Rodwell mTZ
JF-Expert Member
- Nov 16, 2012
- 1,455
- 1,621
Ninayo heshima kubwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya kukuandikia barua hii fupi.
Kwanza kabisa hongera sana kwa kazi nzuri ya kuijenga taifa.
Lengo la barua hii ni kuhusu marufuku uliyoitoa dhidi ya bajaji zinazobeba abiria kutoka kituo cha Mbezi Luisi zikiwapeleka mjini, Manzese na kwingineko
Mimi nina ombi kwako nakuomba kama inawezekana uziruhusu ziendelee kubeba abiria kwa sababu zifuatazo:
(1) Mabasi ya mwendo Kasi hayana uwezo wa kumudu uwingi wa abiria waliopo katika barabara hii. Haswa wakati wa rush hours.
(2) Serikali yako tukufu ni hivi majuzi imetangaza,wananchi tuepuke misongamano isiyo na lazima ili kujikinga na ugonjwa wa COVID-19,kusema kweli Mheshimiwa bajaji zimepunguza sana misongamano kwenye Mabasi.
(3) Mheshimiwa, Mabasi ya mwendonkasi yanasimamisha kutoa huduma inapofika saa tano usiku,hii inanikimbusha ule usemi unaosemwa "ngoma ya kitoto haikeshi" yaani wakati ambapo shughuli za hili jiji zinaendelea Hadi usiku wa manane wao wanalaza Mabasi yao,nadhani wanakua wameishaingiza hesabu inayotakiwa,huwa kuna Mabasi ya mikoani huwa yamechelewa kufika pale kwenye stendi kubwa ya Mbezi,wageni wenye uwezo mdogo wa kukodi texi,bajaji hua zinawasaidia sana.
Mwisho Mheshimiwa Rais nakushukuru kwa kutumia muda wako kuisoma barua hii, naomba nikutakie mafanikio makubwa sana katika shughuli zako zote za kutuongoza.
Asante sana.