Ushamba wa msukuma uko wapi?

Pablo 119

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
1,515
Reaction score
1,962
USHAMBA WA MSUKUMA UKO WAPI?
Ninavyomfahamu
1.Hapendi makuu,ukimchokoza anasema KAYA YA NG'WOBA NAYO KAYA ili siku ipite salama.

2.Hapendi kesi,ukimdhurumu anasema MAGUZU MASESE ili asipoteze muda kufuatilia mambo ya kesi,badala yake afanye kazi.

3.Hapendi kuumiza moyo kwa hasara iliyotokea, akipata hasara anajipa moyo kwa kusema JATULWA MBITI JITATANANHAGA ili aepuke matatizo ya madonda ya tumbo, moyo presha n.k.

4.Hapendi kujikweza, ukimsimanga ugenini anasema NG'OMBE NG'ENI IKAPAMAGWA NA DIDA,wengine husema don't disarenge the funiture while you are still a guest na huo ndo ustaarabu.

5.Ni mvumilivu hata kwenye suala la utafutaji, akianza na mtaji mdogo hujipa moyo kwa kusema BUSHI BO MBULI BUKAKWILILAGA MU BUTUNGO,wengine husema haba na haba hujaza kibaba.

6.Hatoi siri ovyo ovyo, ukimdadisi anakwambia KAMANWA MAMBI KALI MU NG'OMA ili kuepusha uchonganishi.

7.Kipindi cha njaa huwafariji wana familia kwa kuwaambia SHILIWA SHIDOHE BALI BAKWILE ili kuwaondoa hofu akijua baada ya dhiki kuna faraja.

8.Hana roho mbaya,penye watu wengi na nafasi ndogo husema BITOGILWE BATISHITAGA, ili kujenga upendo na kutobaguana.

9.Hana hasira za kukurupuka, ukimchukiza anasema AKULIPA WELELO huku akitafakari cha kufanya.

10.Anajua mambo yote hapa duniani ni ubatili na yote yatapita,akikabiliwa na jambo gumu asiloliweza anasema NDUHU TAABU.

Wasukuma oyeeeeeeee hebu dondosha neno la kisukuma hapo akipatikana mwenzio anzeni kubonga
 
anajua sana kulima huku akiimba na kupepeta jembe
IGEMBENSABO
 
Wabeja sana ngwanaOmayo...bhasukuma bhasabhi bhaMang'ombe...gobhise ndoho tabu.
 
Hahahah shemeji yangu msukuma siku ya kwanza kunywa chai ya karafuu alipiga ukelele alihisi kawekewa tego,siku hizi kazoea hanywi chai bila karafuu na akienda kwao kwimba likizo lazima azibebe πŸ™‚ 😁😁😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…