Ushabiki wa Yanga na Simba una Uswahili Mwingi sana, Mashabiki wajinga

Ushabiki wa Yanga na Simba una Uswahili Mwingi sana, Mashabiki wajinga

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Ukifuatilia wapinzani wa Jadi wa Nchi zingine utaona kwamba Upinzani wa Yanga na Simba una Uswahili ndani yake na wala sio ushabiki proffesional.

Mfano Chukulia Vilabu pinzania vya Al Ahly and Zamalek kule Misiri. Huwezi kuta Mashabiki wa Zamalek eti wanaenda Uwanjani kushangilia tipu pinzani itakayo cheza na Al Ahly. Wale wanaingia Uwanjani kushangilia timu yao na si vinginevyo.

Hata kule Argentina Jiji Buenos Aires ambako kuna rivals Boca Juniors and River Plate bado huwezi kuta uswahili, kuna makala moja nilikuwa naifuatilia wanadai upinzani wa Boca Juniors na River Plate kuna wakati ulikuwa ni Top 1 Duniani miongoni mwa Derby kwa sababu upinzani wao huwa unaambatana na Vurugu kubwa sana kuna wakati ilipigwa marufuku kabisa mashabiki kuangia uwanjani lakini bado wakawa wanapigana hata huku mitaani ba kuchomana visu ni upinzania wa hatari sana ambako siku wanacheza lazima Police kutoka pande mbali mbali za Argentina wamwagwe uwanjani make inapigwa mkono wa hatari.

Ila Pamoja na Upinzani wao wa hatari kabisa kitu ambacho huwezi kukion kwao ni eti Mashabiki wa River plate waende uwanjani siku wanacheza Boca Junior na timu nyingine eti wakashangilie hio timu nyingine, hilo halipo kwao na wako na timu zao ru wanashangilia timu zao.

Sasa Bongo unakuta ni fullu Uswahili anacheza Simba my b na Timu Pinzani hata kutoka nje utaona mashabiki wa Yanga wana enda eti kuipa sapoti hio timu pinzani, au wanacheza Yanga na timu pinzani unawakuta mashabiki wa Simba.

Ni kawaida kukuta inacheza Simba na Mtibwa ila nje ya uwanja zinauzwa jezi za Yanga na Simba tu. Au zinacheza Mtibwa na Bishara United ila nje ya uwanja zinauwa jezi za Simba na Yanga, hizi ndo aina ya shabiki za kipuuzia sana.

Hawa Mashabiki pia wa hizi timu walivyo waswahili eti uwanja hujaaa pale tu hizo timu mbili zinapo kutana, tofauti na hapo hutawaona uwanjani bali wataendeleza ushabiki uswahili wao mitaani.

Kama Simba na Yanga wasingekuwa na mashabiki waswahili basi leo hii hizi timu mbili zinge kuwa mbali sana kimapato, Mapato tu ya Milangoni na kuuza Jezi yangetosha kabisa.Lakini hawa Mashabiki uchwara na waswahili unakuta hawataki kununua hata Jezi OG ya Cluba wanakimbilia zile copy za kichina kisa zinauzwa bei rahisi halafu hawa hawa mashabiki wanataka mafanikio.

Kuna mashabiki kindakindaki wa hizi tumu hawajawahi ungisha club jezi OG misumu na misimu ila wakute sasa kwenye vijiwe vya kahawa.

Hawa mashabiki Waswahili uwanjani huwaoni siku labda Simba anacheza uwanja wa Taifa na Ihefu hutakaa uwaone uwanjani wako mitaani kwenye vijiwe vya kahawa huko, au siku Yanga inacheza na timu ya mkoani hutwaona uwanja.

Fikiria Yanga na Simba wangekuwa wanapewa sapoti na mashabiki wao kwenye mechi zote na viwanja vinajaaa unazani wangekuwa na ukwasi kaisi gani?

Wale mashabiki jana kwenye napokezi ya kombe la Yanga asilimia 70 hawanunuia Jezi OG na wala uwanjani huwaingii wao ni kwenye vijiwe tu vya kahawa.

Hizi timu zisingekuwa zina watagemea wafadhili kama zingekuwa na mashabiki serious badala ya hawa Waswahili.
 
Unatushaurije mkuu sisi mashabiki uchwara?
 
huu ndo ukweli timu zina mashabiki ambao kutoa sapoti hawataki wanataka mafanikioa wanatamani hata uwanjani wawe wanaingia bure na jezi wawe wanagawiwa bure kila msimu, hizi timu mashabiki mfano wenye sapoti ya kufa na kupona kwa club ya yanga na simba kwa Dar hawazidi 5000 kwa kila club hawa ndo wale wanao nunua jezi orijino na pia wanaenda uwanjani hata kama zinacheza na vitimu vidogo vya mikoani na wanalipa kiingilioa kila mechi. Wanao bakia ni wanasubilia zikutane hizo timu mbili na pia jezi wanazo nunua ni zile photocopy
 
Hizi timu zingekuwa tajiri sana kwa Africa shida ni aina ya mashabiki zilio nao hilo ndo shida unakuta pale Dar tu kuna watu unakuta wanajiita mashabiki Damu wa hizo timu ila uwanjani hawajahi kanyaga na jezi hawajahi nunua sasa wakute vijiweni na mitaani huko wanavyo shuka.
 
huu ndo ukweli timu zina mashabiki ambao kutoa sapoti hawataki wanataka mafanikioa wanatamani hata uwanjani wawe wanaingia bure na jezi wawe wanagawiwa bure kila msimu, hizi timu mashabiki mfano wenye sapoti ya kufa na kupona kwa club ya yanga na simba kwa Dar hawazidi 5000 kwa kila club hawa ndo wale wanao nunua jezi orijino na pia wanaenda uwanjani hata kama zinacheza na vitimu vidogo vya mikoani na wanalipa kiingilioa kila mechi. Wanao bakia ni wanasubilia zikutane hizo timu mbili na pia jezi wanazo nunua ni zile photocopy
Tatizo mashabiki wa MAKOLO ....bado Wana elimu duni
 
mfano mzuri kwenye shindano la nani zaidi la kutoa bukubuku limewashinda wengine mpaka wamejitoa wameambiwa bukubuku hazifanyi kitu sasa kama hata buku tu mtu inamshinda ataweza kweli kununua jezi og kwa 50k?
ila ukweli hi hulka ya sisi wabongo kila eneo ni uswahili tupu kuanzia aina ya michezo yote,siasa,muziki n,k
 
kubwa kuliko usishangae mashabiki wa simba wakapungua gafla na wote ukawakuta yanga [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Sidhani kama unafuatilia mpira, timu zote ulizotaja zinapokea na kushabikia wapinzani wa wapinzani wao.

Kama hujui unachoandika uliza kwanza.
 
Uswahili ni tusi? Kwani nyie ni mizungu?

Mizungu au miarabu mnayoiabudu inaweza kusema uzungu/uarabu wao in a negative manner?
 
Hauna akili ww Mzee........uwe unaandika mambo ya maana na sio huu upumbavu wako
 
Back
Top Bottom