Ushauri huu kwa kanumba na kifo chake

kitalolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2006
Posts
1,827
Reaction score
708
HII NILIISOMA KULE GLOBAL NA HUWA KILA MARA NILIKUWA NIKIMWONA KANUMBA NAKUMBUKA HII NA MWISHO NILIPOSIKIA HABARI YA KIFO CHAKE NA CHANZO CHAKE STORY HII ILI- CLIK KWENYE KICHWA CHANGU

kanumba anahitaji tiba

Posted by GLOBAL on October 4, 2011 at 9:30am
View Blog

Madaktari wasema anaumwa Personality Disorder
Steven Charles Kanumba ni staa mkubwa Bongo. Jina lake kwa sasa lina hadhi ya kimataifa. Inawezekana akawa ndiye msanii kijana mwenye mvuto kijamii kuliko mwingine yeyote.

Mvuto wake unatambulika ndiyo maana makampuni mengi ya kibiashara na kijamii hupenda kumtumia kama balozi wao. Kanumba ni fahari ya Tanzania, ni kivutio cha vijana wengi wa kizazi kipya.

Lengo la makala haya ni kumshauri Kanumba. Pamoja na sifa nyingi alizonazo kuna makosa machache huwa anayafanya, hivyo anahitaji kupokea ushauri ambao utamsaidia kuepuka visa vya hapa na pale ambavyo humvunjia heshima.

MATATIZO NI NINI?
Hapa kuna baadhi ya matukio ambayo yamewahi kuripotiwa, hivyo kumchafua Kanumba, kwa hiyo anapaswa kujitenga nayo ili heshima yake ibaki kuwa juu.

MOSI: Ugomvi na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu mpaka kufikia hatua ya kupelekana polisi.
PILI: Sylvia Shally alikuwa mpenzi wake lakini naye waligombana mpaka kufikishana polisi. Mrembo huyo alitinga ubaoni akidai Kanumba alimtishia maisha.

TATU: Alizama kwenye dimbwi la mahaba (kama alivyodai mwenyewe) na Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed. Walipoachana, alifunguka kuwa mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, alikuwa anamtesa sana.
NNE: Anadaiwa kuwa na uhusiano wa siri na Aunt Ezekiel (ingawa wote wanakanusha), juzikati walitibuana, kisha yeye alimpa mitama mrembo huyo na kusababisha soo hilo litinge polisi.

ISHU IKOJE?
Kwa nini kila siku ugomvi na wanawake? Inakuwaje polisi na yeye kwa makosa ambayo yana alama za kimapenzi?
Daktari aliye pia bingwa wa saikolojia, Godfrey Chale aliiambia Showbiz kuwa tatizo linalomsumbua Kanumba linaitwa Personality Disorder na tiba yake ni ushauri na nasaha.
“Personality Disorder ina matawi mawili, inferior (kujihisi unyonge) na superior (kujiona unahitaji kuogopwa). Vitu hivyo hutengeneza wivu na migogoro mingi (conflicts).

“Mtu kama huyo atakuwa anajiona superior, kwa hiyo hujikuta ana chembechembe za dharau kwa kuamini ni maarufu na ni lazima mpenzi wake amnyenyekee. Ikiwa atakutana na hali tofauti, mfano akigundua mwenzi wake hafuati anavyotaka au anamsaliti, kwa kawaida hujisikia vibaya.

“Ile tabia ya kujiona superior ndiyo humfanya ashindwe kukubali matokeo hasi kutoka kwa mwenzi wake, kwani anaamini yeye ni mtu wa kunyenyekewa. Kutokana na hilo, ndiyo maana hupata kesi za kugombana au kusumbuana na wapenzi wake kwa sababu ya kutokubali matokeo,” alisema Dk. Chale ambaye ana hospitali binafsi, pia hutoa ushauri wa afya kupitia magazeti ya Global Publishers.

Dokta Patrick Mirumbe wa Hospitali ya Capricorn alisema: “Tatizo lake ni wivu. Hiyo naweza kuzungumza kwa kifupi na tiba yake ni ushauri na nasaha. Akipata ushauri wa kutosha anaweza kubadilika na kuwa mtu safi.

KANUMBA ASHIKE NINI?
Mwanasaikolojia ambaye hutoa ushauri wake kwenye magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota alisema kuwa jambo ambalo Kanumba anapaswa kushika ili kuepukana na vitu ambavyo vinaweza kushusha heshima yake ni kujitambua.

“Katika makundi ya saikolojia, lipo linaloitwa Legal Psychology. Hili linamtaka mtu atambue mazingira anayoishi na ufahamu wake. Kanumba anatakiwa ajijue yeye ni mtu maarufu na heshima yake ipo juu, kwa hiyo asipojitambua itakuwa tatizo sana.

“Namuomba Kanumba ajijue yeye ni nani, awe mwepesi kuepukana na shari ndogo ndogo ambazo mwisho wake huwa ni mbaya, kama kupelekana polisi. Nadhani akijitambua, akiwa mwepesi kuelewa dalili za ugomvi, ataweza kujirekebisha.
“Anaweza kwenda kwa washauri zaidi lakini hapa mimi nampa kitu muhimu zaidi na akishike. Anaweza kuishi kwa amani maisha yake yote bila migogoro. Akijitambua, hata anapoachana na wapenzi wake, amani itatawala na hakutakuwa na fujo za polisi,” Manyota.

HITIMISHO
Naamini kuwa maneno ya madaktari akiyashika sawasawa pia ushauri wa mwisho wa mwanasaikolojia Manyota, bila shaka atashinda mitihani inayomkabili. Lengo ni kuona heshima yake inazidi kupaa juu na msimamo ni kwamba Kanumba bila polisi inawezekana.

IMEANDIKWA NA LUQMAN MALOTO


MY TAKE: Tujaribu kuwa tunafwata ushauri wa wataalamu pengine leo tungekuwa tunaongea tofauti
 
mkuu naona unafanya kazi ya CSI!

Lawyer wa Lulu akiiona hii atafurahi sana........Lulu atashinda!!!

aisee
 
mkuu naona unafanya kazi ya CSI!

Lawyer wa Lulu akiiona hii atafurahi sana........Lulu atashinda!!!

aisee
Inategemea na credibility ya lulu pia,REFER kesi ya ubakaji ya DSK.pamoja na Dsk kuwa na allegations zingine France,but alishinda kesi ya Newyork
 
MY TAKE: Tujaribu kuwa tunafwata ushauri wa wataalamu pengine leo tungekuwa tunaongea tofauti



Ndugu yangu na wewe changanya za kwako kama mbayumbayu
je? ulitaka afe kifo gani?
agongwe na gari?.........bado utashauri
afe kwa ngoma?...........bado utashauri
afe kwa malaria...........
afe kwa ,,,,,,,,,,,,,,,,,



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…