Ushahidi mkubwa hadi sasa wa kusulubiwa wapatikana huko Uingereza kutoka nyakati za Warumi

Ushahidi mkubwa hadi sasa wa kusulubiwa wapatikana huko Uingereza kutoka nyakati za Warumi

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Moja ya ushahidi wa mwanzo wa kusulubishwa kwa Warumi umepatikana katika mji uliyo katikati mwa Uingereza.

Mfupa wa mwanamume uliyokuwa na msumari kupitia kisigino chake ulipatikana katika mji wa Fenstanton, karibu kilomita 115 kaskazini mwa London.

Mtaalamu wa mifupa wa Chuo Kikuu cha Cambridge Corinne Duhig amesema ugunduzi huo ni "kitu cha kipekee" kwenye eneo ambalo lilitambuliwa hivi majuzi kama makazi ya Warumi wa kale.

Mtaalamu huyo alisema kwamba hata huko Uingereza "wenyeji wake hawakuweza kuepuka moja ya adhabu ya kikatili zaidi iliyotolewa na Warumi."

Kwa wengi wa wanaakiolojia ambao wamefanya kazi mahali hapa, ni "ushahidi mkubwa zaidi hadi wa leo" wa kusulubiwa, adhabu ambayo imevutia hisia za mamilioni ya kuwa njia ambayo Yesu Kristo alikufa, pia katika mikono ya Warumi.

Makazi hayo yaligunduliwa na kituo cha uchunguzi wa Akiolojia cha Albion, ambacho kilianza kuchimba eneo hilo kama sehemu ya kazi za maendeleo ya miji.

Huko walipata makaburi madogo matano ambapo watu wazima 40 na watoto watano walikuwa wamezikwa, wengi wao wakiwa jamaa.

Inakadiriwa kuwa makaburi hayo yalitumiwa kati ya karne ya 3 na 4 baada ya Kristo.

Huko pia waligundua mabaki ya mtu ambaye alikuwa na kipande cha msumari kwenye kisigino chake.

Mbali na chuma hicho, majeraha kadhaa ambayo huenda mwanamume huyo aliyapata kabla ya kifo chake pia yalirekodiwa kwenye mfupapa huo. Miguu yake ilikuwa na athari za maambukizo au uvimbe ambao ungeweza kusababishwa na shida ya kimfumo au kufungwa kwa pingu.

Ugunduzi wa kipekee
Kwa mwanaakilojia Kasia Gdaniec, kutoka baraza la manispaa ya Cambridgeshire - eneo ambalo ugunduzi huo ulifanyika-, "makaburi haya na makazi haya ambayo yaliundwa na barabara ya Kirumi iliyovuka Fenstanton yametoa dalili mpya katika utafiti wa kiakiolojia."

"Taratibu za maziko ni nyingi na tofauti katika kipindi cha Warumi. Na mara kwa mara tuliona ushahidi wa ukeketaji wa kabla au baada ya kifo, lakini kamwe kusulubiwa."

Kwa Duhig, ambaye ni mtaalamu wa mifupa katika Chuo cha Wolfson, "mchanganyiko wa bahati nzuri wa uhifadhi mzuri na msumari walioacha kwenye mfupa umeturuhusu kuchunguza mfano huu wa kipekee wa nini kusulubiwa kulikuwa."

"Hii inaonyesha kwamba watu ambao waliishi hata katika vijiji vilivyo mbali na katikati ya Milki ya Kirumi hawakuweza kuepuka adhabu moja ya kikatili iliyokuwepo wakati huo," aliongeza.

Ugunduzi huu unafanana na zingine chache ambazo zimetoa ushahidi wa kusulubiwa ulimwenguni: moja huko Larda, huko Italia, nyingine huko Mendes huko Misri na nyingine huko Giv'at ha Mivar, kaskazini mwa Yerusalemu, ambayo ilipatikana mnamo 1968.

Ugunduzi huu wa hivi punde zaidi ndio unaofanana zaidi na ule wa Uingereza: pia unaonyesha kipande cha msumari uliozikwa kwenye mfupa na ulifukuliwa katika nafasi sawa na ule uliopatikana huko Fenstanton.

Kwa mujibu wa uchambuzi uliyofanywa na Baraza yenyewe, ilikuwa ni kawaida kwamba baada ya kusulubiwa misumari iliondolewa ili kuitumia tena, lakini katika kesi hii, msumari ulipigwa na kudumu kwenye mfupa.

Wakati wa uchimbaji, vitu kama vile sarafu, vioo vya mapambo na mifupa ya wanyama pia vilipatikana

Baraza hilo pia lilibaini kuwa ugunduzi wa jengo kubwa ungeonyesha kuwa ni makazi ya Warumi yaliyopangwa na ishara za biashara inayofanya kazi sana.

Na walibainisha zaidi kuwa walitarajia kuonyesha matokeo kwa umma katika siku zijazo.
 
Kwahiyo unataka kusema kuwa ile dhana ya kwamba story ya kusurubiwa kwa Yesu ilipikwa na Warumi ili kudumisha mila zao ni ya kweli!
 
Kwahiyo unataka kusema kuwa ile dhana ya kwamba story ya kusurubiwa kwa Yesu ilipikwa na Warumi ili kudumisha mila zao ni ya kweli!
Kulingana na tafiti hiyo ni kweli ila si yule yesu wa kwenye filamu.
 
Back
Top Bottom