Ushauri bora wa kuhifadhi tunda aina ya Parachichi

Matukutuku

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
269
Reaction score
126
Wakuu nimekuwa nikipata tabu sana na namna ya kuhifadhi Parachichi kwenye friji pale unapoyakata na kushindwa kula ukiamini kwamba ukiweka kwenye friji kesho yake yatakuwa fresh, lakin badala yake huwa yanakuwa meusi kwa juu, ukitaka kuyala mpaka uondoe huo ukoko mweusi ndo uweze kula.

Sasa nilitaka kujua ni kwa namna gani tunatakiwa kuhifadhi maparachichi yasioze au yasitoe hiyo utando mweusi, au haitakiwi kabisa kuweka kwenye friji?

Au labda hutakiwi kununua maparachichi mengi yaliyoiva, kwamba unatakiwa ununue machache ya kula siku hiyo hiyo??

jee kuweka parachichi kwenye friji ni sahihi au la?

Ushauri jamani.
 
Sio sahihi kujuwa zaidi mungu pekee!!
 
Usiweke kwenye Friji hilo Tunda weka mahali penye hewa pasipokuwa na joto kali.
 
Kwani kwenye friji kunajoto?acha fix kaka.

Hakuna joto kaka ha ha ha haaaa, nilikuwa sijui namna ya kuhifadhi hilo tunda ukishalikata. Upo hapo? Na bila shaka umepata eeeelim ya kutosha hapa.
 
acheni kunitamanisha jamani...nakumbuka parachichi na mihogo au wali maharage, utamu wake ni balaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…