G Jonathan Kamenge
Member
- Apr 8, 2023
- 30
- 23
Niliandika mwanzoni mwa mwaka huu kusema "Changamoto za kijamii kwenye jamii yetu zinahitaji wanamageuzi kuliko mageuzi yenyewe", ambapo nilitafakari nanyi pamoja na mambo mengine, mchango wa kitaaluma wa "wanasayansi jamii" wetu. Hii ilikuwa baada ya kauli kwamba "ubakaji unaongezeka mitaani kwa vile kuna mijanaume bachela inaranda huko mitaani", tena kauli hii ikitolewa mimbarini, mbele ya wanaume na viongozi wa kijamii, na ikitolewa na mwanamke kiongozi wa jamii. Nimeyakumbuka haya baada ya kauli hiyo kujirudia katika maoni ya mwanamke mwingine, tena kwenye jukwaa linalojinasibu na kujadili "mpango wa taifa 2050" ikidai kupimwa wanaume kabla ya kuoa ili kuhakikisha ndoa zinadumu; haya ndiyo mawazo ya jamii yetu na bado tunadhani tuko salama!!!! Hiki ni kichaa kibaya naapa na humu Simo!!
Mafanikio ya Mkutano wa Beijing pamoja na mambo mengine, yalikuwa ni kutengeneza "Wanaume wenye miili ya kike" asomaye na afahamu, na kisha hilo likazaa wanawake wenye miili ya kiume na hapo katikati tumezalisha machotara ambamo tumepata wafiraji na wafirwaji tena wakidai kutambuliwa haki zao na hivyo yametimia maneno ya mwanafalsafa wa kale kusema "Demokrasia itaiharibu dunia kwa vile Maskani atadai ukwasi wa tajiri, na demokrasia itampatia, Mtumwa atadai ubwana na demokrasia itampatia, Raia atadai mamlaka ya Mtawala na Demokrasia itampatia, mwanamke atadai mamlaka ya mwanaume na demokrasia itampatia, Mtoto atadai mamlaka ya Mzazi na Demokrasia itampatia, na mwisho tutakuwa na sintofahamu (chaos) ulimwenguni. Ni aibu kwamba maneno haya yametimia upesi kuliko yalivyosemwa. Demokrasia imetufundisha "haki" bila wajibu na Waafrika tulivyo mbumbumbu, hatujajifunza kwamba msingi wa maisha ya jamii ni falsafa za jamii hiyo zaidi kuliko kiwango cha pesa na mali, maana mwisho wa siku tofauti ya tajiri na maskini inakomea mezani, kitandani na kaburini asomaye na afahamu!!! Kwanza tulianza na dini; wageni walituletea namna yao ya kuabudu na sisi kama mazuzu tukapokea bila kuhoji wala tafakuri tukisahau "uungwana" wa Waberoya haukutokana na kufuata mkumbo, bali umakini wao katika uelekevu wao katika "kuyachunguza" maandiko" (Matendo 17:10-11) ili waone kama waliyofundishwa ndivyo yalivyo. Leo dini zimekuwa juu ya Mungu kiasi Waafrika tumeshuhudia zama ambapo watu kwenye mataifa kadha wameuana, wengine hawazikani, hatuoleani hata hatusemeshani kisa dini zetu na waliotuletea dini zetu ndiyo waliotuuza utumwani, ndiyo walioua babu zetu, ndiyo waliotutazamisha"ufalme wa mbinguni" wakati wakiiba dhahabu, Almasi, Shaba na madini yetu mengine na kujenga "ufalme wa Uingereza " ambapo leo Uingereza una dhahabu nyingi kwenye hazina zake kuliko mataifa yote ya kiafrika kwa pamoja. Waafrika sasa tuko kwenye majumba ya ibada tunajidhalilisha kwa vituko, tunalamba chumvi mbichi kama Ng'ombe, tunalipa fedha kuuziwa maji na vitambaa, tukitengeneza matajiri wakubwa ilhali sisi tukivakia hoehae!!! Twendeni tu!!
Kwenye ndoa, wanawake walikutanika Beijing wakakubaliana uwe "mwisho wa kukandamizwa" na mfumo dume, kwa hekima kubwa sana wakaamua kwamba sasa watafute "haki sawa", huenda kwa vile pia walishindwa kutambua kwamba haki inakuja na wajibu na wajibu unalingana na uwezo wa kimaumbile kuwajibikia hicho kikupasacho. Tukaanza kudemkwa tena kwenye ngoma za "haki sawa" na matokeo yake tukafanikiwa kuzalisha "wanaume wenye miili ya kike" kwa vile sasa "what a man can do, a woman can do even better". Ujinga ni kwamba tangu kale, wanawake walikuwa "wakifanya kazi" kwenye jamii zao, walikuwa na majukumu yao na yaliheshimiwa, ila walichotaka wao ni "kutambuliwa" kana kwamba hawakuwa na utambulisho hapo awali. Maneno ya mwanafalsafa na mwanasayansi wa kale kusema "Demokrasia itaiharibu dunia kwa vile raia atadai mamlaka ya Mtawala na Demokrasia itampatia, Mtoto atadai mamlaka ya Mzazi na Demokrasia itampatia, Mwanamke atadai mamlaka ya Mwanaume na Demokrasia itampatia......na mwishowe tutakuwa na sintofahamu (chaos) ulimwenguni" yametimia upesi kuliko tulivyodhani. Leo kila mtu anayo mamlaka yake binafsi na anadai "haki zake" kwa nguvu, kila mtu anataka "kutambuliwa". Wafirwaji wanataka "kutambuliwa" haki zao, Wasagaji wanataka "kutambuliwa" haki zao, hata watoto wadogo wanataka "kutambuliwa" haki zao bila yeyote kati ya hawa kutaka kutambua wajibu wake wala haki za wengine, ni ulimwengu wa Demokrasia na haki za binadamu hata pale ambapo binadamu anaishi na kutenda kinyume cha binadamu maana jambo likikosa tafsiri moja inayokubalika kuwa sahihi, holela huwa halali.
Leo, wanawake wako "busy" kufundisha wanaume jinsi ya kuwa "wanaume" ilhali wao hawajawahi kuwa wanaume, na hakuna siku watakuwa wanaume, lakini ndiyo wanaamua "sifa na wajibu wa mwanaume", wanaume nao wameamua wengine kuwa "majike dume" na wanadai haki zao "kutambuliwa" wakijiita non binary" na majina mengine lukuki mradi tu kila mtu analo la kusema na kutenda katika ulimwengu wetu huu wa haki bila wajibu. Swali ambalo wengi tunashindwa kulijibu ni: Wakati tulipoamua kwamba tunataka kuondoa"mfumo dume" na kuweka "haki sawa" tulifanya utafiti kwanza kujua kwamba sharti tutapitia kwanza "mfumo jike" na ndipo tufike huo "Usawa wa kijinsia"!!?. Hatutaki kama ambavyo hatukutaka kujiuliza "ujinga" huo, tunataka 'kutambuliwa' kwa usawa wa kijinsia' kati ya mwanaume na mwanamke kwenye maeneo yote ya maisha.
Tuliwaza kwamba huo tunaoita "usawa wa kijinsia" maana yake nini na athari zake zote yaani hasi na chanya zitakuwaje!!? Au tuliamini tu kwamba wenye athari hasi ni mfumo dume lakini usawa wa kijinsia ni bwerere (Utopia) na hivyo hauna athari hasi!! Tunajua gharama za kuishi katika ulimwengu wenye "usawa wa kijinsia" wakati hatuna "usawa wa maumbile" na hivyo "usawa wa mahitaji" ya kihisia na hata usawa wa "uwezo wa mwili" na huenda vipawa na utashi hasa wakati kunapokuwa na uhitaji wa stimuli za kukabilianana na "hatari" za maisha!!? Haya, twende tu, hadi tufike mahala ambapo ama tutalazimisha wanawake kukojoa wamesimama au wanaume kuchuchumaa ili wakojoe almuradi tufikie "usawa wa kijinsia". Najua mtasema natukana au my mind is on the gutter, lakini nani kawaambia Nanga miye ninajali unanga wenu kama nyie hamuwezi kujali wa kwangu!!!? Haya, sasa hata vyombo vyetu vya habari vinadhani ni habari kwamba wanawake wanadhani wanaume ndiyo tatizo la kuvunjika ndoa na hivyo kabla ya kuingia kwenye ndoa wapimwe kwanza, lakini hakuna anayejiuliza babu na bibi zenu waliwezaje kuishi na kudumu kwenye ndoa zao pamoja na "ujima" waliokuwa nao, ila nyinyi ambao mmekuwa emancipated hata kukaa kwenye mahusiano ya kawaida tu miezi sita bila ugomvi na vituko hamuwezi!!? Kuna mahali tumeshindwa kufikiri sawa sawa na sasa tunaadhibiwa na upumbavu wa kushindwa kupanga kwa vile hilo linamaanisha tulipanga kushindwa kwenye nyanja hii ya kijamii.