Ushauri: Course ya Engineering ya kusoma

Hongera kwa matokeo mazuri mkuu. Hakika ulitulia sana ukiwa Advance, Naona una focus nzuri hivyo ningependa nikupe ushauri mzuri pia.

Binafsi nimesoma Computer engineering na nimejiajiri na maisha yanaendelea.

Ushauri wangu kabla haujachagua course ni lazima ujiulize maswali yafuatayo;

1. Course unayoichagua ni kwa sababu unaipenda au ni kwa sababu ya kutafuta tu ajira na maisha yaendelee?
Hili swali lina umuhimu mkubwa sana maana kama ukichagua course kwa sababu ya kuipenda lazima mafanikio utayaona tu mkuu, maana walioanzisha hizo courses waliona fursa za jamii kupitia hiyo course hivyo ina umuhimu. Ila ukichagua course kwa sababu ya kupata ajira kwa haraka ni vema ila mambo yanabadilika leo hii course unayodhani ni dili au ipo marketable baada ya miaka mitatu au minne inaweza isiwe marketable kwa kiwango iliyopo kwa sasa. Passion ni muhimu sana.
Ukichagua kitu unachokipenda utakifurahia, utakifuatilia, utafaulu vizuri bila shaka. Unaweza ukabakizwa chuoni kama TA, Tutorial Assistant siku moja. Maisha ya chuo ni maisha ya kuyafurahia mkuu.

2. Chuo gani kinatoa hiyo course?
Chuo ni muhimu sana katika kuangalia course ya kusomea, Vyuo vyote vina wataalamu waliothibitishwa na wana weledi kwa kile wanachofundisha. Ila ni muhimu kuangalia historia ya chuo na course husika especially engineering course, apply kwenye chuo chenye uzoefu wa mda mrefu na hiyo course ili utoke na elimu iliyo-jitosheleza, baadhi ya vyuo vinaanzisha course mpya, usiwe wa kwanza ukatumiwa kama majaribio. Nenda kwenye vyuo vyenye uzoefu wa mda mrefu hasa vya serikali.

3. Kupitia course hiyo uwezekano wa kujiajiri upo?
Hapa kwetu mitazamo ni tofauti sana ukihusisha swala la kujiajiri na kuajiriwa. Kuajiriwa kwa mtazamo wangu ni vema zaidi hasa kwa kijana ambaye huna uzoefu na ni fresh from school ila kujiajiri ni dhana nzuri zaidi. Hivyo chagua course ambayo unaweza ukaajiriwa au la ukajiajiri hata baadaye kama ukibahatika kupata ajira mapema.

COURSE ZA ENGINEERING AMBAZO NI NZURI NA MARKETABLE

1. Mechanical Engineering
2.Chemical Engineering
3.Computer Engineering
4.Civil Engineering.
5. Industrial Engineering
6.Environmental Engineering
7.Architectural Engineering
8. Telecommunication Engineering
9. Electrical Engineering
10. Electronics Engineering
 
Fuata huu ushauri na hiyo kozi ya kwanza hapo juu ndio iwe chaguo lako la kwanza kila la kheri Mdogo wangu....
 
Ahsante kaka kwa ushaur mzuri
 
Mkuu tunazungumza mambo tunayoyajua vyema kwa sababu tumeyaishi.
Mkuu, stashahada na Shahada yangu vyote nimesoma DIT tena in recent years, nikishuhudia madogo wa form six wakitukimbiza sisi wa diploma kama kawaida na wakiyaelewa masomo vizuri kabisa. Tofauti ni kwamba wa Diploma anasoma miaka mitatu na wa form six minne.
 
Ni sawa mkuu. Lakini ule mwaka wa kwanza(General Course) kwa hao wa kidato cha sita hauhesabiki popote. Unakuwa nyongeza tu.
 
Ulikuwa kozi gani pale nyumbani mkuu?
 
Hiyo ni foundation course.
Lakini kwa vyuo vingine, kama University of Dar es Salaam, Ardhi University, University of Dodoma na St.Joseph University huo mwaka wa kwanza unakuwa included pia. Huoni kwamba ni vyema wakaenda huko ili waonekane dhahiri wamesoma semester 8 na si semester 6?.

Usichoke kunifafanulia mkuu.
 
Habari wana JF mimi ni mhitimu wa kidato cha sita 2018 na nimepata ufaulu wa div 1points 4 Yaani:-
PHYSICS-A
CHEMISTRY-B
A/MATHS-A
Naomba mwenye ufahamu wa engineering course ambazo zko marketable kwa sasa anisaidie.
Natanguliza shukrani
Kwanza bro hongera sana kwa ufaulu mzuri.

Sababu ndio una anza chuo au unataka uanze chuo,mimi nakushauri soma ELECTRICAL ENGINEERING.
 
Habari wana JF mimi ni mhitimu wa kidato cha sita 2018 na nimepata ufaulu wa div 1points 4 Yaani:-
PHYSICS-A
CHEMISTRY-B
A/MATHS-A
Naomba mwenye ufahamu wa engineering course ambazo zko marketable kwa sasa anisaidie.
Natanguliza shukrani
Electrical Engineering,Telecom&Electronics,IT&computer science,kama unapenda vitu vya umeme,au piga Civil engineering
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…