USHAURI: Achana na fahari ya Vyeti vya Elimu, jikite kutafuta Ujuzi

USHAURI: Achana na fahari ya Vyeti vya Elimu, jikite kutafuta Ujuzi

Bon-CN

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2020
Posts
1,514
Reaction score
3,000
Naanza mada hii kwa kujadili hatua mbalimbali, ingawaje hatua moja inaweza isiwe na umuhimu kwa mwingine lakini ikawa chachu ya kujitathimini hatua uliyopo.

Wakati Upo Chuo.

Kwa sie masikini hatua hii ni muhimu sana katika kuandaa maisha yetu ya mtaani baada kumaliza chuo. Ukichanga karata zako vizuri kwenye hatua hii, unaweza kupunguza makali ya mtaa pale utakapochelewa kupata ajira. Hata hivyo, hapa nawalenga wale wanaopata posho ya chakula na malazi, maarufu kama "boom"!

Wakati upo chuo, hakikisha unaweka akiba ya angalau 50% ya “boom” kila unapota. Weka akiba kwa njia itakayokufanya ushindwe kuichukua kirahisi. Njia nzuri ni kufungua Akaunti ya Muda Maalumu (Fixed Deposit Account) kila unapopata “boom”! Kama una utalaamu kwenye bitcoin basi wekeza kwenye bitcoin kwa kutumia Cryptocurrency Exchange Markets zinazokuwa regulated na nchi za Magharibi.

Acha kutumia boom kwa kununua vitu kama tv, subwoofer au kufanya ndio mtaji wa kufanyia betting au forex trading. Vyote hivyo havitakusaidia mtaani. Na vitu kama betting ni kujitafutia uraibu (addiction) utakaokutafuna bila huruma hata kama utabahatika kupata kazi nzuri hapo baadae.
Jiepushe na pombe na anasa zisizo na tija. Hizo anasa utapiga sana ukishakuwa na maisha yako mtaani! Acha kuiga wanachofanya wenzako kwa sababu hujui maisha ya kwao yapo vipi. Sie wengine tumeshawahi kufanya kazi na watu ambao kila mwezi wanatumia pesa na wazazi wao ingawaje tayari wana mshahara wao!! Wakati nipo chuo nilikuwa na washikaji wawili ambao walikuwa hawajui hata boom ni kiasi gani na linaingizwa wakati gani!!

Wewe mwenzangu mimi, wakati upo chuo ni hatua ya kuweka akiba itakayokusaidia kuanzia maisha mtaani.

Baada ya Kumaliza Chuo.

Kwa ulimwengu wa leo ni kosa la kiufundi kumaliza chuo na kuingia mtaani wakati huna kompyuta. Hivyo, matumizi ya awali ya akiba uliyoweka kutokana na boom ni kununua PC yenye angalau RAM 4GB, HDD 500GB. Kwa wale wanaoishi Dar es salaam kwa kupanga, unatakiwa kuchagua eneo linaloendana na maisha yako ya kuwa "jobless" lakini usipange mahali kwa mazoea!

Katika hatua hii, hakikisha unachagua maeneo ambayo vyumba ni bei nafuu, na pia ni rahisi kwenda mjini hata kwa mguu pale unapokuwa umeishiwa kabisa. Pia hapo mtaani hakikisha unatengeneza mahusiano ya karibu na muuza bucha na mwenye duka linalopatikana bidhaa zote muhimu! Kama ulikuwa na Fixed Deposit Account (FDR), huu ndio wakati wa pesa iliyokuwa humo kuihamishia kwenye Akaunti ya Akiba! Kama ulikuwa na FDR zaidi ya moja, usikombe zote kwa pamoja!

Acha pesa yako kwenye Akaunti ya Akiba na sio kwenye simu! Achana na mambo ya Mobile Banking; yaani usijisajiri kabisa! Kwenye simu weka pesa ya matumizi madogo madogo tu! Kama una akiba ya kutosha, basi lipa kodi ya mwaka mzima. Kama umepanga chumba mahali ambapo wapangaji mnachanga kulipa umeme, basi lipa angalau wa miezi 6 kwa mkupuo. Vile vile unachotakiwa kufanya kila mwezi ni kupiga mahesabu ya chakula (unga na mchele), maharage, na nyama!! Kama unatarajia kwa mwezi utakula kilo 2 za nyama, basi mwachie rafiki yako muuza bucha (mshirikishe na mmiliki wa bucha) pesa ya mwezi mzima! Fanya hivyo hivyo kwa rafiki yako wa dukani.

Ukifanya hayo hapo juu itakusaidia kupangilia maisha yako bila ya "stress" kwa sababu umelipa kodi mwaka mzima, na pia unao uhakika wa mlo! Na kama huwezi kupika, jifunze sasa!

Sio hivyo tu, kitanda na godoro vinakutosha sana! Kingine unachotakiwa kuwa nacho ni meza ya PC na kiti! Acha gheto lako lionekane halina kitu kwa sababu hiyo huenda itakusaidia kuona aibu kuleta watoto wa kike ghetto! Watoto wa kike nao ni vimeo tu kwa mtu anayetafuta maisha!! Ni kimeo sio tu katika kumgharamia hata kwa vitu vidogo, bali mnaweza hata kutiana ujauzito; kitu ambacho ni "luxury" isiyohitajika kabisa katika harakati zako za kujipanga!

Elon 1.png


Udemy 2.png
 
Jikite Kwenye Kutafuta Ujuzi Mpya, Na Sio Vyeti.

NI kweli kwamba umemaliza chuo na kupata digrii au diploma, lakini hiyo haitoshi!! Chunguza kuona soko la ajira binafsi na ajira rasmi linataka nini! Tafuta ujuzi wa ziada kwa kuangalia mapenzi yako, na kwa kuangalia kinachohitajika kwenye soko la ajira binafsi na ajira rasmi!!! Haiingii akilini kwa mfano, umemaliza Bachelor in Accounting lakini hujui kutumia "accounting package" ya aina yoyote ile! Hapa unatakiwa kujifunza matumizi ya packages kama vile Quickbooks, Xero, na zingine kama hizo!! Unamaliza vipi na kutunukiwa Shahada ya Uchumi wakati hujui hata kutumia angalau SPSS?

Niliyosema hapo juu ni chachu tu, hususani kwenye harakati za kutafuta ajira ya ofisni. Ninacholenga hapa ni kuhamasisha watu kutafuta ujuzi wa ziada unaoweza kubadili hata mwelekeo wako wa ajira!! Kusoma na kutunukiwa Shahada ya Uhasibu pale UDSM au SAUT sio kifungo cha kukufanya usiwe Web Developer! Kusoma BSc. Electrical Engineering sio kifungo cha kukufanya usiwe Graphic Designer au hata Sales Person.

Tafuta ujuzi wa ziada kwa kuangalia soko linataka nini, na sio kuwekeza nguvu zote kupata kile kinachoendana na vyeti vyako ambayo si ajabu havijakupa ujuzi wowote zaidi ya "better grades"! Kwa dunia ya sasa, huna haja ya kurudi kwenye chuo cha aina yoyote ili kupata hayo. Na ukichanga karata zako vizuri, amini usiamini, usishangae ukakuta ni huu ujuzi wa ziada ndio unakutoa kimaisha kuliko vyeti vyako! Na kwa hilo linaweza kufanywa hata na yeyote; yaani hata kama umemaliza Kidato cha IV au cha VI ili mradi una uwezo wa kuelewa lugha ya Kiingereza.

Na wakati wa kutafuta ujuzi huu usihangaika kufahamu kama utapata cheti au hapana! Muhimu hapa ni UJUZI na sio cheti. Cheti kingekuwa na umuhimu huo kwa maisha haya, basi asilimia kubwa ya wahitimu wangekuwa na ajira!!! Na hapa simaanishi watu waachane na elimu rasmi, bali nahamasisha namaanisha kama kile ambacho CEO wa Tesla, Elon Musk alipata kukisema:-
There’s no need even to have a college degree… at all, or even high school. If somebody graduated from a great university, that may be an indication that they will be capable of great things, but it’s not necessarily the case. If you look at, say, people like Bill Gates or Larry Ellison, Steve Jobs, these guys didn’t graduate from college, but if you had a chance to hire them, of course that would be a good idea.


Elon Musk aliitoa kauli hiyo mwaka 2014, na mwaka 2020, akarudia kauli sawa na hiyo

Elon 1.png


Tweet hiyo ya Elon aliitoa wakati Kampuni ya Tesla ilipokuwa imetangaza nafasi za kazi, na akawa anahamasisha watu waombe hizo kazi hata kama hawana shahada ya chuo! Anachosema Elon ni kwamba, unaweza kuomba na kufanya kazi Tesla hata usipokuwa na shahada ya chuo kikuu ya taaluma husika! Anachohitaji kutoka kwako ni kuthibitisha kwa vitendo kwamba unao uwezo wa kufanya kazi husika, na sio vyeti vyako! Unaweza kuajiriwa na Tesla bila kujali kama umemaliza Havard, MIT, au umehitimu kupitia “YouTube University”! Uthibitisho wako kwamba unaweza kufanya kazi husika utatokana na portifolio yako (nitajadili baadae). Portifolio yako itakuwa ndio tiketi ya wewe kuitwa kwenye usaili!

Kwa watu ambao hawajajikita sana mitandaoni kutafuta fursa wanaweza kudhani Elon alikuwa anaichangamsha Twitter tu. Hata hivyo, kwa watu wa mitandaoni, hususani wanaofanya kazi kama Freelancers, hawa wanafahamu Elon amemaanisha alichosema kwa sababu huko kwenye kazi za Freelancing, ni nadra sana kuulizwa vyeti vya elimu! Huko wanachojali ni uthibitisho tu kwamba unaweza kufanya kazi husika!

Jinsi ya Kupata Ujuzi.

Hapa nazungumzia kupata ujuzi kwa njia ya mtandao, na kujifunza ujuzi huo wewe mwenyewe, au ukiwa pamoja na marafiki zako wenye mtazamo sawa. Ujuzi utakaopata utaweza kuutumia kwa njia mbalimbali kama vile kufanya kazi kama Freelancer au kujiajiri. Wakati unaangalia ni kitu gani unaweza kujifunza zingatia mambo makubwa mawili:
  • Mapenzi yako kwa fani husika, na
  • Urahisi wa kuitumia fani husika katika kujiingizia kipato.
Ukisoma fani unayoipenda, utapata msukumo wa kujifunza zaidi na zaidi, na kujitengea muda wa kutosha kwa sababu unasoma unachokipenda. Lakini pia ni muhimu kuhakikisha unachosoma kitakusaidia kukuingizia kipato kwa sababu msingi wa mada ni namna gani unaweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi uliojifunza mwenyewe mbali na elimu yako rasmi.

Kuna mengi unayoweza kujifunza kwa njia ya mtandao. Miongoni mwa kozi/fani unazoweza kujifunza ni pamoja na: Web Design, Web Development, Graphic Design, Coding, Computer Programming, Uhandisi, Social Science, Mapishi, Digital Marketing, na karibu kila fani unayoifahamu!
 
Vyanzo Vya Tutorials.

Coursera


Huenda Coursera ikawa ndio chanzo bora zaidi kwa mtu anayetaka kutafuta ujuzi bila cheti. Ili kuhakikisha ubora wa kozi zinazotolewa hapa, Wakufunzi wa Coursera wanatoka kwenye vyuo bora kabisa vya Marekani na duniani kwa ujumla, pamoja na taasisi zilizojikita kwenye nyanja husika, kama vile Google, na Amazon. Si kila mtu anaweza kupeleka kozi zake Coursera kama ilivyo kwa vyanzo vingine.

Changamoto kubwa ya Coursera ni gharama ya kozi zao ukilinganisha na kipato cha wengi wetu. Mbaya zaidi, malipo ya kozi za Coursera ni kwa mwezi, na kwavile ni ngumu kumaliza kozi ya ukweli kwa mwezi mmoja, basi utaona hadi kumaliza kozi mzima mtu utakuwa umetumia pesa nyingi sana. Hata hivyo, kuna kozi kadhaa zinazotolewa bila malipo. Tofauti pekee kati ya hizi kozi za bure na zile za kulipia mara nyingi ni cheti. Yaani, kozi yenye maudhui (contents) yale yale inaweza kuwa 100% Free lakini hupati cheti, na hiyo hiyo unaamua kulipia kwa sababu tu ya cheti!

KUMBUSHIO LA MADA: Achana na Fahari ya Vyeti vya Elimu; Jikite Kutafuta Ujuzi.

Edx

Edx ni chanzo kingine, na sifa zake zinafanana na sifa za Coursera hapo juu. Kama unachohitaji ni ujuzi na sio cheti, basi utakutana na kozi kibao unazoweza kusoma bila kulipia! Aidha, wakati Coursera ilianzishwa na Maprofesa wa Stanford University, moja ya vyuo vikuu bora kabisa nchini Marekani na duniani kwa ujumla, Edx ilianzishwa na Chuo Kikuu cha Harvard na Massachusetts Institute of Technology (MIT). Na Wakufunzi wanaotoa kozi hapo Edx ni wale kutoka vyuo vikuu bora kabisa, ikiwamo Harvard na MIT!

NOTE: Kama nilivyosema hapo juu, unaweza kusoma kwenye hivyo vyanzo 100% FREE lakini hutapata cheti. Lakini kama unataka kozi ya kulipia ili upate cheti, anza kwanza kusoma kozi husika kwa plan ya bila malipo, na ukishajiona umeilewa vizuri ndipo jisajiri kwa malipo ili kupunguza gharama.

Udemy

Udemy ndiyo chanzo maarufu zaidi kwa elimu za mtandaoni!! Kupitia Udemy, unaweza kusoma fani mbalimbali; hata utengenezaji wa filamu, na Mapishi ya Kihindi!! Changamoto kubwa ya Udemy ni kukosekana kwa udhibiti wa watoa kozi. Yeyote, hata wewe unaweza kupakia kozi yako Udemy!! Kwa maana nyingine, hii nayo ni fursa ya kujiingizia kipato kutokana na fani au taaluma unayoifahamu.

Hata hivyo, suluhu ya changamoto hiyo ni kuangalia watu wangapi wamejisajiri kwenye kozi husika, na “review/rating” ya kozi ipo vipi. Kama namba ya rating ni kubwa, na idadi ya watu waliofanya hiyo review ni kubwa, basi tunatarajia kozi husika itakuwa na ubora.

Chukulia mfano wa kozi ifuatayo:

Udemy 2.png


Hapo utaona wanafunzi 472,248 wamenunua hiyo kozi, na miongoni mwao, wanafunzi 110,186 wamei-review, na kwa ujumla wameipa 4.7/5 (94%! Katika hali ya kawaida, hatutarajii kozi kama hiyo ikose ubora kwa sababu huwezi kuwanunua zaidi ya watu 100,000 kutoa maoni mazuri kuhusu kozi yako!

Changamoto nyingine ni gharama kwa sababu asilimia kubwa ya kozi za Udemy ni za kulipia, ingawaje pia unaweza kupata “introductory courses” bila malipo. Hata hivyo, gharama ya kozi za Udemy ni nafuu mno, na utalipia kozi husika mara moja tu! Na uzuri zaidi, kozi za Udemy mara kwa mara huwa wanatoa punguzo. Kwa mfano, wakati ninapoandika haya, bei ya The Complete JavaScript Course 2021: From Zero to Expert, au QuickBooks Online 2021 Full Course Bookkeeping Accounting (ni muhimi sana hii kwa waliosoma Accounting vyuoni), kila moja bei yake ilikuwa $89 lakini saa 24 baadae, kozi hizo zinauzwa kwa $11.9.

Hata tuisheni ya complete O-Level History pale Mchikichini huwezi kupata kwa hiyo bei!!

YouTube

YouTube ni chanzo kingine unachoweza kupata “tutorials” za fani na kozi mbalimbali bila malipo. Lakini kama ilivyo kwa Udemy, changamoto kubwa ya YouTube ni ukosefu wa udhibiti, na kwahiyo yeyote anaweza kupakia kozi. Changamoto nyingine ni kwamba; hata zile kozi zenye ubora, zingine hutolewa kama Beginner’s Course kwa lengo la kuifanyia "marketing", ili ukivutiwa nayo kiasi cha kutaka kwenda hatu ya juu, basi utalazimika kulipia ili kupata full course.

Pamoja na yote hayo, zipo pia kozi zinazotolewa kuanzia hatua ya Beginners to Advanced Level bila malipo yoyote.

Jinsi ya Kupata Kozi Yenye Ubora Kupitia YouTube

Unaweza kupata kozi zenye ubora kwa kuchunguza mambo yafuatayo:-

Mmiliki wa YouTube Channel:

Zipo taasisi zinazoaminika ambazo hutoa kozi mbalimbali kupitia tovuti zao, na pia wana YouTube Channel wanazotumia kupakia baadhi ya kozi zao. Aidha, kadri unavyopata uzoefu, utakutana na watu binafsi wanaopakia kozi zenye bora mkubwa!

Kwa wale wanaokusudia kusoma IT, Coding, Computer Programing, Software Development, Web Design na Web Development, na kozi zingine sawa na hizo, wanaweza kutumia tutorials za vyanzo vifuatavyo: Free Code Camp, Edureka, Intellipaat, Simplilearn, na nyinginezo. Sasa tuseme unataka kusoma Web Development. Ukisha-type: Web Development Tutorials au Web Development Courses, utapata matokeo ya kozi husika kutoka vyanzo mbalimbali. Ukikuta channel husika ni moja kati ya hizo nilizotaja hapo juu, basi unaweza kuchangamkia na kuipakua kozi husika.

Views, Engagement, and Subscribers:

Baada ya ku-search kozi husika, pia unaweza kuangalia idadi ya Views, Subscribers, na comments kwenye kozi husika. Soma baadhi ya comments kuona watu wanasema nini kuhusu hiyo kozi. Katika hali ya kawaida, idadi kubwa ya hivyo vielelezo inaamanisha kufuatiliwa kwa channel husika. Na kama inafuatiliwa, na Views zipo nyingi basi inaweza kuwa ni ushahidi wa ubora wa hizo kozi.

NOTE:

Pamoja na video wanazopakia YouTube, ukiingia kwenye tovuti ya Free Code Camp utakutana na kozi kadhaa unazoweza kusoma huko (Web Pages) bila kulazimika kuingia gharama za kupakua video za YouTube. Pamoja na Free Code Camp, huduma kama hiyo ya kusoma kupitia kwenye tovuti unaweza kuipata kwenye tovuti zingine kama vile W3schools na Codecademy. Tovuti zote hizo, utasoma kwa kuanzia hatua ya awali kabisa! Kama ingekuwa unajifunza hisabati, basi wangeanza na wewe kwenye 1+1 hadi unafikia hatua ya kusoma Calculus!

Vitabu.

Nimeweka Vitabu kama chanzo cha mwisho lakini haina maana kipaumbele chake ni cha mwisho! Hata kama kwa vyanzo vya hapo juu utakuwa umepata kozi bora namna gani, lakini kama kweli unataka kubobea kwenye fani unayosoma basi ni lazima utumie na vitabu. Na kuna vyanzo mbalimbali unavyoweza kupakua vitabu vya fani mbalimbali bila malipo, na miongoni mwa hivyo vyanzo ni pamoja na pdfdrive.com, na Book Africa.
 
Jinsi Ya Kusoma Fani Yoyote Kama Ilivyoelekezwa Hapo Juu.
  • Kama huwezi usomaji wa peke yako, tafuta marafiki wenye maono kama yako, na kama hawapo, washawishi uwe nao. Mkikubaliana mtajiundia darasa lenu lisilo rasmi na kusoma pamoja kama mlivyokuwa mnafanya mashuleni/vyuoni. Idadi inaweza kuwa yoyote lakini nadhani itakuwa bora zaidi kama hamtazidi 5. Jadilini kwa pamoja kuangalia ni wakati gani mnaweza kukutana kwa urahisi. Hakikisheni mnatengeneza ratiba ya kusoma kwa pamoja na kuifuata ratiba hiyo kama ilivyo kwa elimu rasmi.
  • Video ambazo ni Beginners to Advanced Level zinaweza kuwa ndefu, kuanzia saa 10 na kuendelea!! Hapa usikimbilie kumaliza video husika kana kwamba unatazama tv series. Hapa unatakiwa kuelewa kile unachokisoma hatua kwa hatua! Hata kama kwa siku mzima itakuwa mmemaliza dakika 30 tu ya video yenye urefu wa saa 25, bado itakuwa bora zaidi kwa sababu kwa staili hiyo, itakuwa mmemaliza kozi husika kwa miezi miwili huku mkiwa mmeelewa vya kutosha.
  • Kama mmeamua kusoma kozi zinazohusisha mazoezi ya vitendo kama vile Computer Science, IT, Design, au kozi yoyote sawa na hizo, basi hakikisha kila wakati mnasoma huku mkifanya mazoezi mengi zaidi ya kile mnachokisoma. Ukitumia mtindo huo, utakuwa unamaliza video husika huku tayari ukiwa umepata uzoefu fulani wa vitendo.
  • Kama unasoma Coding, hakikisha unafanya mazoezi mengi zaidi, na kushiriki kwenye coding challenges. Kadri utakavyokuwa unasoma, utaelewa nazungumzia nini na ufanye nini katika kushiriki hizo coding challenges.
  • Use Your Common Sense.
NOTE: Vyanzo hivyo hapo juu ni sehemu tu ya vyanzo kadhaa unavyoweza kutumia kupata tutorials za fani mbalimbali.

Jinsi ya Kuonesha (Kujiuza) Uwezo Wako kwa Waajiri na/au Wateja (How To Showcase Your Skills To Prospective Employers and/or Prospective Clients).


Mwajiri wa kwanza kabisa kwa ujuzi uliopata ni wewe mwenyewe! Kama umesoma Web Development & Web Design, unaweza kuanzisha huduma za kutengeneza websites na blogs. Aidha, unaweza pia kusoma Search Engine Optimazation (SEO), na kuanza kuwa blogger mwenye ujuzi wa kutengeneza blogs zako wewe mwenyewe kwa namna upendayo. Na kwa kutumia utaalamu wako wa SEO, bila shaka utakuja kuwa Blogger mwenye mafanikio! Aidha, kupitia huko huko kwenye blogging utaweza pia ku-market utalaamu wako kama Web Developer.

NOTE: Huhitaji kusoma Web Development & Web Design ili kuwa Blogger. Ili kuwa Successful Blogger ni muhimu zaidi ukijifunza Search Engine Optimazation. Aidha, itakuwa bora zaidi ukiongezea na Social Media Marketing pamoja na Content Marketing. Kozi zote hizo unaweza kuzimalisha ndani ya muda mfupi tu.

Kwa upande mwingine, kama utapenda kufanya kazi kama Freelancer, kumbuka Clients huko kwenye "freelancing platforms" watahitaji zaidi kuona ushahidi wa uwezo wako wa kufanya kazi husika kuliko kujua umesoma wapi, au kuhitaji vyeti vyako. Hapa sasa ndipo unapotakiwa ku-showcase uwezo wako!! Kama umesoma Web Development & Web Design, Graphic Design, au fani yoyote, basi rudi hata JF na kutoa ofa ya kuwafanyia watu kazi hata bila malipo ili mradi tu ofa yako wewe iwe ni ujuzi wako tu. Kama kuna gharama zingine kama vile za hosting, basi gharama hizo ziingiwe na mwenye kuitaka hiyo website. Akishalipia gharana za hosting, hapa tumia ujuzi wako wote kutengeneza website yenye ubora!

Ukishatengeneza websites kwa mtindo huo hata 3 tu, tayari utakuwa umepata uzoefu wa kazi halisi, na pia utakuwa na cha kuonesha kwenye portifolio yako. Na hayo yawe ndo makubaliano yenu na uliyemtengenezea.

Kama ulichosomea ni vitu kama Graphic Design, Animation, na mambo mengine kama hayo, basi hakikisha unatengeneza hata "simple blog" kwa kutumia njia kama Website Builder ambayo aihitaji utaalamu wowote zaidi ya kufuata tu maelekeo. Hapa utatumia blog husika kuonesha (ku-post) kazi mbalimbali ulizotengeneza kwa ajili ya ku-showcase, au ulizotengeneza bila kulipwa kama ilivyo mfano wa kutengeneza website niliotoa awali.

Unakuwa na blog ya kuonesha hizo kazi kama alivyofanya huyu, au huyu. Kwahiyo mtu kama Elon anaposema anaweza kukuajiri hata kama huna digrii, anachotarajia kutoka kwako ni wewe kumuonesha portfolio kama hizo kabla hujaitwa kwenye usaili. Akisharidhika na portifolio yako, wala hana muda wa kujua hayo maujanja umesomea wapi au vyeti vyako vipo wapi! Na hicho ndicho kinachoendelea kwenye freelancing.

Jinsi ya Kutumia Ujuzi Uliopata.

Mbali na kuamua kutumia ujuzi wako kwa kujiajiri, Online Freelancing ni sehemu nyingine inayoweza kuwa ya awali kuanza kutumia ujuzi wako mpya. Mitandao kama www.upwork.com, www.freelancers.com, au www.fiver.com ni sehemu mzuri kuanzia kutumia ujuzi wako kwa malipo. Kama portifolio yako niliyoshauri hapo juu inaonesha una uwezo wa kutosha, amini usiamini, hutachukua muda mrefu kupata kazi yako ya kwanza.

Jisajiri kwenye hiyo mitandao sasa, na usisubiri kupata ujuzi wako mpya! Kwa kujisajiri sasa utafaidika na mambo makuu mawili:

  • Unaweza kupata kazi hata kwa kutumia ujuzi ulionao hivi sasa, na hivyo kupata kipato kitakachokusaidia kusukuma maisha kipindi unatafuta ujuzi wa ziada, na/au
  • Itakusaidia kufahamu soko la ajira huko duniani linahitaji nini sasa kupitia ujuzi unaotafuta. Hapa namaanisha utakuwa unaona matangazo ya kazi yanataka nini hasa kutokana na kile unachosoma.
Vyanzo vya Ziada

Kwa watu wanaofikiria kusoma Graphic Design na kozi zinazoendana nayo, msisahau kutembelea YouTube Channel zifuatazo:-
 
content Iko Useful and applicable Kwa kijana anayetafuta namna ya kuwa professional and expert.
#be blessed
 
Back
Top Bottom