leipzig
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 2,766
- 1,708
Nimeifanya hii kazi kwa muda mrefu ya kurekodi matukio ya rushwa katika polisi wa kawaida na wale wa barabarani. Katika ushahidi wangu nimefanikiwa kuwa na video zenye sauti na picha zikionyesha polisi barabarani wakichukua rushwa mchana kweupee. Wakati mwingine huwa najiuliza hawa polisi wameruhusiwa na serikali kufanya uchafu huu kwa raia?
Uzoefu nilioupata unaonyesha kila mara serikali inapoongeza adhabu kwa makosa ya barabarani ndio furaha na neema kwa polisi. Polisi hawa wala rushwa wakati fulani hutafuta makosa kwa tochi ili mradi wanufaike wao binafsi.
Kuna wanaoamini kuwa ni bora ulipe faini badala ya kutoa rushwa lakini nataka niwaambie polisi akikusimamisha anajitahidi kukujengea mazingira ya kukuchelewesha ili mradi upate nia aliyokusudia. Unakuta wewe dereva ndio unawahi ofisini lakini yeye hata hana habari ndio kwanza atakuhoji ili awe huru kuchukua rushwa kutoka kwako.
Naomba kumuuliza kamanda Mohamed Mpinga yuko tayari kunilinda nimpatie ushahidi huu yeye mwenyewe ofisini kwake? Nasema hivyo kwa sababu miaka ya nyuma kidogo Jerry Muro alipata msukosuko mkubwa baada ya kufichua uovu wa polisi barabarani. Pia afande Mpinga anaweza kuniahidi ni lini nitaona mabadiliko ktk polisi baada ya kumpatia ushahidi?
Kwa kumalizia,nashauri serikali itengeneze mfumo rasmi wa ukaguzi wa magari na madereva ili kuondoa uchafu huu ndani ya jeshi la polisi.
NAWASILISHA.