Usemi wa “Kutokujua Sheria hakuwezi kumuondolea hatia Mtuhumiwa” umetia watu wengi hatiani kimakosa

Usemi wa “Kutokujua Sheria hakuwezi kumuondolea hatia Mtuhumiwa” umetia watu wengi hatiani kimakosa

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Asilimia kubwa ya watu wengi wanaishi vijijini, Vijiji ambavyo kwa asilimia kubwa bado havijaendelea kiasi cha kuzijua Sheria vizuri sana.

Sheria zipo lakini watu wengi hawazijui na hata adhabu zake pia hawazijui. Watu wengi wanaishi kwa mazoea na wako busy kutafuta kipato na sio kusoma na kuzielewa sheria.

Kwa utafiti mdogo unaweza kugundua hili hasa kwa wafanyakazi wengi waliosaini mikataba mibovu iliyoandikwa kwa kingereza hata kiswahili pia.

Maeneo ya vijijini ndiko kwenye ugomvi mkubwa wa Ardhi na makosa hayo hutendeka kwa sababu watu hawazijui sheria.

Kwa kuangalia tu kawaida wanasheria wengi wako maeneo ya mijini wakisubiri kesi ziletwe na si kwenda kutoa elimu vijijini ili kuzuia migogoro.

Vijijini watu wamekuwa wakirubuniwa kuuza Ardhi bila hati za kueleweka na kisha ardhi zao kupokwa na watu wanaozijua Sheria.

Hata kwenye siku za Sheria ni wananchi wachache hufika kusikiliza nini kimefanyika na kinachoendelea kufanyika kwenye masuala ya Sheria.

Uelewa wa wananchi ni mdogo sana kuhusu Sheria.

Sambamba na hayo badala ya kuziachia ofisi za kata kushughulikia maswala ya kisheria huko vijijini ni muhimu sasa kupeleka elimu ya kutosha kwa wananchi wazijue Sheria.

Elimu ya Sheria bado haijafika kisawasawa ndani ya Jamii.
 
Ukweli ni kwamba watanzania wengi hatupendi kusoma....kwenye mkataba hapo Sheria ipo wazi kama mkataba upo kwa Kiingereza unasaini wa nini? Mwananchi yupo kijiji kwa nini asifike halmashauri Yake pale atakutana na mwanasheria na kupewa ushauri wa kisheria bure.
Tupende Kutafuta maarifa ambayo hatuna
 
Taarifa nzuri, ni wakati sasa serikali ingekuwa inaajiri watu wa sheria wanaofanya kazi ngazi ya kijiji, kitongoji na mtaa. Wakati wa vikao vya wananchi kuwe angalau na wasaa wa kuwafundisha wananchi sheria mbalimbali.

Hili litasaidia kuwapa wananchi japo elimu kuhusiana na sheria za nchi.
 
Kabisa dear
 
Ukweli ni kwamba watanzania wengi hatupendi kusoma....kwenye mkataba hapo Sheria ipo wazi kama mkataba upo kwa Kiingereza unasaini wa nini? Mwananchi yupo kijiji kwa nini asifike halmashauri Yake pale atakutana na mwanasheria na kupewa ushauri wa kisheria bure.
Tupende Kutafuta maarifa ambayo hatuna
Hilo pia sidhani kama wanalijua
 
Back
Top Bottom