Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,231
Juhudi zinazofanya za kushusha vifurushi na kuondoa baadhi ya huduma kwenye bima ya NHIF hayo ni matunda tu yaliyooza ila mzizi wake ni wimbi kubwa la wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Idadi kubwa ya watumiaji wa bima ya NHIF ni wagonjwa wa kisukari,shinikizo la damu na saratani magonjwa ambayo visababishi vyake ni mfumo wa maisha (vyakula vya kisasa na kazi zisizotumia nguvu).
Wengi wa wagonjwa wa haya magonjwa ndio waliojaa kwenye mahospitali yetu kila mwisho wa mwezi wakienda kuchukua dawa zao za kudumu (ku-refill) na kutibu madhara ya ziada (complications) ambazo kwa kiasi kikubwa zinagharimu mfuko pesa nyingi sana.
Uwepo wa usasa kwenye vyakula mfano ukaji wa biriyani,kuku wa kukaanga na burger na ongezeko vinywaji lukuki vya sukari na vilevi kama hautadhibitiwa kwa kuwapa watumiaji elimu basi tujiandae kuwapokea hawa watu kama mizigo ya mfuko wa bima huko mbeleni.
Mfuko na wizara ya afya wanapaswa kuwekeza nguvu kubwa sana kwenye kampeni ya kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza (non-communicable diseases) ili kunusuru pesa za walipa kodi na pesa za NHIF.

Upvote
3