Llio 002
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,636
- 2,053
Habari wana jf, kichwa changu kwa muda mrefu kilikuwa kinawaza kufanya kitu kingine kwa ajili ya kuongeza kipato changu ( Alternative way of raising income) katika kuwaza kwangu nikafikilia kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza juisi ya muwa. Nafahamu wapo wafanya biashara wengi wanafanya hii biashara, lakini wengi wao wanatengeneza hiyo juisi ili inywewe na kwisha siku hiyo hiyo kwa maana kuwa haifadhiki na haichelewi kuharibika. Kinachoniumiza kichwa ni nini cha kufanya au cha kuweka ili hii juisi nitakayo itengeneza iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika? Lengo langu nitengeneze hizo juisi ili niwe naza paki kwenye chupa na kuweza kuuza madukani au supermarket.
Ombi langu nisaidieni kitu cha kuweka kwenye hizo juisi zangu ili ziweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.
Ombi langu nisaidieni kitu cha kuweka kwenye hizo juisi zangu ili ziweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.