Elections 2010 Ushahidi wa wizi wa Kura hadharani

akashube

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2009
Posts
401
Reaction score
23
Katika mkutano wa kampeni wa CUF unaoendelea sasa hivi hapa jangwani Dar es Salaam Juma Haji Duni Mgombea mwenza wa Kiti cha urais kwa tiketi ya CUF ametoa hadharani ushahidi wa barua pamoja na vitendea kazi vya kutekelezea wizi wa kura unaofanywa na Tume ya uchaguzi kwa kushirikiana na Usalama Wa CCM(uwt).

My take:

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. CCM wataaibika mno mwaka huu. Za mwizi kweli arobaini.

Jamani kwa wale wabishi mnaonaje? maana kuna mpaka barua ya tume ya uchaguzi kwenda kwa watendaji wa kata kuwataka waibe kura na kwamba atakayetoa siri atafukuzwa kazi/na kuuawa.

KAZI KWENU.
 
Asante kwa taarifa hiyo. Hata hivyo tunaomba ufafanue kwa zaidi huo ushaidi ni nini au ni kitu gani kinafanyika?
 

Kwa taarifa hizi, Kikwete hatafanya mdahalo kesho.

Naomba na ziwe za kweli.

Mungu Ibariki Tanzania kwa kutuondolea utawala wa mafisadi.
 
Ananifurahisha Lipumba... anaichambua CCM na ahadi zake
waliahidi kuwapatia maji safi na salama watu wa Tabora ambayo yanapatikana kama kilometa 20 kutoka mjini, wameshindwa na sasa wanaahidi kuwaletea maji kutoka ziwa victoria! wameahidi treni ya umeme wakati hiyo ya dizeli imewashinda
 
Taarifa na nyaraka feki sawa na za Slaa alizopelekewa toka Tunduma za makaratasi ya kura kwenye konteina la ft 40.
Viongozi wa upinzani wanaingizwa kiulaini kwenye mitego ya kijinga halafu baadaye wanaumbuka baada ya kutangaza vitu vya uongo majukwaani.
Tufungue macho na kujifunza kutokana na makosa ya Slaa, hakuna mpango utakaotengenezwa na kuvuja kirahisi hivyo. Ni vitu vya kutengeneza kwa lengo la kuumbua viongozi
 
CCM NI WEZI WAKURA
SIKU ZAKUANGUKA KWAKE ZIMEWADIA, ndio maana kila wanalogusa , linawateleza.
 

mhhh!!!!!!!!
 

Mpango upo, mbona kelele za kukubali matokeo zinazidi mpaka zinakera? Mbona zamani hili tangazo halikuwepo/ Tutavaa chupi moja safari hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…