Tairi bovu
JF-Expert Member
- Sep 28, 2017
- 3,063
- 2,985
Habari wanabodi,
Haya yanayotokea hayatokei kwa bahati mbaya. Ni mipango ya makusudi ikiongozwa na kuratibiwa na vyombo vya ulinzi.
Mwaka Jana nilikuwa kwenye jimbo moja la uchaguzi. Pale kulikuwa na madiwani wawili toka upinzani.Kati yao mmoja anatoka CUF na mwingine CDM.Ulikuwa msimu wa kuunga mkono juhudi.
Nikiwa pale walikuja viongozi wa CCM wa mkoa. Wakati wapo pale wale madiwani waliunga mkono juhudi na kuhamia CCM.
Ukatangazwa uchaguzi wa marudio.Siku
wakati wa kurudisha fomu, DED wa pale siku ile alimwamuru mhasibu wa mapato asiwepo kabisa ofisini na azime simu yake Sababu wagombea wa upinzani wakirudisha fomu wasiweze kulipa wataambiwa mhasibu hayupo. Kweli hakuwepo maana nami nilimtafuta ili nilipe malipo fulani.
Pia Siku ile Ded alifunga kabisa ofisi yake na kumtafuta OCD na kwenda kupiga mitungi. Walianza asubuhi hadi usiku.
Mtendaji wa kata huwa ndiyo wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata, wa pale siku ile aliingia mara mojamoja kwa machale ofisini alipopokea tu za CCM akaita Polisi na kufunga na kuondoka zake.
Hatimaye wale madiwani waliunga mkono juhudi na kupita bila kupingwa.Hivi ndivyo ilivyofanyika nchi nzima.Haya ya kushindwa kujaza fomu ni uongo tu.
Inawezekanaje kutoka Tabora hadi Mtwara na Mbeya kwa mfano makosa yawe sawa na kwa wapinzani tu? Je, walijifungia chumba kimoja na kujaza?
CCM ikumbuke haya kaburu alijenga miundombinu lakini alichukiwa,Iddi Amini alinunua ndege 67 lakini alichukiwa; Ghaddafi na Sadam hivyo hivyo.