USHAURI: CCM msiwasahau 'wazee' wa Dar es salaam,katiba mpya itambue uwepo wao!

USHAURI: CCM msiwasahau 'wazee' wa Dar es salaam,katiba mpya itambue uwepo wao!

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Mbio za kuelekea kwenye upatikanaji wa katiba mpya zimeshika kasi, ambapo hivi sasa tupo kwenye hatua ya mabaraza ya katiba kuipitia rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti Mhe.Joseph Sinde Warioba. Yote tisa, kumi ni vimbwanga vinavyofanywa na viongozi na makada wa CCM kupinga baadhi ya mapendekezo ya tume kama uwepo wa serikali tatu na madaraka ya rais na kuweka msimamo wa chama badala ya kusisitiza mjadala wa kitaifa kuwaunganisha wananchi wenye mawazo tofauti. Nje ya hayo yote, nimeona ni vema nikawashauri CCM Kuwakumbuka wazee wa Dar es salaam kwenye kikatiba mpya. Wazee hawa wamekuwa msaada kwa CCM na serikali kwa ujumla ambapo Rais wa JMT ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amekuwa anakimbilia huko kuomba ushauri, maoni na pengine kutoa taarifa mbalimbali pindi masuala magumu yatokeapo mathalani njaa,mgomo wa madaktari,walimu n.k Najua hamna haja na wazee wa Mbeya,Tanga,Mwanza, n.k. Acheni siasa, watambueni wazee hawa mnaowatembeza juani!
 
Back
Top Bottom