Ushahidi wa kuwatia hatiani Mbowe na wenzake 11 watiliwa shaka na Mahakama Kuu

Ss Jr

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2018
Posts
577
Reaction score
451
Uamuzi wa Mahakama Kuu kwamba warufani hawakuwa sehemu ya maandamano waliyokuwa wakidaiwa kuyaongoza ni mwendelezo wa uchambuzi wa hukumu ya Mahakama Kuu kuelekea hitimisho la shtaka la pili lililokuwa likiwakabili.

Hili ni shtaka la kufanya mkusanyiko usio halali, wakidaiwa kuufanya Februari 16, mwaka 2018 katika maeneo matatu tofauti. Eneo la kwanza ni viwanja vya Buibui walikokuwa wakifunga kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.

Eneo la pili walikokuwa wakidaiwa kufanya mkusanyiko huo ni katika Barabara ya Mwananyamala na la tatu katika Barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni, wakati wakiandamana na wafuasi wengine wa chama hicho kwenda ofisi ya Mkurugemzi wa Manispaa ya Kinondoni kudai barua za mawakala wa uchaguzi.

Hata hivyo, Jaji Mugeta baada ya kufanya uchambuzi wa ushahidi aliamua kuwa mkusanyiko katika viwanja vya Buibui ulikuwa halali na Barabara ya Mwanyamala akaamua kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha vinginevyo.

Katika uamuzi kama washtakiwa walikuwepo katika mkusanyiko eneo la Mkwajuni, Jaji Mugeta amerejea ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi kisha sheria na uamuzi wa kesi mbalimbali kuhusiana na kanuni na taratibu halali na sahihi la utambuzi wa washtakiwa.

Kwa upande wa mashtaka, Jaji Mugeta amerejea ushahidi wa baadhi ya mashahidi ambao kulingana na mwenendo wa kesi ya msingi, waliwatambua washtakiwa kizimbani. Kisha alirejea muhtasari utetezi wa washtakiwa ambao kila mmoja alisema kuhusishwa kuwepo katika tukio hilo.

Viongozi hao wa Chadema waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo ni pamoja Mwenyekiti Taifa, Freeman Mbowe ambaye pia alikuwa mbunge wa Hai na Dk Vincent Mashinji (katibu mkuu wakati huo ambaye sasa ni kada wa CCM na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti) na aliyekuwa mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Wengine walikuwa ni manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara, sasa Katibu Mkuu) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) pia mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko. Pia walikuwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Bawacha na mbunge wa Kawe, Halima Mdee; aliyekuwa mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na aliyekuwa mbunge wa Bunda, Ester Bulaya. Katika utetezi wao wote walikana kuwepo mahali pale pa tukio (barabara Kawawa- Mkwajuni). Wengine walidai kuwa waliondoka kabla ya mkutano kumalizika na wengine wakidai kuwa baada ya kufunga mkutano waliondoka kwenda ofisini na wengine wakidai walikwenda nyumbani kwao.

Kabla ya kuamua kuuzingatia au kutokuuzingatia utetezi huo wa warufani, Jaji Mugeta ameamua kuangalia kwanza ushahidi wa upande wa mashtaka kama kuna ushahidi wa kuthibitisha kosa hilo na hasa akianza na utambuzi wa washtakiwa/warufani kuwepo eneo la tukio.

Katika hilo Jaji Mugeta ameanza kwa kusema kuwa hana mashaka na mashahidi hao kuwatambua washtakiwa. Lakini anabainisha kuwa washtakiwa/warufani kwa kuwa ni wanasiasa basi ni watu maarufu.

Hivyo amesema kuwa inaweza kuwa rahisi kwa shahidi muongo na mla rushwa kudai kuwafahamu washtakiwa katika suala la utambuzi. Anasema changamoto hiyo ndio inayoibua umuhimu mkubwa wa kuamua kuaminika kwa mashahidi hao.

Jaji Mugeta anasema udadisi wake wa kutaka kujiridhisha na kuaminika kwa mashahidi hao unaungwa mkono na kanuni ya kisheria iliyokwishawekwa, kwamba linapokuja suala la utambuzi wa mtuhumiwa haitoshi tu kuangalia vigezo vya utambuzi sahihi na kwamba, muhimu ni kuaminika kwa mashahidi.

Katika kusisitiza msimamo huo Jaji Mugeta anajielekeza katika kesi ya Jaribu Abdallah dhidi ya Jamhuri, iliyopo katika kitabu cha taarifa za kisheria mwaka 2003 ukurasa wa 271.

Hata hivyo, Jaji Mugeta anasema kuwa kwa bahati sheria kesi (sheria inayotokana na uamuzi wa mahakama katika kesi fulani) imeweka kinga dhidi ya ushahidi usio wa ukweli katika suala la ushahidi wa utambuzi.

Anabainisha kuwa pale shahidi hana uzoefu (wa kumfahamu) mtuhumiwa kinga ni gwaride halali la utambuzi (pale ambapo watuhumiwa wengi huwekwa katika msitari au misitari na shahidi anatakiwa kumtambua mtuhumiwa wa tukio fulani la uhalifu). Lakini, pale ambapo shahidi anadai kuwa na uzoefu wa mtuhumiwa, basi kinga ni mapema kiasi gani alimtaja mtu huyo aliyetambuliwa. Katika hoja hiyo Jaji Mugeta amerejea kesi ya Marwa Wangiti Mwita didi ya Jamhuri ripoti ya sheria mwaka 2002, ukurasa wa 39, ambapo imeamuriwa kuwa:

“Uwezo wa shahidi kumtaja mutuhumiwa mwanzoni kabisa ni uthibitisho muhimu wa kuaminika kwake, vilevile kama kuchelewa kusiko na maelezo au kushindwa kufanya hivyo huifanya mahakama kutumia busara zake kufanya uchunguzi,” inasomeka sehemu ya uamuzi huo kwa tafsiri isiyo rasmi.

Baada ya kurejea kanuni hiyo Jaji Mugeta amesema kwamba kama alivyokwishaonesha awali, upande wa mashtaka hakuwezesha kutolewa kwa ushahidi kuonesha kuwa ni lini mashahidi wake waliwataja warufani kama walivyokuwa wamewaona katika maandamano eneo la Mkwajuni.

Amesema kuwa tukio linalodaiwa (maandamano) lilitokea Februari 16, 2018 na warufani walishtakiwa kwa makundi, ambapo kundi la kwanza lilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 27, 2018.

“Ushahidi kuhusu ni mapema kiasi gani mashahidi waliwataja warufani kama wahalifu, ungetoa uthibitisho kuaminika kwa mashahidi kuhusu utambuzi wao. Kwa hiyo ushahidi wao kuhusu utambuzi si wa kuaminika,” amesema Jaji Mugeta.

Akizungumzia ushahidi wa shahidi wa pili na wa nane wa upande wa mashtaka, Jaji Mugeta amesema kuwa ushahidi wao ni wa kutilia mashaka kwa sababu ya kujikanganya kwao iwapo walikutana eneo la tukio la uhalifu mara tu baada ya tukio (la maandamano).

Katika ushahidi wake shahidi wa pili alieleza: “Maafisa wa Polisi walili mabomu ya machozi…Tuliamua kukimbia kutoka pale. Kwenye muda wa saa 1:00 tuliamua kurudi eneo la kazi… Siku iliyofuata maafisa wa polisi walikuja eneo letu la kazi kupeleleza kuhusu kilichotokea. Niliwaleza maafisa wa Polisi kuhusu kile kilichotokea.”

Shahidi wa Nane, yeye alieleza kuwa: “Niliwatambua maafisa wa Polisi ambao wanaweza kuwa mashahidi, na vilevile mashahidi huru ambao walikuwepo pale wakati wa ghasia. Miongoni mwa watu waliotambuliwa kama mashahidi ni (shahidi wa pili), Shabani Hassani Abdallah.”

Lakini, Jaji Mugeta amesema kuwa kimantiki shahidi wa pili asingeweza kutambuliwa mapema mara tu baada ya tukio kwa sababu alikimbia.

Amesema kuwa sehemu hiyo ya ushahidi wa shahidi wa pili na wa nane kuhusu ni lini shahidi wa pili alikutana na maafisa wa polisi na kutambuliwa kama shahidi muhimu sio tu kwamba unajikanganya, bali pia hauwezi kupatanishwa.

Amesema kuwa wakati shahidi wa pili akisema ilikuwa siku iliyofuata (kukutana na polisi) shahidi wa Nane alisema ilikuwa siku hiyo hiyo mara tu baada ya tukio na kwamba tarehe na muda sahihi walipokutana (na Polisi) ni jambo linalohusiana kwa kadri kuaminika kwao katika utambuzi wa warufani kunahusika.

“Kueleza kwao stori tofauti kuhusu jambo hili muhimu pamoja na kukosekana kwa ushahidi kuwa ni lini waliwataja watu waliowatambua kunajenga shaka kuhusu utambuzi wa watuhumiwa na pia hupunguza kuaminika kwao,”amesema Jaji Mugeta na kuhitimisha:

“Kwa hiyo ninamua kuwa haijathibitishwa kuwa warufani walikuwa sehemu ya watu waliokusanyika katika barabara ya Kawawa.”

Source: Mwananchi
 
“Kwa hiyo ninamua kuwa haijathibitishwa kuwa warufani walikuwa sehemu ya watu waliokusanyika katika barabara ya Kawawa[emoji736][emoji817][emoji2996][emoji2996][emoji2996][emoji2996]
 
Na ninategemea baada ya hukumu ya hii kesi,nini hasa kilichopelekea mtanzania mwenzetu Akwilina kupigwa risasi na kupoteza maisha yake na polisi(ambao wamekula kiapo cha kulinda raia na msli zao)kitajulikana ili hii family ipate closure ili maisha yao yaendelee maana kwa sasa yamesimama.
 
Back
Top Bottom