Gamba la Mbu
Senior Member
- Jun 28, 2020
- 160
- 417
Kuna ombwe kubwa la ufahamu katika jamii yetu hususani kwenye suala la ujenzi. Nani ni nani na anafanya nini kwenye ujenzi? Hii nitaleta mada yake siku za usoni.
Twende kwenye mada!
Kuna baadhi yetu nyumba zetu hugeuka makaburi wakati wa joto ila feni hugeuka mkombozi huku tukiomba Tanesco wasikate umeme.
Yumkini hufahamu katika hatua za awali kabisa za usanifu kuna baadhi ya mambo hayakwenda sawa hivyo kukoleza makali ya joto. Lakini wengine changamoto hii hupungua kwa kiasi kikubwa.
Hatua za ujenzi:
01. Hatua za awali kabla ya kusanifu ramani /Pre-design Stage (PD)
02. Hatua za Usanifu ramani /Schematic Design (SD)
03. Hatua ya uendelezaji usanifu ramani /Design Development (DD)
04. Uandaaji wa Michoro ya Kujengea/ Construction Drawings (CD)
05. Ujenzi /Construction
Kwa leo mada yetu itagusa sana kipengele cha kwanza kwani ndio kiini cha mada yetu.

Katika hatua hii kuna mambo ya msingi mengi ambayo yataamua kutoa taswira katika hatua zingine za usanifu. Vitu hivyo huibuliwa katika hatua ya kwanza ambayo:
A. Muainisho wa vitu vilivyopo katika kiwanja /Site inventory
B. Upembuzi wa vitu vilivyomo kwenye Kiwanja /Site Analysis

Hii ni orodha ya vitu ambavyo kiwanja chako kinakuwa kinavyo au kupakana navyo.
Mfano; vitu vya asili kama vile aina ya udongo, uoto wa asili na hali ya hewa kama vile uelekeo wa upepo kuzama na kuchomoza kwa jua (Hapa utahitaji sana data za watu wa Mamlaka ya hali ya hewa kwa eneo husika ili upate taarifa sahihi)
na vitu visivyo asili i.e man made features lama zipo mfano miundombinu ya barabara, maji, umeme n.k
B. Upembuzi wa vitu vilivyomo kwenye Kiwanja /Site Analysis:
Hii ni hatua muhimu sana kabla ya kuanza usanifu wa ramani ya nyumba/ jengo kwani huchambua kila kilichobainika katika Site Inventory.
Hapa ndio utaamua nyumba yako iweje ili kuendana na mazingira husika ya eneo ulilopo.
Hapa utachakata data za hali ya hewa kisha utabaini eneo husika lina tabia gani katika vipindi mbalimbali vya majira ya mwaka.
Aina mbalinbali za hali ya hewa na jinsi gani usanifu wa nyumba yako unapaswa kuwa:
1. Maeneo ya Joto: Hapa yamegawanyika katika makundi mawili yaani:
Hot and humid climate (Maeneo yenye joto na hali ya hewa ya unyevunyevu - ukanda wa pwani na maziwa makuu) na
Hot and dry climate (Maeneo ya joto yenye ukavu - Maeneo ya kati ya nchi ambayo yapo mbali na bahari na maziwa)
2. Maeneo yenye baridi
1. Nini cha kuzingatia katika maeneo ya joto?
a. Uelekeo wa Nyumba (Orientation of building)
- Sehemu ndefu ya nyumba itazame Kaskazini na kusini
Kipindi cha jua kali upande wa mashariki na magharibi ndio hupigwa jua la moja kwa moja hivyo kufanya hivi hupunguza athari za jua la moja kwa moja kuingia kwenye sehemu kubwa ya nyumba kupitia kwenye madìrisha.
ii. Madirisha makubwa:
Ukubwa wa madirisha usiwe chini ya mita za mraba 15 - 20 za eneo la mita za mraba za sakafu ya chumba husika.
iii. Mzunguko wa hewa wa kuingia na kutoka katika vyumba (Cross Ventilation):
Hili ni suluhisho la tatu ambapo hewa ya asili inayoingia inaruhusiwa kutoka kwa upande mwingine na hivyo kuwezesha kupunguza makali ya joto katika nyumba.
iv. Uoto wa asili:
Katika mazingira ya nje/landscape unashauriwa kupanda miti ya vivuli inayostawi mwaka mzima ili kusaidia kupoza ukali wa jua kuzunguka nyumba yako
.................................................................................
Itaendelea