuwa nayo moyoni. Nilijutia kosa langu kumsaliti mwanaume alietoa posa nyumbani kwetu na kunioa hadi nikapata ujauzito wa kukuleta duniani Jessica! Ilipotambulika kuwa nimepata ujauzito wa mwanaume mwingine niliomba radhi akanisamehe kabisa. Lakini sikujua kuwa alibaki na kinyongo moyoni, mwanaume huyu sio baba yako mzazi kama ulivyojua, ni baba yako wa kambo, ameamua kulipiza kisasi kwa kukupa ujauzito tena ukiwa usingizini kwa mbinu alizozijua yeye! Siwezi kuvumilia kumuona duniani ni bora tufe wote.

Sijakuacha yatima mwanangu baba yako yupo hai ni Dr. George”

Mwili wangu ulipata ganzi kwa maneno haya sikutaka kuamini chochote kile kilichotokea kuanzia mauaji yale hata maneno yaliyoandikwa katika karatasi.

Mazishi yalifanyika, sikuweza kupinga ukweli kuwa niliingiliwa kimwili na baba yangu ambaye sikujua kuwa hakua mzazi wangu halisi.

Machungu ya mkasa huu yalianza kupungua siku hadi siku japo siwezi kusahau.

Namshukuru mungu kwani pamoja na ukatili wa mama yangu, alikumbuka kuacha ujumbe ambao ama kwa hakika usingekuepo, huenda ningeishia jela! Jessica alisema kwa uchungu.

Share hadithi hii inayofundisha umuhimu wa kusamehe na kusahau,ili wote tue kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom