ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
MAUTI.
Tuishi na kukumbuka
Kama si leo ni kesho
Ni siku ya kuanguka
Nyakati zako za mwisho
Ni lini itakufika
Na vipi mataarisho
Dunia ni ya kupita
Tuyakumbuke mauti..
Tuishi kwa kuingoja
Kutenda njema amali
Mbele yetu inakuja
Usiseme iko mbali
Yani ni sekunde moja
Roho inaacha mwili
Siku hiyo utajuta
Yakikufika mauti..
Kifo njia ya lazima
Kila mtu atapita
Dhalili mwenye heshima
Mauti yatamkuta
Basi tutendeni mema
Vya dunia vinapita
Ili usije kujuta
Yakikufika mauti..
[emoji2398]ibn kimweri.
Tuishi na kukumbuka
Kama si leo ni kesho
Ni siku ya kuanguka
Nyakati zako za mwisho
Ni lini itakufika
Na vipi mataarisho
Dunia ni ya kupita
Tuyakumbuke mauti..
Tuishi kwa kuingoja
Kutenda njema amali
Mbele yetu inakuja
Usiseme iko mbali
Yani ni sekunde moja
Roho inaacha mwili
Siku hiyo utajuta
Yakikufika mauti..
Kifo njia ya lazima
Kila mtu atapita
Dhalili mwenye heshima
Mauti yatamkuta
Basi tutendeni mema
Vya dunia vinapita
Ili usije kujuta
Yakikufika mauti..
[emoji2398]ibn kimweri.