Kumekuwa na kamtindo cha kupandisha bei ya bidhaa kwa kuwavutia wateja na kuwapotosha bei halisi na kusema ni bei punguzo ili kuwe na nafasi ya kuongeza gharama za ununuaji wa bidhaa hiyohiyo kwa kipindi kijacho. Kwa mfano bei halisi ya bidhaa ni shilingi 100 anasema bei halisi ni sh 200 okoa asilimia 50 nunua kwa sh 100 kumbe ndio bei yake. Baadae ukija unakuta ni sh 200. Sale imekwisha. Labda ninapotosha naomba maoni zaidi juu ya hili swala.
Kwa huko ughaibuni kuna kitu kinaitwa REBATE. Jisomee hapa kwa maelezo zaidi.
Pengine kuna wasanii wachache wa mfano uliyoeleza hapo juu, hata hivyo, discount nyingi ughaibuni si za kilaghai. Kipindi cha summer kwa mfano, unaweza kuona discount ya nguo za winter, nguo ambazo sio rahisi kupata soko baadae katika kipindi kijacho cha winter.