Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 7,621
- 12,505
Wakuu kwema
Enzi sijafunga ndoa nilizaa mtoto wa kiume na binti mmoja wa kiislam kutoka Tanga. Hatukua na mpango wa kuoana hivyo mtoto alipofikisha umri wa miaka miwili kasoro nikamchukua na kuishi naye mimi, na sasa ana miaka 12
Mama yake alifanikiwa kupata kazi serikali lakini hakubahatika kuolewa wala kupata mtoto tena. Kwa bahati mbaya sana Mungu amemuita, amefariki.
Ikabidi nimchukue niambatane na mwanangu kwenda mazishini Tanga. Mambo nilio yakuta huko sina hamu kabisa.
Kikao cha ukoo kikakaa kikateua msimamizi wa mirathi na wakati wa kikao ikaonekana kwakuwa marehemu ana mtoto mmoja tu na hana mume wala wazazi hivyo mali za Marehemu (mafao, Nyumba na kiwanja kigamboni) sehemu zitakua za mtoto wa marehemu BALAA LIKAANZIA HAPO.
Ikaonekana mimi nimeenda na mtoto makusudi ili turithi mali za marehemu, ndugu wakagoma kabisaaa.
Kuepusha shari nikasema jamani sisi tumekuja kuzika tu mali za marehemu fanyeni mnavyo weza ninyi, kuna baadhi ya ndugu wakagoma wakasema nikosa na mtoto akikua atakuja kudai mali za mama yake
Baada ya kujadiliana sana wakaja na agenda ya kwamba nimuache mtoto chini ya usimamizi wao ili sasa maliziwe chini yao na watamsomeaha hadi hatakapokuwa mkubwa. SIKUKUBALIANA NAO KABISA.
Msimamizi mwenye ni kaka yake mkubwa mtata balaa eti yeye ndio asimamie mali za marehemu na mtoto akae naye huko Tanga tena kijijini.
Mzozo ukawa mkwabwa nikaanza kutishwa hadi kurogwa, kesho yake asubuhi nikapanda basi nikatudi zangu Dar.
Bado natafakari nifanyeje. Akili inaniambia niwapotezee lakini nikimuangalia mwanangu naona ana haki na mali za mama yake
Ili kusiwepo na mzozo wataalamu wa sheria hii niende nayo vipi?