Ushamba wa lifti

Kamaka

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2010
Posts
563
Reaction score
33
Mzee mmoja alikwenda na mtoto wake kwenye ghorofa moja la shirika la bima..

Walipofika

mtoto : Akaanza kumuuliza baba hii nini (huku akimuonesha lifti ya ghorofa)

mzee : Mwanangu sijawahi kuona kitu kama hiki maishani mwangu!!!!!!

baadaye kidogo,
akaja kikongwe mmoja kwenye baiskeli akabonyeza vitufe vya mlangoni.

Baadaaye mlango ukafunguka,akaingia ndani,mlango ukajifunga.
Namba zikaanza kujiandika 1,2,3,4.... N.k

baada ya muda mzee na mtoto wakiendelea kuangalia namba zikipanda zikaanza kushuka kuanzia 7,6,5,4,3,2,1.
Mlango ukafunguka mara akatoka binti mmoja mrembo....

mzee akastajabu sana akamuambia mtoto wake kimbia nyumbani kamlete mama yako!!!!!!!!!!!!
 
Sounds familiar!i dont know a TV commercial perhaps.Try and b a bit creative.
 
Hhahaahahah.....mzee nae anataka mkewe awe kabinti!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…