George J Minja
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 289
- 203
Wakuu ni muda sasa tokea niache kutunga na kusoma mashairi ila naamini hiki ni kipaji ndani yangu naomba wote wenye uwezo wa kutunga na kuimba mashairi tujitokeze hapa kuweka mashairi yetu ili jamii ya JF pia ijifunze kwa njia hii leo naanza hivi
Tunakoelekea
Tulikotoka twajua,tuendako giza nene
Tujiulize kwa sala,yajayo twayaonaje
Tulianza kwa pamoja,bila kuwa na upande
Wapi tunaelekea,Yarabi utujalie
Ee mola utujalie,tuijue yako nia
Maisha tuyapatie,tusije poteza nia
Waliyoweka wazee,kutupa maisha mema
Wapi tunaelekea ,yarabi utujalie..............................;;
Nimejaribu tuu kuona kama kale kauwezo kapo au la,ila nikirudi nitakuja malizia hili shairi,karibuni washairi tuendelee sio lazima ya Kimapokea kama lanu(yenye Vina na Mizani) la hasha hata la kisasa weka tuendelee kuburudika
Ahsanteni