Wadau kwa Hali ya mvua mwaka huu kilimo Cha mpunga chaweza kuwa na manufaa,nataka kuwekeza mikoa ya shinyanga na tabora,ushauri kwenu Ni mda gani sahihi wakusia mbegu kabla ya kupanda-naweza mwaga mbegu nipande January mwishoni,ushauri wadau
Nadhani hujachelewa sana maana huku kanda ya ziwa watu wapo bize wamepanda na wanaendelea kupanda mpunga.Nakushauri tafuta mbegu ya muda mfupi tena inayohimili hali ya hewa yaukame kiasi maana sidhani kama miezi mitatu ijayo kutakuwa na mvua mikoa hiyo hivyo ni vema mpunga ungekuwa umeshapandwa ila kama una mbinu za umwagiliaji basi lima tu maana kama eneo lina maji ya uhakika mpunga ni simple tu.