USHAURI: Epuka Makosa haya 10 Kabla ya kumiliki Chombo cha Moto

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
Salam wana Jukwaa.

Rejea kichwa cha habari. Gari ni chombo cha usafiri kinachomwezesha mwanadam kutoka sehem moja kwenda nyingine kwa haraka. Chombo hiki kikitumiwa ndivyo sivyo kinaweza kuchangia kumgharimu mmiliki na kuathiri shughuli zake za maendeleo.

Kikitumiwa vizuri kina nafasi kubwa ya kuinua uchumi wa wa mmiliki kwani chombo hiki ni mashine ambayo humwezesha mwanamdamu kuzalisha kwa kua kinampa tulizo la akili tofauti na akitumia usafiri wa umma, humjengea kuaminika katika biashara zake, humfikisha kwenye shughuli zake ndani ya mda na kumuwahisha kupumzika, uhuru wa kutoka sehem moja kwenda nyingine bila kikwazo chochote n.k

Zingatia haya kabla hujaamua kumiliki gari, au kama una gari basi endelea kuyazingatia yafuatayo ili pesa uliyotumia kuagizia gari yako isipungue kwa kasi.

1. Fanya Service/Matengenezo madogo na makubwa ndani ya mda. Matengenezo madogo namaanisha kubadiri oil ya injini na gia box ndani ya mda, kusafisha chekeche la hewa na ukaguzi wa mfumo wa breki. Matengenezo makubwa hujumuisha hayo madogo na vitu kama kubadiri shock ups, bearings, joints, bush, au kitu chochote kinachohitaji mabadiriko kwenye gari lako. Ukiweza kufanya hivi, gari yako itabaki kwenye ubora wake siku zote na itakuepusha na madhara makubwa zaidi yanayoweza kukugharimu fedha na hata uhai kwa kuchelewa kushughulikia matatizo haya ndani ya mda.

2. Kagua gari yako kila asubuhi kabla ya kuanza safari. Ukaguzi unaosemwa hapa ni wa vitu kama kiwango cha oil ya injini na gia box, maji ya katika rejeta, upepa na nati za matairi na taa zote za break na kubwa. Iwapo oil imepungua kutokana na kuvuja kwa baada ya gari kujigonga kwenye sample katika mashimo tunayopita, utapata nafasi ya kuchukua hatua stahiki, kama nati zililegea utapata wasaa wa kuzikaza, iwapo taa zitakua hazifanyi kazi utaweza kuzibadirisha na hivyo kukuwezesha kufanya mawasiliano mazuri na watumiaji wengine wa barabara hivyo kukuepusha na ajali n.k Imekua ni kawaida ya sisi watanzania tulio wengi kuhisi kwamba gari jipya halihitaji ukaguzi wa mara kwa mara na hivyo tunajiweka kwenye hatari pasipo sisi wenyewe kujua ambayo inaweza kugharim pesa na hata uhai wa mtumiaji na watumiaji wengine wa barabara.

3. Usipite kwa mwendo kasi njia yenye mashimo. Kuna ka utamaduni kanajengeka sana kwa baadhi ya sisi watanzania tunaotumia vyombo vya moto kutaka kukimbia hata sehem ambazo ni za kwenda mwendo wa kawaida tu, mwingine anapita njia ya vumbi kwa mwendo mkali bila kujua analegeza bodi pamoja na vifaa vingine katika gari yake kwa sababu ya mtikisiko mkubwa unaokuwepo garini humo. Hii ni sawa sawa na unapomuazima mtu leo gari akae nalo siku 2 lakini anaporejesha unakuta imekua tofauti sana, vivyo hivyo hata kama wewe hutumii chombo hichokwa ustaarabu basi uwezekano wa kukiharibu ni mkubwa na hivyo waweza kulazimika kuingia gharama ambazo hukuzipanga na mwishowe inaweza kufanya gari yako ionekane mbovu na kushushwa thamani.

4. Usafi wa gari yako ni muhim. Mwonekano nadhifu wa ndani na nje ya chombo chako hufanya thamani yake isishuke kwa kasi tofauti na mtu ambae hasafishi gari yake mara kwa mara, lakini pia kwa waopita njia zenye tope, unapochelewa kusafisha matope chini ya gari yanayonasa kwenye mabati, kuna uwezekano mkubwa gari yako ikashika kutu na hivyo kuharibu maeneo husika. Lakini pia ni muhimu ukajitahidi kutoshusha vioo mara kwa mara ili vumbi lisiingie ndani na kuchafua roof, dashboard, pamoja na njia za AC, iwapo matundu ya AC yatachafuliwa kuna uwezekano mkubwa sana gari yako ikashushwa thamani wakati unahitaji kuuza....binafsi ninayekuandikia hapa, niliuza gari nilotumia kwa miaka 5 kwa bei sawa na niliyonunulia kwa sababu tu ilikutwa iko vizuri kila kitu ila AC na usafi wa Dashboard ulimpa mteja yule amani ya moyo kwamba gari imetunza vizuri.

5. Egesha gari sehem zenye usalama na nafasi ya kutosha. Kwa wakazi wa Dar es Salaam, parking imekua ni changamoto na mara nyingi tunalazimika kuegesha magari kwa kusogeleana sana, madhara yake ni kwamba unapoegesha gari kwenye kona nyembamba au eneo ambalo gari zinasogeleana sana uwezekano wa kukwanguliwa na madereva wengine ni mkubwa. Iwapo gari yako itakwanguliwa mara kwa mara itakulazim kupiga rangi mara kwa mara na ikifika kipindi unataka kuuza mnunuaji ataona gari imepigwa sana rangi hivyo ataishusha thamani kwa kigezo hicho.

6. Weka mafuta kutoka vituo vya mafuta na uchukue risiti. Hii ni njia moja wapo ya kuikinga injini yako na wauzaji wa mafuta wa reja reja wasio waaminifu ambao hununua mafuta na kuyachanganya ili wajipatie faida zaidi na hivyo kuiweka gari yako katika hatari ya kuharibu injini. Jambo hili kwa miji kama Dar es Salaam limepungua sana siku hizi ikilinganishwa na baadhi ya mikoa ambapo wakati mwinginevituo vya mafuta viko mbali hivyo kuwalazim watu binafsi kulangua mafuta na kuyauza reja reja, madhara yake pia yanaweza kua kwenye uchafu unatuama katika madumu hayo ambao unaweza kudhuru pampu au chekeche la tank kuziba.

7. Usizoee kumuachia gari mtu mwingine. Hii ni kwa sababu kila mtu ana utunzaji wake wa chombo, yawezekana kukawa kumetokea tatizo asije kukwambia kwa kuhofia kua utamchukulia kama muharibifu, lakini pia iwapo mtu huyu atapata ajali kama ni gari binafsi, kampuni za bima wanaweza kuamua kutokukulipa kwa kua sheria haimtambui mtu uliyemuazimisha gari, hua wanalipa katika kudumisha uhusiano mwema na wateja wao.

8. Jizoeze kutobeba watu au mzigo kubwa kupita uwezo wa gari. Kila gari imewekewa kiwango cha uzito ambao unapendekezwa kubeba, inapotokea mzigo ni mkubwa zaidi unadhuru mfupo wa shock up, balance inakua sio nzuri barabarani na pia inakulazim kutumia mafuta zaidi kwa kua gari inakua nzito.

9. Kanyaga mafuta taratibu huku ukiacha gari yako ichanganye yenyewe. Hii ni kwa wale wanaoamini mbio inamfikisha haraka aendako, mtu anakamua gari kwa mfano katika jiji la Dar es Salaam ambalo lina changamoto ya foleni za hapa na pale akienda hatua chache mbele unamkuta kasimama wala hakuna alichowahi, bila kujua unakua unajiumiza kwenye matumizi ya mafuta, unapokanyaga mafuta na mshale wa RPM ikanyanyuka sana ndivyo ambavyo ulaji wa mafuta hufanyika kwa kasi pia. Sehem ya kutumia lita 10, utajikuta umetumia lita 15 au zaidi na hivyo kukufanya uone gari yako inakula sana mafuta kumbe gari haina tatizo isipokua tatizo ni namna unavyokanyaga.

10. Usipuuze jambo lolote lisilo la kawaida katika gari yako. Mfano, kelele za vuma chini kama bush zilizoisha, shick ups, taa za onyo za kwenye dashboard n.k Yawezekana kabisa bush zikawa zimeisha na hivyo vyuma kugongana hivyo wakati unachukulia kawaida na kusubiri upate pesa ndipo ufanye marekebisho unakuja kukuta kumbe kuna vuma vingine vya muhimu vimekatika eneo hilo na hivyo gari yako kuhatarisha usalama wako na watumiaji wengine. Taa za onyo wengi tumekua tukizichukulia kama short ya umeme pasipo kufanyia uchunguzi kwa wataalamu na hivyom kujikuta tukipata matatizo barabarani.

Karibuni kwa maoni na ushauri zaidi au maswali.
 
0746267740
Kimomwe Motors Tanzania Limited--- Waagizaji wa magari kutoka Japan
Ahsante kuna madhara yoyote usipobadili shockups?
Sijui ndo shock absorber mnaita?..
 
Unazungunziaje matumizi ya Engine Oil kwa kilomita 10,000 badala ya zile Engine Oil kwa kilomita elf 3,000/5000

Majina siyajuii nmesahauu
 
Oil zinazoenda kilomita 10,000 zimetengenezwa kwa teknolojia hiyo na pia zinazoenda kilomita 3000/5000 ni maalum kwa umbali huo.

Mtengenezaji anaweza kua ni kampuni moja mfano Total akatengeneza zote 2, utazitofautisha kwa kusoma kwenye dum husika kwa kua mara nyingi hua zimeandikwa.

Cha msingi na muhim ni kwamba unapoweka oil inayoenda kilomita zaidi ya 5000 ni muhim pia uhakikishe filter itakayotumika ni ile original ya kuhimili hizo kilomita. Ukiweka oil filter ya kawaida mara nyingi hua inavujisha oil kabla ya hizo kilomita 5000/8000/10000
 
Ahsante kuna madhara yoyote usipobadili shockups?
Sijui ndo shock absorber mnaita?..
Usipobadiri shock ups madhara yake ya kwanza ni gari kukosa balance nzuri inapokua mwendo kasi na mbaya zaidi ni kulika kwa tairi upande mmoja, lakini pia usipobadiri mapema uzito unavyoelemea spring au koil spring unaweza kuikata na kuongeza gharama zaidi.
 
Wale ambao hatuna magari ndio tutakaouzingatia ushauri huu mzuri pindi tutakaponunua magari, wenye magari wako busy hawasomi huu uzi
 
KIMOMWEMOTORS hebu nishauri kwenye gari diesel engine ya cc3500 inaweza kutumia mafuta sawa na gari ya petrol engine ya 2000cc?
Hapana zina tofauti kidogo kiongozi, kwa wastani diesel hailiki sana kama petrol, na kwa uzoefu ni kua Cc 3500 inaenda kilomita chachr zaidi bila kujali kama hiyo Cc 2000 prtrol ni six au four. Cc 2000 kama ni four huenda wastani wa km 12 hadi 14 kwa lita, wakati Cc 2000 six huenda wastan wa km 10-11.5 kwa lita.

Wakati ile ya Cc 3500 diesel hua inaenda kwa km15- 16 kwa lita. Diesel ni mafuta mazito wakati petrol ni gas inayoyayuka
 
Usipobadiri shock ups madhara yake ya kwanza ni gari kukosa balance nzuri inapokua mwendo kasi na mbaya zaidi ni kulika kwa tairi upande mmoja, lakini pia usipobadiri mapema uzito unavyoelemea spring au koil spring unaweza kuikata na kuongeza gharama zaidi.
Hio beiii nlotajiwaaa ilibidi niondoke kwanza

Labda nkirudi inaweza badilika
 
Na kwa mfano gari ilikua chini sana ikanyanyuliwa kwa kuwekea 'spacer sijui spencer' mnaita wenyewe...
Je hii yaweza kuwa mbadala wa hizo shock ups?
 
Hapana boss, spacer haifanyi kazi kama shock up, yenyewe ni kipande kidogo kinachofungwa juu inapoishia shock kwa dhumuni la kunyanyua gari tu kidogo ili isiwe chini sana
 
Hio beiii nlotajiwaaa ilibidi niondoke kwanza

Labda nkirudi inaweza badilika
Pole sana, ndio changamoto hizo za gari, jaribu kutafuta kwa watu tofauti tofauti, ukishindwa kabisa vizuri uipaki gari kwa mda ili usiipatie madhara zaidi
 
Ahsante sana kwa ufafanuzi
Itabidi niweke tu maana..,
 
Salam wana Jukwaa.

Rejea kichwa cha habari. Gari ni chombo cha usafiri kinachomwezesha mwanadam kutoka sehem moja kwenda nyingine kwa haraka. Chombo hiki kikitumiwa ndivyo sivyo kinaweza kuchangia kumgharimu mmiliki na kuathiri shughuli zake za maendeleo.

Kikitumiwa vizuri kina nafasi kubwa ya kuinua uchumi wa wa mmiliki kwani chombo hiki ni mashine ambayo humwezesha mwanamdamu kuzalisha kwa kua kinampa tulizo la akili tofauti na akitumia usafiri wa umma, humjengea kuaminika katika biashara zake, humfikisha kwenye shughuli zake ndani ya mda na kumuwahisha kupumzika, uhuru wa kutoka sehem moja kwenda nyingine bila kikwazo chochote n.k

Zingatia haya kabla hujaamua kumiliki gari, au kama una gari basi endelea kuyazingatia yafuatayo ili pesa uliyotumia kuagizia gari yako isipungue kwa kasi.

1. Fanya Service/Matengenezo madogo na makubwa ndani ya mda. Matengenezo madogo namaanisha kubadiri oil ya injini na gia box ndani ya mda, kusafisha chekeche la hewa na ukaguzi wa mfumo wa breki. Matengenezo makubwa hujumuisha hayo madogo na vitu kama kubadiri shock ups, bearings, joints, bush, au kitu chochote kinachohitaji mabadiriko kwenye gari lako. Ukiweza kufanya hivi, gari yako itabaki kwenye ubora wake siku zote na itakuepusha na madhara makubwa zaidi yanayoweza kukugharimu fedha na hata uhai kwa kuchelewa kushughulikia matatizo haya ndani ya mda.

2. Kagua gari yako kila asubuhi kabla ya kuanza safari. Ukaguzi unaosemwa hapa ni wa vitu kama kiwango cha oil ya injini na gia box, maji ya katika rejeta, upepa na nati za matairi na taa zote za break na kubwa. Iwapo oil imepungua kutokana na kuvuja kwa baada ya gari kujigonga kwenye sample katika mashimo tunayopita, utapata nafasi ya kuchukua hatua stahiki, kama nati zililegea utapata wasaa wa kuzikaza, iwapo taa zitakua hazifanyi kazi utaweza kuzibadirisha na hivyo kukuwezesha kufanya mawasiliano mazuri na watumiaji wengine wa barabara hivyo kukuepusha na ajali n.k Imekua ni kawaida ya sisi watanzania tulio wengi kuhisi kwamba gari jipya halihitaji ukaguzi wa mara kwa mara na hivyo tunajiweka kwenye hatari pasipo sisi wenyewe kujua ambayo inaweza kugharim pesa na hata uhai wa mtumiaji na watumiaji wengine wa barabara.

3. Usipite kwa mwendo kasi njia yenye mashimo. Kuna ka utamaduni kanajengeka sana kwa baadhi ya sisi watanzania tunaotumia vyombo vya moto kutaka kukimbia hata sehem ambazo ni za kwenda mwendo wa kawaida tu, mwingine anapita njia ya vumbi kwa mwendo mkali bila kujua analegeza bodi pamoja na vifaa vingine katika gari yake kwa sababu ya mtikisiko mkubwa unaokuwepo garini humo. Hii ni sawa sawa na unapomuazima mtu leo gari akae nalo siku 2 lakini anaporejesha unakuta imekua tofauti sana, vivyo hivyo hata kama wewe hutumii chombo hichokwa ustaarabu basi uwezekano wa kukiharibu ni mkubwa na hivyo waweza kulazimika kuingia gharama ambazo hukuzipanga na mwishowe inaweza kufanya gari yako ionekane mbovu na kushushwa thamani.

4. Usafi wa gari yako ni muhim. Mwonekano nadhifu wa ndani na nje ya chombo chako hufanya thamani yake isishuke kwa kasi tofauti na mtu ambae hasafishi gari yake mara kwa mara, lakini pia kwa waopita njia zenye tope, unapochelewa kusafisha matope chini ya gari yanayonasa kwenye mabati, kuna uwezekano mkubwa gari yako ikashika kutu na hivyo kuharibu maeneo husika. Lakini pia ni muhimu ukajitahidi kutoshusha vioo mara kwa mara ili vumbi lisiingie ndani na kuchafua roof, dashboard, pamoja na njia za AC, iwapo matundu ya AC yatachafuliwa kuna uwezekano mkubwa sana gari yako ikashushwa thamani wakati unahitaji kuuza....binafsi ninayekuandikia hapa, niliuza gari nilotumia kwa miaka 5 kwa bei sawa na niliyonunulia kwa sababu tu ilikutwa iko vizuri kila kitu ila AC na usafi wa Dashboard ulimpa mteja yule amani ya moyo kwamba gari imetunza vizuri.

5. Egesha gari sehem zenye usalama na nafasi ya kutosha. Kwa wakazi wa Dar es Salaam, parking imekua ni changamoto na mara nyingi tunalazimika kuegesha magari kwa kusogeleana sana, madhara yake ni kwamba unapoegesha gari kwenye kona nyembamba au eneo ambalo gari zinasogeleana sana uwezekano wa kukwanguliwa na madereva wengine ni mkubwa. Iwapo gari yako itakwanguliwa mara kwa mara itakulazim kupiga rangi mara kwa mara na ikifika kipindi unataka kuuza mnunuaji ataona gari imepigwa sana rangi hivyo ataishusha thamani kwa kigezo hicho.

6. Weka mafuta kutoka vituo vya mafuta na uchukue risiti. Hii ni njia moja wapo ya kuikinga injini yako na wauzaji wa mafuta wa reja reja wasio waaminifu ambao hununua mafuta na kuyachanganya ili wajipatie faida zaidi na hivyo kuiweka gari yako katika hatari ya kuharibu injini. Jambo hili kwa miji kama Dar es Salaam limepungua sana siku hizi ikilinganishwa na baadhi ya mikoa ambapo wakati mwinginevituo vya mafuta viko mbali hivyo kuwalazim watu binafsi kulangua mafuta na kuyauza reja reja, madhara yake pia yanaweza kua kwenye uchafu unatuama katika madumu hayo ambao unaweza kudhuru pampu au chekeche la tank kuziba.

7. Usizoee kumuachia gari mtu mwingine. Hii ni kwa sababu kila mtu ana utunzaji wake wa chombo, yawezekana kukawa kumetokea tatizo asije kukwambia kwa kuhofia kua utamchukulia kama muharibifu, lakini pia iwapo mtu huyu atapata ajali kama ni gari binafsi, kampuni za bima wanaweza kuamua kutokukulipa kwa kua sheria haimtambui mtu uliyemuazimisha gari, hua wanalipa katika kudumisha uhusiano mwema na wateja wao.

8. Jizoeze kutobeba watu au mzigo kubwa kupita uwezo wa gari. Kila gari imewekewa kiwango cha uzito ambao unapendekezwa kubeba, inapotokea mzigo ni mkubwa zaidi unadhuru mfupo wa shock up, balance inakua sio nzuri barabarani na pia inakulazim kutumia mafuta zaidi kwa kua gari inakua nzito.

9. Kanyaga mafuta taratibu huku ukiacha gari yako ichanganye yenyewe. Hii ni kwa wale wanaoamini mbio inamfikisha haraka aendako, mtu anakamua gari kwa mfano katika jiji la Dar es Salaam ambalo lina changamoto ya foleni za hapa na pale akienda hatua chache mbele unamkuta kasimama wala hakuna alichowahi, bila kujua unakua unajiumiza kwenye matumizi ya mafuta, unapokanyaga mafuta na mshale wa RPM ikanyanyuka sana ndivyo ambavyo ulaji wa mafuta hufanyika kwa kasi pia. Sehem ya kutumia lita 10, utajikuta umetumia lita 15 au zaidi na hivyo kukufanya uone gari yako inakula sana mafuta kumbe gari haina tatizo isipokua tatizo ni namna unavyokanyaga.

10. Usipuuze jambo lolote lisilo la kawaida katika gari yako. Mfano, kelele za vuma chini kama bush zilizoisha, shick ups, taa za onyo za kwenye dashboard n.k Yawezekana kabisa bush zikawa zimeisha na hivyo vyuma kugongana hivyo wakati unachukulia kawaida na kusubiri upate pesa ndipo ufanye marekebisho unakuja kukuta kumbe kuna vuma vingine vya muhimu vimekatika eneo hilo na hivyo gari yako kuhatarisha usalama wako na watumiaji wengine. Taa za onyo wengi tumekua tukizichukulia kama short ya umeme pasipo kufanyia uchunguzi kwa wataalamu na hivyom kujikuta tukipata matatizo barabarani.

Karibuni kwa maoni na ushauri zaidi au maswali.

0746267740
Kimomwe Motors Tanzania Limited--- Waagizaji wa magari kutoka Japan

Nyongeza....

11. Unapofanya service au repair yoyote hakikisha unakuwepo mwenyewe uone kwa macho yako filter imetolewa imewekwa mpya, oil imemwagwa na imewekwa mpya, kila kitu kama ni shock absorber imewekwa mpya. Mtindo wa kumuachia fundi afanye service/repair na wewe kuondoka kwenda kukaa bar alafu anakuletea gari anakuambia "boss tayari kila kitu" achana nao kabisa. MAFUNDI HAWABADILI OIL FILTER WANAIFUTA WANAIRUDISHA HIYO HIYO, HATA SHORK ABSORBER WANAKUPIGA.

12. Ukiweza nunua vifaa/spare (original) unavyoviamini mwenyewe na UMSIMAMIE fundi avifunge. Ukigeuza mgongo utashangaa umenunua oil ya uhakika (eg.TOTAL) wanabadili dumu unawekewa oil fake. Umenunua filter original ya 18,000 unawekewa ya 5,000.

13. WHEEL ALIGNMENT ni muhimu sana (japo ni ghali, maeneo mengi DSM ni 60,000) kwa balance nzuri ya gari kwani inaondoa sterling kuvuta upande mmoja na kuzuia tairi la upande mmoja kula upande mmoja.
 
Back
Top Bottom