Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Jana waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu alitoa maelekezo kwa Lightness Shirima (22), mwanafunzi wa Chuo Cha Serikali za Mitaa (LGTI), Hombolo - Dodoma kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuchukua kitambulisho chake kilicho zuiwa kutolewa kutokana na kushindwa kulipa deni la tsh 9M la matibabu ya baba yake aliye fariki dunia July 4 mwaka huu.
Kwenye andiko lake, Mh. Waziri anakiri uwepo wa gharama kubwa kwenye upatikanaji wa huduma za afya kwenye zama hizi cha maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Aidha, uhalisia wa gharama za kupata bima za kawaida kwa watanzania ni mkubwa sana. Mfano, gharama za kukata kifurushi cha chini kabisa cha bima kutoka NHIF ni tsh 192,000/= kwa mtu mmoja ambapo huduma nyingi hauwezi kuzipata. Kifurushi hiki huitwa Najali afya.
Vifurushi vingine pia vya ngazi ya chini kabisa ambavyo huitwa wekeza na timiza huwa na gharama za tsh 384,000/= na 516,000/= mtawalia, vyote vikihusisha mtu mmoja pekee. Pesa hii huongezeka kulingana na idadi ya watu, utegemezi wao pamoja na aina ya matibabu.
Ni pesa ndogo kwa wenye nacho, ni kubwa sana kwa namba kubwa ya watanzania hasa inapotolewa mara moja.
Lazima tukiri kuwa siyo watu wote hawana uwezo wa kukata bima hizi. Changamoto nyingine kubwa ni elimu ambayo haijatolewa kwenye jamii kuhusu umuhimu wa watu kuwa na bima za afya.
Sheria ya bima ya afya kwa kila mtu iletwe haraka. Hii imekuwa ni ahadi ya serikali kwa muda mrefu sasa. Itasaidia kuepusha adha kubwa inayojitokeza kwa sasa ambapo wanachi wengi wamekuwa wanashindwa kumudu gharama za sasa.
Utaratibu huo ambao utaruhusu kuchangiana kidogo kidogo kwa manufaa ya umma kwa ujumla utakuwa ni mwarobaini katika kuokoa jahazi hili ambalo linaelekea kuzama sasa.
Nashauri pia gharama za bima hiyo pindi itakapo huishwa iwe ni ndogo na rafiki, pia iweke utaratibu utakaopunguza ukakasi, kero na urasimu wa sasa uliopo katika kupata huduma za afya kwa watu wenye bima.
Kuna kina Lightness wengi sana mtaani wasio na sauti. Tumemsaidia huyu mmoja, vipi kwa wale wengine wenye changamoto hii wasio na sauti?
Turekebishe sera zetu za afya sasa ili ziwe na manufaa kwa kila mtu.
Elimu inayohusu umuhimu wa watu kuwa na bima ya afya utolewe sasa, pia sheria ya bima kwa wote iletwe haraka.
===
Kuhusu Lightness Soma Waziri wa Afya, tunakuomba usiishie kwa Lightness tuu, tupo lukuki ambao vitambulisho vyetu vya NIDA vimeshikiliwa Mloganzila Hospitali