Ushauri: Biashara ya muziki

PAPAA JIWE

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
863
Reaction score
149
Habari Wakuu,

Nahitaji kufungua biashara ya muziki ili kukuza kipato changu na kutoa ajira pia.

Lengo ni kupiga muziki kwenye sherehe mbalimbali na misiba, kutoa matangazo ya aina mbalimbali mitaani na kadhalika.

Tafadhali naomba kupata ushauri ni vifaa gani natakiwa kununua, bei yake kama inajulikana, na namna bora ya kuendesha biashara ya namna hiyo.

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kuimba au unatafuta na waombaji?

Usinisahau kwenye Baraza Jipya.
 
Unajua kuimba au unatafuta na waombaji?

Usinisahau kwenye Baraza Jipya.
Hapana mkuu, mimi sijui kuimba, ila nataka niwe nakodisha vifaa vya muziki kwenye matukio mbalimbali. Hapo nitatoa ajira kwa DJ na kijana mwingine wa kusaidia kazi ndogondogo.

Kama kutakuwa na deal zaidi kutakuwa na ajira ya MC pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa MC mmoja yupo nafahamiana nae anakamata jukwaa hasa, ikifikia hatua ya mc nishtue nikupe namba zake

Usinisahau kwenye Baraza Jipya.
 
Sasa mkuu unaanzisha biashara hujui nini kinahtajika, kweli upo serioz ?

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Fanya utafit kwanza chief....ktk tafit zako utajua masoko, jinsi ya kuiendsha hyo biashara na pia utajua ni vifaa gan utahitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…