Ushauri: Hivi hii Kidini/ Kiimani/ Kitaalamu tunatatuaje?

Kuna vitu hujaviweka wazi ili uweze kupata ushauri muafaka.

Awali ya yote, hizo pesa unazipataja nikimaanisha umeajiriwa ama unafanya biashara.

Hayo matatizo yanayokuja ni ya aina gani na je yanajirudia kila upatapo pesa.

Tatu na kubwa zaidi je matumizi yako yanashabihiana na kipato unachoingiza?

Isije ikawa huna mishe ya maana ya kukuingizia pesa continuosly halafu unatarajia ukigumia pesa zitakaa.

Isije ikawa unaendekeza mambo ya kijinga kama vile kamari na pombe halafu unatarajia pesa isipuputike ghafla.

La muhimu zaidi isije ikawa unaingiza laki moja kwa mwezi huku maisha yako unaishi ya milioni kwa mwezi.

Mara nyingi kwenye swala la pesa kikubwa ni nidhamu ya matumizi. Usipothamini shilingi 100 kwa kukimbilia elfu 10, niamini hutokuja kukaa ukapata pesa. Hata milioni huanzia na shilingi mia.

Kuna mtu hapo juu ka comment kuwa umeelekeza fikra zako kwenye ushirikina, hakukosea. Huko ndio unaenda kumalizwa kabisa huku ukinufaisha waganga/mitume wa makanisa feki/ma ustaadh uchwara.

Mchawi mkubwa wa pesa zako ni tabia/nidhamu yako ya matumizi. Jichunguze kwanza.
 
Nidhamu ya pesa ni ugonjwa wetu kama hesabu tu za shule zilivo. Kwanini hii elimu haifundishwi sana wakati ndio msingi wa mafanikio ya kiuchumi?
 


Kijana,


Umenena vyema ….azifakar nondo hizo mchana na usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…