#COVID19 Ushauri: Baba yangu amekaa na mtu anayehusiwa kufa kwa Corona

#COVID19 Ushauri: Baba yangu amekaa na mtu anayehusiwa kufa kwa Corona

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,297
Jamani hapa naomba ushauri huko kijijini kwetu kuna vifo vya ghafla huyu ni mtu kama wa sita, mtu anabanwa tu anaondoka
Sasa jana kazidiwa mzee wa jirani kabanwa tu na alikuwa haumwi alishindwa kupumua watu wakaitwa kumsaidia na kumuombea akiwemo baba yangu mzazi mwenye miaka 64, ( baba hana ugonjwa wowote afya yake ni njema) wakawa wanamsaidia baada ya muda akapelekwa hospital hata akufika akawa kafariki,.

Hiyo taarifa mimi imenikosesha raha, japo wao wanaichukulia poa nifanyeje wapendwa, mimi nipo mbali ila sijui cha kufanya hawa wazee hata hawachukui tahadhari jamani[emoji24][emoji24]

Napenda babangu bado namuhitaji sana,sina raha niambieni cha kufanya nimuokoe na huyu ibilisi corona
 
Sina amani kabisa Mungu naomba atende miujiza uwiii
Kwa kifupi ni kumuomba Mungu tu na ku-hope for the best! Wakati mwingine korona huwa ina tabia ya kufanya damu iwe nzito na kuziba mishipa ya damu. Nadhani kuna dawa huwa wanatumia kwa tahadhari inayoweza kusaidia hii hali isitokee. Nimeisahau jina ila pengine kuna madakta hapa watakushauri.
 
basi akachanje kama kazi rahisi
Chanjo inaanza kufanya kazi kidogo baada ya wiki 2 mpaka 3 baada ya sindano ya kwanza. Unachoma sindano ya pili na kukaa baada ya wiki 2 chanjo inakuwa iko kwenye level ya kiwango cha juu.
 
Ondoa hofu. take easy.
na usithubutu kumuambia kitu, maana utampanikisha.

ikatokea akaumwa na yeye.
USIMPELEKE HOSP.
NARUDIA USIMPELEKE HOSP
 
Daah mkuu mbona tungekua tushakufa wote sidhani kama ipo hivyo unavyodhania watu wanapeleka wagonjwa wa corona hospital wanapona na kurudi home wengine tunaugua na kupona bila hata kujua wala kupima ingawaje kujikinga za corona ni muhimu..barakoa na sanitizer
 
Jamani hapa naomba ushauri huko kijijini kwetu kuna vifo vya ghafla huyu ni mtu kama wa sita, mtu anabanwa tu anaondoka
Sasa jana kazidiwa mzee wa jirani kabanwa tu na alikuwa haumwi alishindwa kupumua watu wakaitwa kumsaidia na kumuombea akiwemo baba yangu mzazi mwenye miaka 64, ( baba hana ugonjwa wowote afya yake ni njema) wakawa wanamsaidia baada ya muda akapelekwa hospital hata akufika akawa kafariki,.

Hiyo taarifa mimi imenikosesha raha,japo wao wanaichukulia poa nifanyeje wapendwa, mimi nipo mbali ila sijui cha kufanya hawa wazee hata hawachukui tahadhari jamani[emoji24][emoji24]

Napenda babangu bado namuhitaji sana,sina raha niambieni cha kufanya nimuokoe na huyu ibilisi corona
Kijiji gani hicho ninyi ndo mnaozua taharuki.
 
Dah nimesoma Uzi nimecheka na nimefurahi

Baba hakupata hata mafua ,Glory to God [emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom