Boss hoja yako ni nzuri lakini kuna makandokando mengi sana yanatusonga....
Kwanza soka la ulaya unaliona kiurahisi na kulisikiliza kiurahisi kwa sababu linatangazwa sana, unawasikia sana akina Suarez kwa siku kuliko hawa akina Ngasa. Hasheem Thabeet anacheza kikapu marekani na ni mtanzania lakini vyombo vya habari vya bongo vinakaa hadi miezi 6 bila kuwa na habari yake hata moja. Kila siku vichwa vya habari ni Arsenal na manchester kwa kuwa ndio zinauza magazeti yao na tv + radio zinasikilizwa sana.
Leo hii mimi shabiki wa Yanga nikitaka kuvaa jezi ya timu yangu hakuna duka hata moja ambalo nikenda nikasema niuzieni official jezi ya yanga nitapata, licha ya potential kubwa ya clubs kutajirika kwa kujitangaza na kuuza bidhaa zao. Viongozi wa clubs za mpira ni kama wanasiasa. Kiongozi wa TFF hajui hata utamaduni wa timu ya yanga anang'ang'ania wavae nyekundu ambayo kimsingi kila shabiki wa simba atachukizwa na wana yanga kuvaa nyekundu, na utamaduni huu tumeuona toka utotoni. Wakati wa kombe la kagame hadi watangazaji wa super sport walishangaa kuona kuwa Tanzania kun fan base kubwa kiasi cha kujaza uwanja wa watu 60elfu, lakini hakuna anaetumia hii potential kuingizia fedha klabu, watu ni wezi tu, hawataki hata watu wakae uwanjani kwa nambari za viti ili kusiwe na takwimu za watu wangapi wameingia uwanjani wao waendelee kuchakachua. TFF wanapokea mamiliono toka kwa wadhamini lakini hawajawahi hata siku moja kutoa tangazo luningani la biashara kuitangaza mechi yoyote ya ligi kuu, wanachoangalia wao ni fursa zilizowazi na hawana ubunifu kutafuta fursa zingine kutangaza ligi na kuongeza mvuto na mashabiki, wanafanya kazi kwa mazoea na uchakachuaji. Mi nilishangaa sana watu wawili wa tasnia moja walipopata nafasi za kazi ktk TFF huku ikijulikana kabisa kuwa hawana jipya, hawana mbinu zozote za kibiashara zinazoendana na wakati huu kidunia, just wameenda pale kujiponya njaa na they are inspired na namna Mwakalebela alivyotajirika haraka
Mambo hayo na mengine mengi kama watu kuingiza siasa kwenye mpira ndio yanasababisha watu kuhamia ughaibuni ambako kwanza soka inavutia mno, kuna mbinu za ufundi zilizo wazi, tofauti na huku wanashindana kwenda kwa waganga wa kienyeji tu. Hakuna ladha ukienda uwanjani, wachezaji wavivu, hawawezi hata kicomplete five passes. Niende uwanjani kufanya nini kama Tegete anaingia kwenye basi kugombana ngumi na shabiki na inachukuliwa poa tu? Nitapendaje soka letu wakati wanaoliendesha hawalipendi?