USARE; mbinu ya kutawala nchi na Dunia

USARE; mbinu ya kutawala nchi na Dunia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
USARE; MBINU YA KUTAWALA NCHI NA DUNIA.

Na, Robert Heriel

Kwa maana nguvu ya utawala, mafanikio, mamlaka na ushindi waijuayo ni wachache. Hao ndio wenye kuheshimika, kutukuzwa na hata kuabudiwa. Basi ikiwa kutawala ni siri basi acha ibaki kuwa siri, na ikiwa ushindi ni fumbo siruhusiwi kulifumbua. Lakini leo hii nitakupa sehemu ya funguo katika moja ya milango ya kutawala mtu, jamii, taifa na dunia kwa ujumla.

Niite Taikon wa Fasihi, mwanafalsafa kutoka nyota ya mbali.

Kama nilivyoandika katika kitabu cha “Nadharia za Taikon” nikaweka kanuni, sheria, mbinu na mikakati mbalimbali zitakazomsaidia mtu katika suala zima la utawala iwe kwenye siasa, biashara, dini, miongoni mwa mambo mengine. Basi jumbe hii leo ni sehemu ndogo katika yale yaliyomo katika kitabu hicho.

Kutawala ni jambo gumu sana, kuwa mtawala kunahitaji moyo wenye ujasiri, hisia zenye ustahimilivu, akili za dharura zenye matokeo yenye manufaa, maono ya mambo yajayo, maamuzi thabiti yenye hekima na busara. Ili mtawala asifiwe na akumbukwe zaidi kwa kuleta mabadiliko chanya iwe ndani ya familia, jamii, taifa na dunia basi lazima awe na sifa hizo hapo juu.

Kutawala ni ngumu sana ikiwa mtu hafuati kanuni muhimu na za lazima. Kwa kweli kutawaliwa kuna raha sana kuliko kuliko kutawala. Pengine hilo linaweza kukuchanganya, lakini usichanganyikiwe. Ipo hivyo.

Huwezi tumia nguvu, na akili nyingi kutawaliwa lakini kumtawala mtu, jamii, taifa au dunia sharti utumie nguvu na akili nyingi. Hii pekee yake inaweza ikaeleweka kwa wengi.

Watu wengi hufikiri kutawala ni raha, hutamani kuwa watawala kwenye masuala ya kisiasa, kijamii, kidini na hata kiuchumi. Hii ni kutokana na umbo la nje la utawala ambalo siku zote linapendeza na kuvutia. Katika kitabu cha “Nadharia za Taikon” Nimeeleza pia umbo la utawala ambapo nimeeleza kwa kina aina tatu za umbo la utawala; Umbo la nje(Ganda Wakawaka), umbo la kati(Ganda Sakusi), umbo la ndani( Ganda giza). Ubora na nguvu ya utawala inategemea zaidi umbo lake. Umbo la utawala ndio huamua utawala Fulani udumu kwa muda gani.

Maisha yanahitaji na kutegemea zaidi utawala na mamlaka. Kila mtu hupenda utawala na mamlaka ili kuyaongoza maisha yake. Mtu asipojua namna bora na mbinu za utawala basi ni rahisi kushindwa kutawala maisha yake, na ukishindwa kutawala maisha yako basi lazima utakuwa kwenye kundi la kutawaliwa.

Miaka ya nyuma niliwahi andika makala Fulani kuhusu mbinu za kumtawala mtu , makala ile nilieleza kwa kifupi mbinu chache ambazo unaweza kuzitumia kumtawala mtu, nilisema ili mtu atawaliwe basi sharti mambo mawili yafuatayo yafanyike:
  • Dhibiti Akili yake;
  • Huwezi mtawala mtu aliyekuzidi akili, utawala wako utakuwa mashakani na huenda usidumu kwa muda mrefu. Akili humsaidia mtu kuishi. Hivyo kukamata akili ya mtu ni kuchukua maisha ya mtu huyo, kuyaendesha maisha ya mtu huyo. Akili humsaidia mtu kuwa huru, kuidhibiti akili ya mtu ni kudhibiti uhuru wake. Huenda ukajiuliza kuwa uhuru ni nini? Uhuru ni kujitegemea, kujiendesha, kuwa na maamuzi bila kuingiliwa. Yote hayo hushikiliwa na akili. Endapo akili ya mtu ukiidhibiti basi utakuwa unaendesha maisha ya mtu huyo, utakuwa na maamuzi ya mtu huyo, pia atakuwa tegemezi kwako.

  • Zipo mbinu kadhaa za kudhibiti akili ya mtu; chache miongoni mwa nyingine ni; Kuunda Nadharia Njama, Haribu elimu ya mtu, jamii, au taifa Fulani, Kosesha mahitaji ya msingi ya kuishi, miongoni mwa mbinu zingine.

  • Dhibiti Imani yake.
  • Mwisho wa akili ya mtu ndipo imani huanzia. Jambo ambalo akili ya mtu haiwezi kulifanya au kulitatua ni rahisi sana kuingiza imani. Siku zote watu wenye akili finyu ndio huzipa imani sehemu kubwa ya maisha yao. Katika Mlinganyo wa msawazo baina ya Akili na Imani, ipo hivi: Akili ndogo husababisha mtu kuwa na imani kubwa, halikadhalika akili kubwa husababisha mtu kuwa na imani ndogo.

  • Pia watu wenye akili sana wafanyapo mambo makubwa ambayo watu wenye akili finyu hawawezi kuyafanya basi huitwa wachawi, manabii, wanafalsafa, mitume na majina mengine ya namna hiyo.

  • Ukitaka mtu au jamii Fulani isifikiri kwa kiwango kikubwa basi dhibiti imani yake. Mpe imani kubwa, hamasisha mambo ya kiimani zaidi kuliko mambo ya kiakili(uwezo wa kufikiri, kuchanganua mambo, kubuni n.k). Ukifanikiwa katika hili utakuwa umefanikiwa kumtawala katika maisha kwani kadiri imani yake inavyoongezeka ndivyo akili yake inavyoshuka. Hatimaye kila jambo atalichukulia kiimani zaidi hata kama ni uhalisia.
Sitaki kuacha kuzungumzia mbinu muhimu ya utawala, hasa katika kutawala jamii, nchi na dunia kama sio Ulimwengu mzima. Mbinu hiyo nimeipa jina la USARE kama nilivyoelezea katika kitabu cha “ Nadharia za Taikon”

USARE ni nini?

Usare ni mbinu ya utawala kwa Mujibu wa nadharia za Taikon ambayo mtawala hutaka kuwafanya watu anaowatawala wawe sawa kiakili, kiimani, kiutamaduni, kimtazamo, miongoni mwa mambo mengine.

Mbinu hii ni moja ya mbinu muhimu ambayo mtawala yeyote ni lazima aitumie, isipokuwa Mtawala wa kwanza ambaye ni Mungu. Mungu katika Mbinu ya Usare ameweza kuitumia kwenye mahitaji ya msingi kama vile; watu wote sharti wale chakula, wanywe maji, walale usingizi, waugue, wafe miongoni mwa mambo mengine. Hii ninaiita kanuni ya Usare ya uhitaji na uhitajiwa kama nilivyoeleza katika Nadharia za Taikon.

Kitu pekee ambacho Mungu hajakiweka kwenye Usare ni akili, mtizamo, maumbile, imani, na mihemuko. Na hii nimeeleza sababu ya mambo hayo kuwa hivyo katika Nadharia za Taikon.

Usare tunaitumia maeneo mengi kama sehemu ya kutawala watu, mfano kwa shuleni ni lazima wanafunzi wavae Sare, Wanajeshi, mapolisi, manesi miongoni mwa wanaovaa Sare. Sare ni utambulisho, mtu anapovaa sare hii hueleza jambo moja kuwa yeye ni mtu Fulani ana anawakilisha kundi Fulani. Ikiwa mwanajeshi atavaa sare ya jeshi basi muda huo yupo chini ya utawala wa kijeshi, yaani anatawaliwa na jeshi na kanuni zake. Na hii humfanya ku-behave kama mwanajeshi kwani yupo chini ya utawala wa kijeshi. Endapo atavunja sheria za utawala wa jeshi akiwa ndani ya Sare basi ni wazi atakuwa amelichafua jeshi na kanuni zake. Hivyo hivyo na kwa wanafunzi, mwanafunzi hawezi fanya uhalifu wowote akiwa kava sare ya shule Fulani kwani itakuwa ni rahisi kutambulika. Hivyo itambidi avae nguo nyingine au avae nguo isiyomhusu kuwapoteza maboya watakaomsaka.

Aina za Usare kwa Mujibu wa Nadharia za Taikon;
  • Usare wa mavazi
  • Usare wa kiakili
  • Usare wa kiimani
  • Usare wa Kiitikadi hasa wa kisiasa
  • Usare wa Kibiashara
  • Usare wa Kisanaa
Usare wa kisanaa huu unajitokeza katika mambo ya burudani, michezo na Sanaa kwa ujumla. Kwa mfano; Kwa upande wa wanamuziki usishangae kuona mwanamuziki Fulani akimuiga mwanamuziki mwingine. Usishangae kuona waimbaji wengi wakimuiga muimbaji mmoja. Kwa hapa Tanzania, waimbaji wengi huiga uimbaji na madoido ya Msanii Diamond Platunum. Hii tafsiri yake Diamond kwenye muziki amefanikiwa kutawala wanamuziki wenzake hasa wale wanaomuiga. Mfano wa pili; Wachezaji wengi duniani wamemuiga Marehemu Michael Jackson katika kucheza kwake. Tafsiri yake ni kuwa Michael Jackson amewatawala kisanaa wasanii wengine kimichezo.

Hii pia ipo kwenye uigaji wa sauti kwa baadhi ya watangazaji wa televisheni, usishangae kuona watangazaji karibu wote wa vipindi wa redio au televisheni wanafanana sauti na misemo. Hii ni sehemu ya kutawaliwa na aliyeanzisha mtindo huo. Hii pia ipo kwenye masuala ya miziki ambapo muziki wa jamii Fulani huweza kutawala miziki ya jamii nyingine mathalani kwa wakati huu muziki wa singeli ambayo kwa sehemu kubwa unatokea sehemu za pwani unaanza kuteka miziki ya asili ya jamii zingine na kuudondosha muziki wa singeli.

Usare wa Kibiashara;

Hii hutokea pale bidhaa moja huzitawala bidhaa zingine. Mfano simu ya Samsang au Iphone huweza kuzitawala simu zingine kama vile Huawei, Nokia na Tecno. Hii hutegemea zaidi Propaganda ambapo makampuni husika hutumia media mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuzipaisha bidhaa hizo na kuzizima bishaa shindani kwa kuzipa sifa mbaya. Hii hutaka watu wote watumie simu moja kwani ndio simu bora na yenye heshima. Hivyo watu kwa kutaka heshima hujikuta wakinunua simu hiyo na kuziacha simu zingine na hapo kampuni ya simu hiyo huibuka mtawala katika bidhaa za simu bora duniani.

Usare unakuja hapa; sio lazima watu wote watumie simu ya aina moja, ila wafanyabiashara huunda njama na hila ikiwemo propaganda kwamba watu watumie simu zao kwani ndio simu bora lengo ni kukusanya wateja na wapenzi wa bidhaa zao. Na wakifanikiwa hili basi hugeuka watawala.

Kwa leo tuishie hapa, tutaendelea wakati ujao.

Pata kitabu cha Nadharia za Taikon kujua zaidi.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

0693322300 / 0711345431
 
bila hata reference?
sijui wewe ni msomi wa kiwango hadi unaandika vitu kama vile ni njozi
 
bila hata reference?
sijui wewe ni msomi wa kiwango hadi unaandika vitu kama vile ni njozi

Hata reference ni sehemu ya mbinu ya Usare katika kutawala suala zima la elimu na masuala ya ktaaluma.

Maoni yako yamesaidia wadau humu jamvini kuzidi kuelewa kile nilichokielezea katika post yangu.

Chuoni watu hawafundishwi kufikiri wao kama wao bali huelekezwa namna ya kufikiri kile wengine walichofikiri, na ndipo hapo huambiwa watafute reference vinginevyo wataonekana sio wasomi.

Usishangae kwa sasa wasomi wengi hawana uwezo wa kuamini mawazo yao, nadharia zao, misimamo yao, na falsafa zao, wao huamini zaidi katika mambo ya watu wengine, na hii ndio tunaita wapo chini ya utawala wa watu hao.

Karibu sana Mkuu, Msomi unayehitaji reference, wakati wanao watakuja tumia maneno yangu kama reference kwa sababu Baba yao(wewe) ulitumia za wengine.
 
Back
Top Bottom