Nina plan za kusoma MBA-Project Management & Strategic management Kwenye hiki chuo cha African Nazarene University ambacho kipo Kenya Eneo linaitwa Ongata Rongai - Kajiado County. Naomba kufahamishwa yafuatayo
Je njia rahisi ya kufika Ongata Rongai kutokea Dar kwa usafiri wa basi ni ipi?
Je chuo hiki ni kizuri?
Je hoteli/Guest house/Hostel zilizopo karibu na Chuo hiki zina wastani wa bei kiasi gani kwa siku.
Kwa waliosoma kwenye hiki chuo naomba wajitokeze ili niwauulize mawili matatu.