SoC04 Ushauri huu ukitumiwa na serikali unaweza kupunguza madhara ya uvutaji sigara

SoC04 Ushauri huu ukitumiwa na serikali unaweza kupunguza madhara ya uvutaji sigara

Tanzania Tuitakayo competition threads

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Kwa mujibu wa utafiti wa umoja wa mataifa, kila baada ya sekunde 8 mtu mmoja hufa kutokana na madhara ya sigara.
Mwili_wa_mvutaji_sigara.jpg

📸Wikipedia

Sigara ina madhara makubwa sana katika mwili wa binadamu, lakini pamoja na hayo bado watumiaji ni wengi na mbaya zaidi uvutaji wa kiholela husababisha madhara hata kwa wasiovuta.

Hatari ya sigara zote za kawaida na za kielekitroniki kama shisha na zile ndogo ndogo portable

NINI KIFANYIKE ILI KUKOMESHA AU KUZUIA UVUTAJI SIGARA HADHARANI?

Bunge litunge sheria itakayoamuru wauza wa sigara kuwa na leseni ya kujitegemea kama ilivyo pombe na miamala kwa sasa.

USHAURI
Leseni hii iwe ghali ili wauzaji wawe wachache. Ili upate leseni ya kuuza sigara kwa rejareja lazima uwe umetenga eneo maalum la wavutaji sigara.

Ikiwa mfanyabiashara anataka kuomba leseni ya kuuza sigara mtumishi au mkaguzi wa serikali anapaswa kuja kukagua sehemu ya kuvuta kama ipo, iwe imejificha(isiwe wazi)

Baada ya sheria hii kupita itolewe notisi ya muda wa mwisho kwa wauzaji wa sigara kutenga eneo la kuvutia na ikiwa watashindwa basi usiuze sigara.

KWA WAVUTAJI
Ikiwa unataka kuvuta sigara hakikisha unaenda kwa muuzaji aliekamilika, ana leseni ana eneo la kuvutia iyo sigara.

FAIDA KWA JAMII NA SERIKALI
Kwanza jamii itaepuka madhara yatokanayo na moshi wa sigara, mazingira yatakuwa safi kutokana mabaki ya sigara (vichungi vyake kutokutapakaa ovyo) na serikali itakuwa imepata chanzo kipya cha mapato kutokana na utoaji huo wa leseni zake.

Mwisho kabisa kwa sababu ya masharti na vigezo kuwa vigumi huenda wavutaji wakapungua na hatari ya vifo vitokanavyo na madhara ya sigara yakaoungua toka sekunde 8 kwenda hadi siku.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom