Ninavyo mfahamu Msukuma hufanya yafuatayo;
View attachment 1819539
1- Hapendi makuu ukimchokoza anasema
Kaya ya Ng'wobha nayo Kaya ili siku ipite salama.
2- Hapendi Kesi, ukimdhurumu anasema
Maguzu Masese ili asipoteze muda wa kufuatilia mambo ya kesi badala yake afanye kazi.
3- Hapendi kuumiza moyo kwa Hasara iliyo tokea Akipata hasara anajipa moyo kwa kusema
Jatulwa Mbiti Jitatananhaga ili aepuke matatizo.
4- Hapendi kuzikweza ukimsimanga ugenini anasema
Ng'ombe Ngeni ikapamwaga na Deda wengine hapa husema don't disarrange the furniture while you still a guest. Nahuo ndo ustaarabu.
5- Ni mvumilivu hata kwenye swala la utafutaji akianza na mtaji mdogo hujipa moyo kwa kusema
Bhushi bumboli bhukakwililaga mu bhutongo hapa humaanisha haba na haba kujaza kibaba.
6- Hatoi siri hovyo hovyo ukimdadisi anasema
Kamwana mwambi kale Mung'oma ili kuepusha uchonganishi
7- Kipindi cha njaa huwafariji wana familia kwa kusema
Shilewa shidohe bhali bhakwele ili kuwaondoa hofo akijua baada ya dhiki faraja
8- Hana roho mbaya penye watu wengi na nafasi ndogo husema
Bhitogilwe bhatishitaga ili kujenga upendo na kutobaguana.
9- Hana hazira za karibu wala kukurupuka ukimchokoza anasema
Akulipa welelo huku akitafakari jambo la kufanya.
10- Anajua mambo yote duniani ni ubatili na yatapita akipatwa na jambo au wakati mgumu hujipa moyo kwa kusema
Ndoho tabhu
Hao ndo wasukuma ninao wafahamu hebu kama kuna Msukuma mtaje na adodoshe kommenti ya kisukuma na misemo mingine ya kisukuma