Muza madafu
Member
- May 2, 2024
- 8
- 8
Usawa wa Kijinsia ni hali ya uapatikanaji sawa wa rasilimali na fursa bila kujali jinsia.
Suala la usawa wa kijinsia limewekewa nguvu kubwa hapa nchini, ikiwa ni pamoja kuwekwa sera, utoaji wa elimu ya masuala ya kijinsia na kukomesha vitendo vya ukatili. Inasikitisha sana kwamva baadhi ya watu wamepotosha maana halisi ya usawa wa kijinsia huku wengine wakitoa kauli,misemo na kutoa tafsiri zinazo hamasisha migogoro, chuki na visasi kati ya mwanaume na mwanamke.
Picha kutoka tovuti ya iStock
Ili kuipata Tanzania imara tunayoutaka ni muhimu kukomesha upotoshaji kuhusu suala la usawa wa kijinsia. Upotoshaji unaweza kuathiri lengo mahususi la dhana hii na kupelekea kuharibu kizazi kijacho na kutengeneza taifa lenye matukio mengi zaudi ya ukatili wa kijinsia na hivyo kuharibu dira ya taifa ya miaka ijayo katika nyanja mbalimbali kama ifuatavyo.
sheria na haki. Ili kufikia Tanzania tunayoitaka miaka ijayo ni lazima sheria mpya na sera zinazotungwa katika mifumo ya utoaji wa haki izingatia uhalisia wa usawa wa kijinsia na sio kuelemea upande mmoja. Wakati sheria zikitungwa kumlinda mwanamke dhidi ya ukatili pia zimlinde mwanaume pia dhidi ya ukatili bila kuegemea upande mmjoja wa jinsia. Kupitia wizara yenye dhamana pamoja na wadau wa sheria wahakikishe wanalilinda taifa lijalo katika nyanja zote bila kuegemea upande mmoja wa jinsia.
Picha kutoka tovuti ya Shuttle stock
Siasa na uongozi;
Usawa wa kijinsia katika nyanja za siasa na uongozi ni jambo la msingi sana, Si vyema kuruhusu taifa letu kutengeneza kizazi cha ubaguzi wa kijinsia katika siasa. Hatutakiwi kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa kwa kuwapunguza wanaume, bali tunaweza kuwajengea uwezo wa kuwa washindani katika nyanja za siasa na hivyo kupata ushiriki wa wanawake katika siasa bila kugandamiza wanaume. Hii itasaidia kuimarisha dhana halisi ya usawa na kupata suluhu bila kuongeza matatizo mengine.
Picha kutoka tovuti ya AdobeStock.
Ustawi wa jamii
Kutokana na taarifa za takwimu mbalimbali zilizotolewa hivi karibuni , imeoneka wazi kwamba katika suala la ustawi wa jamii hali sio shwari kabisa. Idadi ya juu ya ndoa kuvunjika ni hatari zaidi kwa Tanzania tunayoitaka miaka ijayo, huku miongoni mwa sababu ikiwa ni usindani wa mamlaka kati ya mwanaume na mwanamke (wanandoa)., Familia nyingi zinaongozwa na mzazi mmoja suala ambalo linaharibu msingi wa malezi ya vizazi vijavyo.
Picha kutoka tovuti ya iStock .Ni muhimu serikali kwa kishirikiana na wadau wengine kama mashirika binafsi na taasisi za dini iangalie kwa ukaribu suala hili na kutoa elimu, semina mbalimbali ili kutoa elimu sahihi juu ya nafasi ya kila mmoja bila kujali jinsia zao. Ikumbukwe kizazi bora kijacho kinategemea malezi bora yanayotolewa , uimara wa familia na ubora wa jamii ya sasa.
Elimu
Ni wazi kwamba serikali kupitia wizara ya elimu imejitahidi sana kujenga mazingira sahihi na mazuri kw amtoto wa jinsia ya kike katika nyanja za elimu kupitia juhudi mbalimbali kama vile ujenzi wa shile bora za wasichana na mabweni nchi nzima. Hili ni jambo jema na la kupongezwa lakini ikumbukwe kuwa kizazi kijacho sio kwa ajili ya jinsia ya kike pekee, bali mtoto wa kiume nae anapaswa kuandaliwa katika mazingira sahihi bila kubaguliwa ili kupata Tanzania bora tunayoitaka na yenye usawa wa jinsia.
Kupitia wizara inayoshughulikia masuala ya jinsia na watoto kuhakikisha juhudi zinawekwa kwa watoto wote walio katika hatari ya kutokupata elimu bila kuegemea upande mmoja wa jinsia kwa kuwa usawa wa jinsia unahusisha watoto wote ambao ni taifa la kesho.
Ajira na kazi
Ni wazi kabisa dhana ya usawa wa kijinsia inaeleza kwamba watu wote ni sawa na wana haki sawa ya kushiriki na kupata nafasi katika nyanja mbalimbali za ajira na kazi. Lakini kwa nafasi ya pekee sera katika zinazotungwa mwanamke amepewa kipaumbele katika kupata nafasi hizo ili kutengeneza usawa wa kijinsia. Hivyo baadhi ya waajiri hutoa nafasi kwa upendeleo wa jinsia hiyo hali ambayo inatengeza uhasama baina yao jinsia inayonyimwa nafasi.
Ni vyema serikali na wadau wote kuhakikisha hali hii inadhibitiwa na uwezo wa utendaji bila kujali jinsia ndio umpatie nafasi mhusika. Mbinu mbadala zitumike kuwainua wanawake kama vile kuwajengea uwezo wa usindani pamoja na umahiri wa utendaji ili kupata ushiriki wao katika nyanja za ajira na kazi kwa usawa.
Mila na desturi
Utamaduni mila na desturi njema ni nguzo ya taifa. Ili kuifikia Tanzania bora zaidi na yenye mafanikio yenye urari katika nyanja zote, ni lazima kuondoa mila na desturi potofu zinazosababiaha ukatili wa aina yeyote wa kijinsia ili kupata jamii ya watu wenye furaha na kujiamini. Lakini pia ni muhimu kuhakikisha tunatunza mila na desturi njema ambazo zinaongeza ustaarabu na haiba njema kwenye jamii zetu baina ya mwanamke nawanaume na sio kupotosha maana halisi ya mila na desturi kwa mgongo wa usawa wa kijinsia.
Mwisho: huwezi kutatua tatizo kwa kutumia njia zinazotengeneza tatizo jipya.
Picha kutoka kwenye tovuti mbalimbali.. iStock AdobeStock na shuttle stock.

Upvote
6