Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ilikua ni familia ya watoto watatu, wa kwanza wa kike, wa pili wa kiume na watatu wa kike. Yule mtoto wa kwanza alimaliza darasa la 12 na kupelekwa kwa mama mdogo kujifunza ujuzi. Mume wa mama mdogo ni mbunge na ana biashara nyingi ikiwemo mini supermarket, mgahawa na nyumba ya kulala wageni.
Alitokea mmoja wa wageni wa mume wa mama mdogo alimuelewa yule bint kutoka bush na alimuoa, jamaa alikua mhasibu huko Wilayani. Baada ya harusi binti alikua na kwake. Sasa yeye ndiye nyota ya Jaha nyumbani kwao. Kaka yake amemaliza shule na anawasaidia wazazi shambani.
Mwaka wa pili binti hajakamata ujauzito, wakati huo mdogo wa mwisho amemaliza form four nae amekwenda kukaa kwa dada. Si unajua mjini asubuhi kuna chai na maziwa ya Nido ukibahatika unapata na mkate wenye blueband.
Kale katoto kalipenda tamthilia, usiku dada yake alikwenda kulala na kukaacha sebuleni kakiangalia movie za Kinigeria na English yake ya form four A. Shemeji akirudi anakakuta tena kamevaa upande wa kitenge kifuani. Shemeji alianza mazoea. Haijapita miezi miwili kabinti kana mimba ya shemeji.
Shemeji kuona ameyaharibu alikwenda kwa wakwe na matofali kama 2,000 anataka kuwajengea nyumba ya kisasa pembeni ya pale wanapokaa na ikiisha awafungulie wholesaler store pale ilipo nyumba ya sasa hivi.
Yule shemeji anae lima na wazee shambani alipigwa milioni tano akatafute biashara ya kufanya. Baada ya kuyaweka hayo sawa amerudi mjini anamwambia mama kijacho arudi kwa wazazi kabla dada hajastuka na kutapika tapika kwake.
Kabinti kamerlid kijijini baba anauliza mimba ni yana ni kusema ni ya shemeji baba alikataa. Baada ya kuulizwa sana aliwaambia jibu lile lile ilibidi waamini. Shemeji alikua na shida ya mtoto vibaya sana na baba mkwe amepewa nyumba na duka ananwambia mkwe haya tutayamaliza kifamilia usiwe na shida.