tujuemoja
Member
- Jul 26, 2022
- 7
- 2
1. Upendo ni kuthamini, Kisicho Thamini,
Na sioni Kunufaika, Kwa kuondoa upendo,
Bora niondoe kosa, Kuliko upendo,
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika.
02. Kuondoa kosa, si maringo wala sifa,
Na nikiacha kosa, undugu nao utakufa
Kumbuka undugu, ni bora kuliko mwanasesele,
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika.
03. Zamani Undugu, ulikuwa nikusalimiana kikwetu,
Hata mbali, Ndege kupanda, lakini tukikutana
Kikwetu ulituunganisha, na kutufanya tushikamane,
Upendo ni kuthamini, Kisicho thaminika.
04.Tuwapo mikutanoni, nyumba za ibada,
Wimbo wetu tunaimba, ni wapi ulipo upendo,
Leo Natamani, utambue kwamba,
Upendo ni kuthamini kisicho thaminika.
05. Je, utaweza kuthamini, bila kuwajali wajane,
Vipi ambao umewaumiza, kwa kuzui wao kupaka haki yao,
Lakini kuna ambao umewarudhulumu, mali zao
Upendo ni kuthamini, kisicho,Thaminika
06. Yatima saidia bila , kudai picha kupiga
Ombaomba wahurumie, bila kuwafanya kuwa mitaji
Tulipofika ni Machafuko mno, upendo kuwa mtawala
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
07. Ukipata jukwaa, madhabauni kupandishwa,
Sera yako, kujinadi kwayo iwe upendo
Chuki mwangushe, madhabauni mkeme
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
08. Lakini Acha unafiki, kutangaza upendo
Ili hali mgongoni, umeficha mapanga
Hapo hatujengi, tunabomoa
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika
09. Ukatili si Akili, Wenye Akili wajua,
Ukabaji ni uhuni, vijana tambueni
Wizi si diri, Na Biblia inadai ni dhambi
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika
10. Ni kweli si tajiri, lakini kidogo alitafuta,
Kwa nini macho kukodolea, thamani ya mtu mwingine,
Kura yako chagua upendo, ni thamani ya wanjonge,
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika.
11. Mauaji ya ndugu, ni baraha kuzua,
Kukabana kwa mali, atakazo tafuta mjukuu,
Ni ujinga na upumbavu, shika mpini usisahau jembe,
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika.
15. Kumiliki mali, hakukupi sifa ya kuwa gaidi,
Bado una moyo, maumivu yasikie
Kumgandamiza masikini, sio ujanja
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
16. Hivi,wale watililishao, mifereji ya damu
Roho wa ukatili, bado anazidi kuwabatiza
Kataa huo, ubatizo, una mfukuza upendo moyoni
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
17. Sijawaacha Ndugu, Waoneaji na wazushaji
Ingefaa mwanze leo, kuchukua somo la habari
Matukio sahihi kutuzushia, tutakuona umetambua fursa
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
18. Acha kujaza msuli, kupambana na moyo wako
Jirani yako ni wewe, na wewe ni yeye
Ya nini kutaka kutoa roho yako, kwa jirani,
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
29. Labda sijafahamu, hivi ufisadi ni upendo
Utakatishaji fedha au uhujumu uchumi,
Sikia kwa jirani, kuna watu wanaumizwa,
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
30. Harufu inayovuma, ni kama si ngeni kwangu
Mganga kudai viungo, Ni miaka mingi imepita
Naomba ninong'onezwe, hivi bado inaendelea
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
31. Kuzaa mtoto kizazi hiki, Haina maana atakupenda
Ubaba sikuizi si hofu, kumtisha mwanao
Kisu atakuwekea tena, Mbele ya mama shahidi
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
31. Ujumbe wangu ni mrefu, kutokana na ninachokitetea
Lakini haiwezi shinda, ushairi wa mapenzi
Ambao ni maandalizi, ya mapinduzi ya upendo
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
32. Ninakupenda kwa dhati, ni wajibu wakusema
Muwapo mbele ya umati, na mbele ya kasisi
jioni tunasikia, Nakupenda kwa dhati ameleta maafa.
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika
33. Naweka wazi hili, Shikamo
Sio kigezo cha, kutambua upendo
Wapo wale wa hali gani, mioyoni chuki
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
34. Leo hii Naogopa, hata kupewa pole
Maana ni maandalizi, ya kilio cha kesho
Kutema matabishi, Na kumeza washazoea
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
35. Lakini ukimya usianze, kushindwa kusema
Ubaya ni adui, na upendo ni thamani
Na kamwe, hawezi kupindua meza
Upendo ni kuthamini kisicho thaminika
36. Kipindi cha Mitume, upendo uliwekwa nje
Ndio utambulishe, wa joho zao
Lakini saizi ni Kinyume, Na kinyume uumiza
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika
37. Kuna wakati waweza, usukani ang'atuke
Kumbe shida ni mioyo, mwili una tii tu
Ubaya jiuzuru, upendo tumsimike
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
38. Labda niwe shehe, kasisi kukemea ubaya
Kwa presha ya wafuasi wa ubaya, na hofu kupingwa
Biblia nifundishe, Misahafu ni wasome
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika
39. Akili ndio tatizo, Haitambui upendo
Shule imewapa, lakini ya ukatili
Na ashakuwa mwalimu, kwa wasioenda shule
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
40. Misasa tuinoe, Seremala mbona mnajitenga
Sugua akili za mbao, upendo mwakani apite
Asiye kuelewa, ndio wakuanza ili aelewe
Huo sio ukatili, bali ni usafishaji ubongo
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
41. Nakumbuka darasa, Nguvu kufundisha,
Ni kichwa changu, maana hata kikielewa,
Sheria lazima itungwe, jianzali usivunje,
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika.
42. Sio mswada, lakini ni sheria
Ambazo, utetea haki za watoto,
Wazee, walemavu na wanawake,
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika.
43. Tamati inapiga hodi, Madini ya mwisho zingatia
Upendo hauji, kwa sauti ya mmoja
Ubaya ni mwingi, Andaa mawe ya kutosha
Upendo ni kuthamini kisicho thaminika
44. Nitashanga, kuona bado unafiki
Katika kumpiga, Adui ubaya
Nia tunayo na mwakani, Anakaa chini
Upendo ni kuthamini, Kisicho Thaminika
45. Mikono mfukoni, Ni dalili ya utengano
Jembe kushika, mpini ni umoja shambani
Nyuma unafanya nini, Adui yuko huko harikisha
Upendo ni kuthamini, kisicho thaminika
46. Ukimshindwa adui, usione aibu ungana naye
Si na hapa, umoja tutajenga
Kidedea mwakani tutapiga, Upendo ni mtawala
Upendo ni kuthamini kisicho thaminika
Mwandishi wako:-
© tujuemoja
(David Malunda)
MWANAFUNZI KATIKA CHUO CHA RUCU

Upvote
1