Ushauri: Ana division four ya 29, akasomee nini?

Kuna fundi nilikuwa naongea naye alipita njia kama hii aisee kibongo bongo naweza kusema amejipata ana maisha fulani yanayoeleweka
Huyu dogo jinsia ni KE, anaweza kufanya Hii?
 
Veta kuna kozi nyingi tuu za ufundi mfano magari, umeme, computer, ujenzi:-[:-[ acha hizo unazozijua za kupika.
Mtoto wa kike wengine hawapend hayo mambo wanadhan ni za wanaume so nimempa simple option
 
Huyu dogo jinsia ni KE, anaweza kufanya Hii?
Sijaona mafundi mekanika wengi wa kike ila wapo...ushauri wa kuangalia kote ni mzuri Vocational Training ina uzuri wake pia ingawa jamii inaichukulia kama ni kimbilio la waliofeli lakini tunapoingia kwenye maisha yenyewe ndio unakuta wana fursa za kupata hela ya kujitosheleza kwa sababu jamii kubwa inahitaji zaidi utaalamu wao
 
Ahsante Mkuu
 
Famasia wanachukua hadi four ya 29?
Mfumo wa elimu yetu hauangalii hizo division bali ufaulu wa D 4 unaohusisha masomo ya sayansi. kwa maana hiyo Bio D, Chem D, Phy F, Engl F, Math F hawezi kusoma kozi ya afya. Lakini endapo hizo D zingine zingeangukia kwenye masom ya Hesabu na Physics angesoma vizuri kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…