Ushauri: Bustani ya Miti ya Matunda katika Nyumba

Ushauri: Bustani ya Miti ya Matunda katika Nyumba

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Habari wakuu,
Hembu wazoefu wa kilimo,nipeni ushauri huu.

Kwanza angalizo la mwazo:-

Miti hiyo ni kama decoration,badala ya kuwa na mauwa kwenye Nyumba,nimeamua iwe ni Royal Fruits House of my dream.
Kwahiyo sio kwa biashara.Ni matumizi ya inhouse or just friend wataotembelea na pia neighbors .

Niliipenda hii maana niliikuta Kenya,kuna biz man mwenzangu yeye alijenga house ana courtyard kubwa kiasi alipanda fruits trees kwa mfumo mzuri sana.Na alipoimaliza na kuipangisha basi ananiambia Customers wengi walikuwa attracted na miti ya matunda,licha ya kwamba alikuwa na ziada ya Swimming pool na Tennis Court.So,alikuwa pesa tamu sana kwa wa Russia Waliokodi waliokuwa attracted na mfumo wa nyumba,na huyu jamaa alinipa Idea na kuniambia kwamba dunia inabadilika.
Na mfumo alioutumia ni kwamba alinunua kiwanja kisha akapanda miti,then after two years akaanza kujenga,so in 3 years miti yake ikawa imeanza ku bear fruits.

Naomba mnijuze sasa wazoefu.

Mie nimelist miti hii hapa chini,ningependa kujua kwanza kama hakuna miti yenye allergy na mwenzie(hahaha).

Najua swali linalofuata ni kujua ardhi,ufupi itakuwa Kigamboni au Chanika ndiko ambapo ninaplan kutia team January kuchukua eneo.
Pia nina plan kama ardhi haita suite baadhi ya mazao,niliona Kenya wanahamisha udongo na kuweka kwenye pot,au kuongezea chini ili ku suite zao husika,maana altitude inaonekana haina athari kubwa sana.

-Je mazao hayo yanaweza kuwa pamoja
-Kwa wazoefu,ni ukubwa gani wa eneo natakiwa niwe nao kwa miti yote hiyo.Just for trees tu,maana ukubwa wa House,swimming pool,tennis Court(converted to Basketball pitch and Volleyball pitch) ukubwa wake ninao tayari.

-Ushauri mwingine wa ziada pia unakaribishwa

List hapa chini ila mwenye ziada anaweza kuongeza

Aina ya mti na idadi yake

1)Miembe 2
2)Mipera 2
3)Avocado 1
4)Michungwa 2
5)Michenza 2
6)Ndimu(Lime) 2
7)Lemon 1
8)Komamanga 2
9)Shokishoki(Rambutan) 2 -3(Imependekezwa na mdau idadi iwe mitatu by bintikikongwe
10)Minazi 6 (Kitamli,kwa madafu tuu)
11)Michikichi 4 (Lengo ni kuvutia ndege na viota vyake)

12)Apples 6 (Hii imefelishwa moja kwa moja na wadau waliotangulia
13)Stafeli 3
14)Bilimbi(mbilimbi) 2
15)Topetope(Custard Fruit) 2
16)Carambola 2
17)Minanasi 10
Ziada nimeyopata kwa mdau humu Chaula Rich
Naongeza
18)Fenesi(Jack Fruit) 1
Ziada ya mdau chuma cha rel
19)Bungo Tree 2
20)Mipapai 6
Ziada ya mdau Rolandi
21: Pilipili,miti 10 au 20 ya aina tofauti

Ziada kwa mdau
Kingmairo
22:Zambarau 1 (umefelishwa na bintikikongwe kwa kuwa unachukua eneo kubwa sana unless kuwe na ya kisasa
23:Mangosteen 2 : (imependekezwa na Bintikikongwe)
24:Mitufaa (malay apples) 2: (imependekezwa na Bintikikongwe)

Miti tiba:
Karafuu 2
Mironge 2
Mkunazi 1
 
Ongezea na Fenesi,Limau,Piches na Matunda damu.

Asante kaka
Lemon nimeweka kwenye list
Matunda damu,hapa naona kama kila mkoa wanaita matunda damu ila ukiyaona yanakuwa tofauti,ila najua ni aina ya berries lakini sijajua ni yapi mkuu.
Kuhusu Piches,hili zao zilijua kaka
Fenesi,hili nilikuwa nafikiria kuwemo kwenye list.Nimeliweka,asante sana
 
Ongeza na Mabungo...ila mjomba kuna tunda moja maarufu sana kama tiba kwa watu wanaokosa choo umerisahau PAPAI
 
Ongeza na Mabungo...ila mjomba kuna tunda moja maarufu sana kama tiba kwa watu wanaokosa choo umerisahau PAPAI

Aisee yaani kweli kuna siku mtu unaweza kuondoka nyumbani ukasahau kuvaa hata chupi
Hahaha,maana nimestuka sana kusikia nimesahau mabungo,wakati ni miongoni kwa Juice maarufu huku Zanzibar hadi kwenye mahoteli makubwa.

Papai nimelitoa ila litakuwepo,nimelitoa kwakuwa linachukua muda mfupi,so halina presha sana na ninawez akulichomekea wakati nimefix structure ya eneo.Ila litakuwepo na Pia hata nanasi nitaweka.

Shukran kaka nime ongezea Bungo juu hapo,asante sana
 
hyo idea ht mm ninayo kitambo mkuu,,ukishafanikisha ntaomba mrejesho,kila la heri
 
Asante kaka
Lemon nimeweka kwenye list
Matunda damu,hapa naona kama kila mkoa wanaita matunda damu ila ukiyaona yanakuwa tofauti,ila najua ni aina ya berries lakini sijajua ni yapi mkuu.
Kuhusu Piches,hili zao zilijua kaka
Fenesi,hili nilikuwa nafikiria kuwemo kwenye list.Nimeliweka,asante sana

Pichesi zinapatikana sana Mikoa ya Njombe,Iringa na Mbeya,kuhusu matunda damu sisi tumezoea kuyaita hivyo hivyo.
 
Japo unazungumzia sana fruits lakini si mbaya ukaongeza pilipili, hata kama hutumii tukija sisi zitatufaa
 
Japo unazungumzia sana fruits lakini si mbaya ukaongeza pilipili, hata kama hutumii tukija sisi zitatufaa

Hahaha,asante mkuu,najua wewe ndugu yake dharumendra.Nime ongeza mkuu,maana najua hizi hazichukui nafasi,zinaweza kupandwa hata chini ya mti mwingine.
Shukran
 
hyo idea ht mm ninayo kitambo mkuu,,ukishafanikisha ntaomba mrejesho,kila la heri

Asante kaka mrejesho lazima nitauleta,na ndio maana nataka kwanza nipate mawazo ili nijue nachukua eneo ukubwa gani.
Yaani niliingia nyumba ya huyu Mshkaji Pale Kisumu,niliganda,yaani ananiambia nyumba hii haina mngojwa wa upungufu wa vitamins,matunda yanapishana kwa msimu,so lazima tu kila siku matunda yaliwe.Na alipowapangisha jamaa alikula pesa nzuri mno.Na main attraction ilikuwa ni Fruits Garden.Na ndio aliniambia ni bora ninunue eneo nje ya mjini ili in years to come,watu watajua nini maana ya kuchukua eneo kubwa na ku build dream Fruits Garden House.
 
Ongeza zambarau na zabibu

Asante Kingmairo.
Zambarau ni Idea nzuri pia,nimeongezea pale mkuu,ila Zabibu inashida kidogo kwenye kuchukua eneo la utambaaji na uangalizi wa karibu.Mazao niliyo plan ni yale ambayo hayachukui muda saana kwa mutu kufanya uangalizi.Ila nitategemea ideas nyingine namna ya upandaji wake,kama linaweza kifit kutambazwa na miti mingine.
Ila Zambarau nimekubali nimeliweka kaka.
Halafu lazima niweke na First Aid kit,maana mizambarau naiju,ilituvunja sana watu miguu aisee.
Yaani unapanda kwenye mti,kila ukijongea unaona unakaribia kushika zambarau mara mti kwaaa,chini.Hahaha

Angalia hawa hapa chini kwa utam wa Zambarau wameona wapande juu ya lorry aisee
attachment.php
 
Attachments

  • IMG_3563.JPG
    IMG_3563.JPG
    57.4 KB · Views: 902
Asante kaka mrejesho lazima nitauleta,na ndio maana nataka kwanza nipate mawazo ili nijue nachukua eneo ukubwa gani.
Yaani niliingia nyumba ya huyu Mshkaji Pale Kisumu,niliganda,yaani ananiambia nyumba hii haina mngojwa wa upungufu wa vitamins,matunda yanapishana kwa msimu,so lazima tu kila siku matunda yaliwe.Na alipowapangisha jamaa alikula pesa nzuri mno.Na main attraction ilikuwa ni Fruits Garden.Na ndio aliniambia ni bora ninunue eneo nje ya mjini ili in years to come,watu watajua nini maana ya kuchukua eneo kubwa na ku build dream Fruits Garden House.

yani ni bonge ya idea,,inshort hyo nyumba hakuwez kuwa na mgonjwa wa aina yyte ile labda awe hatak mwenyew kula hayo matunda,,tena yanakuwa fresh kabisa sio ya kusubir kutoka tanga au sauzi
 
yani ni bonge ya idea,,inshort hyo nyumba hakuwez kuwa na mgonjwa wa aina yyte ile labda awe hatak mwenyew kula hayo matunda,,tena yanakuwa fresh kabisa sio ya kusubir kutoka tanga au sauzi

We,acha na wazungu wanataka fresh,yaaani waliikodi fasta kwa pesa ya ajabu.Yaani alipangisha nyumba bei kubwa ni sawa na mtu yupo Chanika anapangisha nyumba bei ya Masaki.Maana ukiwa kwenye Courtyard yake wala huwezi jua kama upo eneo hilo,maana Simming pool,outdoor gym,Tennis Court mabayo imekuwa designed kwa alama maalum ambazo zinewza kuwa converted to Basket ball and volleybal pitch,na vyote full equipped.Membea za watoto kwa kiwango kidogo kulinagana na ukubwa wa nyumba,ambao ni 4 bedroom house. Yaani ni eneo la kawaida tu kama Chanika mkuu,ila ukiingia kwenye eneo la ndani ni balaa.

Maana anasema cha mwanzo wakati anawapa wateja wake briefing cha mwanzo walivamia miembe na michungwa,kula saana,walimpongeza sana kwa great Idea yake,ndio jamaa aka share na mie na kuni encourage kwamba flowers garden zinapitwa na wakati kwa dunia inapoelekea.Hata kama una uchochoro basi panda mti wa matunda na sio kujaza ma hibiscus

Na hili naliona huku Zanzibar,ukipogea wazungu Airport,wengi wanakuambia uwapitishe market wakanunue matunda,wanakuambai fresh kwao hakuna,na wengine wanakuambia kabisaa kwamba tangu wanazaliwa wanakula matunda ya kutoa mbali ambayo yanadawa kali sana na utam sio halisi.
Kuna Mjerumani alikula nanasi huku anakuambia taste ni tofauti saana na aliwahi kula kwenye maisha yake yote,basi kila siku anapita pale sokoni anachukua.Ila cha ajabu ananiuliza mie nimekula lini nanasi,namuambia wiki tatu zilizopita tena kipande,alicheka sana
 
Habari wakuu,
Hembu wazoefu wa kilimo,nipeni ushauri huu.
-Je mazao hayo yanaweza kuwa pamoja
-Kwa wazoefu,ni ukubwa gani wa eneo natakiwa niwe nao kwa miti yote hiyo.Just for trees tu,maana ukubwa wa House,swimming pool,tennis Court(converted to Basketball pitch and Volleyball pitch) ukubwa wake ninao tayari.

-Ushauri mwingine wa ziada pia unakaribishwa

List hapa chini ila mwenye ziada anaweza kuongeza

Aina ya mti na idadi yake

1)Miembe 2
2)Mipera 2
3)Avocado 1
4)Michungwa 2
5)Michenza 2
6)Ndimu(Lime) 2
7)Lemon 1
8)Komamanga 2
9)Shokishoki(Rambutan) 2
10)Minazi 6
11)Michikichi 4
12)Apples 6
13)Stafeli 3
14)Bilimbi(mbilimbi) 2
15)Topetope(Custard Fruit) 2
16)Carambola 2
17)Minanasi 10
Ziada nimeyopata kwa mdau humu Chaula Rich
Naongeza
18)Fenesi(Jack Fruit) 1
Ziada ya mdau chuma cha rel
19)Bungo Tree 2
20)Mipapai 6
Ziada ya mdau Rolandi
21: Pilipili,miti 10 au 20 ya aina tofauti
Ziada kwa mdau Kingmairo
22:Zambarau 1

Miti tiba:
Karafuu 2
Mironge 2

Hiyo ni idea nzuri. Mimi kwangu nimefanya hivyo, nimepanda aina nyingi ya miti ya matunda na sasa yana mwaka wa pili hivi. Mingine tayari imeanza kuzaa (mipapai, mipera, carambola).

Ila ningekushauri miti ifuatayo uwe na hadhari:
-Michikichi ni ya nini kwenye yard? Ikiwa utapenda labda panda mmoja au miwili tu.
-Apples haziwezi kuota kwenye joto, zinahitaji kipindi cha baridi katika ukuaji wake, sawasawa na peaches na plums (matunda damu)
-mishoki shoki hebu cheki nadhani unahitaji mitatu (ulizia kama iko dume na jike tafauti.... ni vyema ukaenda kituo cha utafiti kizimbani kupata usahihi zaidi). Pia upate aina ya 'nyama peke yake' - ulizia kwa wenye mishoki shoki aina hii maeneo ya Mwera.
-mangosteen (ulizia kizimbani) matunda yake ni safi sana.
-miembe panda ile midogo ya kisasa.
-mitufaa (malay apples) iko mekundu na meupe. Ni mizuri kuipanda karibu na nyumba
-minazi chukuwa kitamli (ya madafu) ndiyoo mizuri karibu na nyumba. Ile mirefu (east african tall) yana changamoto zake, kwani nazi ikidondoka kutoka juu ni hatari.
- mzambarau, mkunazi au mkwaju kwa nyumba ya kawaida inakuwa mikubwa sana, labda kama utakuwa na shamba.

Ingependeza zaidi ukiacha sehemu ndogo kwa ajili ya kupanda mazao ya bustani - mchicha, matembere, nyanya, pilipili na vyengine vya msimu

Kuhusu spacing kwa miti aina ya mifenesi, miparachichi unatakiwa angalau iwe mita 5 x 5, na itapendeza zaidi ikiwa utapanda kwa mistari.
 
Asante kaka kwa ushauri,Ubarikiwe.
Michikichi
nimeweka kama attraction ya viota vya ndege na ndege wenyewe pia ili kuwe na mvuto kwa aina nyingi za ndege,naweza kuipunguza ikawa 2.
Apples,
nitaziondoa kwenye list kwa ushari wako
Mishokishoki -
Nitapitia Kizimbani kupata ushauri wa kitaalam,na nitaongeza kuwa mitatu kwa ushauri wako
Mangosteen
Ubarikiwe nimeongeza kwenye list,na pia nitapitia Kizimbani kwa ushauri
Miembe:
Hii ni ya Kisasa
Mitufaa(Malay Apple)
Ubarikiwe kwa ushauri,maana mie nipo huku fuoni Zanzibar,ipo kibaoo na inakivuli kizui kweli,maana majani yake mapana kama Mshokishoki.
Nimeongeza kwenye list
Minazi:
Nitachukua kitamli ndio plan yangu,maana lengi ni kwa madafu na sio nazi za kupikia,asante kwa msisitizo
mzambarau, mkunazi au mkwaju
Hii nayo changamoto,nimeliona hili,nita edit lits yangu
Maana sidhani kama kuna mizambarau au mikwaju ya kisasa,yoote nikiona ni mikubwa saana.

Kuhusu kuwa na eneo la mboga mbona ipo considered kaka,ni muhim pia sana

Kuhusu Spacing:
Hili ndio muhim sana ili nijue nachukua akubwa gani,na ndio maana nasubiria list ya mazao itimie na ushauri wenu kama huo then niweze kupata zaidi uelewa wa spacing.
Maana ndio itafanya kupendeza kwa madhari husika
 
Halafu wakati naenda ku edit list.
Ningependa kwanza pia kujua,maana kumbe mimeo nayo inatongozana hadi iwe na jike na dume?

Maana kuna ushauri wa bitimkongwe

Je nikipanda mti mmoja hautaweza kuzaa hadi nichanganye na angalau aina moja ya mti dume kwa upevushaji?

Back
Top Bottom