Ushauri - Biashara Kadi za Mialiko, michango n.k

arnolds

Senior Member
Joined
Oct 10, 2009
Posts
105
Reaction score
57
Amani kwenu wadau, natumaini wote mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu yenu kama kawaida.
wakuu naomba ushauri hapa, nafikiria kuanzisha biashara ya kutengeneza kadi mbalimbali kama za harusi, sendoff na nyinginezo. kwenye swala la design hamna tatizo coz naweza kudesign mwenyewe. nataka kufaham ni vifaa gani vingine nitakavyohitaji (zaidi ya computer ambayo naitumia ku-design)?..naomba kwa anayefaham anitajie pia na mahali ambapo vifaa hivi vinapatikana.

shukrani sana, na Mungu awabariki.
 
Kama unataka kutengeneza kadi ambazo ni nzuri zaidi hautakiwi kukurupuka mkuu nenda pale tahfif kama uko dsm kaangalie aina ya kadi walizonazo utajua ni nini kinahitajika

Lakini kwa kadi za kawaida unahitaji printer(laserjet)utahitaji mkasi,cutter,ribbon,transparent paper na samples za kadi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…