Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
USAMBAZAJI WA MAJI YA BOMBA MUSOMA VIJIJINI
Jimbo la Musoma Vijijini lenye vijiji 68 linayo miradi ya usambazaji wa maji ya bomba ndani ya vijiji vyote 68 - tunaishukuru sana Serikali yetu
Mradi wa Kata za Busambara & Kiriba:
Tenki la ujazo wa lita 500,000 limejengwa Kijijini Mwiringo kwa ajili ya usambazaji wa maji ya bomba ndani ya vijiji vyote sita (6) vya Kata hizo mbili.
DC wa Wilaya ya Musoma, Mhe Juma Chikoka anaufutalia mradi huu na mingine ya Jimboni mwetu kwa ukaribu sana. Mkuu huyo wa Wilaya ataenda kuzindua utumiaji wa maji ya bomba ya mradi huo mwezi ujao - msikilize kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.
RUWASA inaendelea kupongezwa kwa kazi nzuri inazozifanya Jimboni mwetu - kila kijiji kupata maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria au/na kuchimbiwa kisima kirefu cha maji - hongereni sana!
CLIP/VIDEO 2 zilizoambatanishwa hapa zinaelezea utekelezaji wa mradi wa maji ya bomba ya Kata za Busambara na Kiriba - tafadhali zifungue!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumamosi, 15 Feb 2025